Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Leo hapa Japani katika Chuo Kikuu cha Soka, kulikuwa na mashindano ya kutoa hotuba kwa lugha ya Kiswahili kuwania kombe la mwasisi wa Chuo hicho Daisaku Ikeda. Mashindano hayo yameandaliwa na Chuo hicho kwa uratibu wa mmoja wa wahadhiri wake Bi. Midori Uno. Haya ni mashindano ya 21 na yaliwakusanya wageni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Balozi wa Tanzania hapa Japani Bi. Salome Sijaona , na afisa wake , wawakilishi wa Balozi za Kenya na Kongo DRC pamoja na Shirika la Utangazaji la Japani-NHK WORLD. Ma-MC walikuwa mabinti wa wawili(Angalia picha hapo chini)... Jina moja limenitoka lakini wakulia ni Kiko Sawajiri..

Balozi Salome Sijaona aliongea mwanzoni mwa hafla hii (Pichani)kwa kueleza mafanikio ya kijamii, kisiasa na utamaduni yalivyofikiwa Nchini Tanzania na eneo lote la Afrika Mashariki kwa kukitumia kiswahili na kusema kuwa lugha hiyo sasa ni ya kimataifa hivyo inapaswa kuenziwa na kusambazwa kote duniani...Amewapongeza wanajumuia wa Chuo Kikuu cha Soka kwa kuendeleza mashindano hayo...
Haya fuatilia tukio hilo kwa njia ya picha...

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Baadhi ya washiriki wa shindano hilo kuanzia juu: Bi.Kyoko Oonishi, Bw. Takaaki Hiei, Bw. Tomoaki Saitou na bi Natsuki Wada (Karanga)



Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Washiriki walikaa pamoja kusikiliza uamuzi wa majaji na kumtangaza mshindi. Burudani ziliendelea huku nyoyo zao zikidunda..!

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Washindi walipatikana. Wa kwanza ni huyu Bi. Rie Teraguchi. Huyu ni muongeaji mzuri wa Kiswahili kama walivyo wenzake wawili, Mshindi wa pili na watatu. . Simulizi yake ilikuwa ya kusismua sana. Alipata mtoto wa pili siku moja tu baada ya maafa ya Japani, wakampa jina mtoto wao 'Sala au maombi..wakati wakiwa Tanzania. Alikaa Mwembechai , Dar...na akatoa simulizi juu ya maisha ya eneo hilo... wote walifanya vyema , lakini hawa ni washindi...

Picha za chini hapo... Mshindi wa pili, Bi. Natsuki Wada (Karanga)...
Mshindi wa tatu, Bi. Haruka Nakamura..

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Baada ya kazi nzima kukamilika...majaji na wageni waalikwa walipiga picha ya pamoja. Picha ya juu: Tuliovaa maua mekundu..kuanzia kwangu kwenda kulia kwako, BM, Ali Attasi(Jaji Mkuu), Mr. Mwenda Afisa mwandamizi ubalozi (DRC-Kongo), Mh. Salome Sijaona , Balozi wa Tanzania hapa Japani, Bw. Francis Mossongo, Afisa mwandamizi Ubalozi wa Tanzania Japani, Bi. Doroth kutoka Ubalozi wa Kenya na kushoto kwake ni Afisa Ubalozi wa Kongo -DRC hapa Japani. na maafisa wa Ubalozi wa Kenya hapa Japani, Bi. Doroth na Mr. Kaikai. Waliosimama nyuma ni washiriki wa shindani hilo na baadhi ya wahadhiri wao.

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Posted by BM. on Saturday, November 26, 2011

Maafisa usalama wakiwa wanaulinda mti wa krismas wenye urefuwa mita 2.4 uliotengenezwa kwa kutumia madini halisi ya dhahabu na kuonyeshwa katika duka la vito vya thamani la Ginza Tanaka Kikinzoku lililopo jijini Tokyo.

Mti huo umetengezwa kwa vipande vya dhabu na majani yake , wote ukiwa na kilo 12. Mti huo hauuzwi lakini thamani yake inafikia Yeni Millioni 150 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zinazofikia Trillioni 3.1. Duh watu bwana!...

Posted by BM. on Thursday, November 24, 2011

Jana ilikuwa siku ya mapumziko nchini Japani, ambapo walikuwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi...siku ya kupogezana kwa kazi ngumu wanazozifanya kulijenga taifa lao. Katika pitapita yangu jijini Tokyo nikakutana na onyesho la wazi la vijana wadogo ...ambao walikuwa wakishindanishwa kucheza mbele ya kadamnasi kuonyesha vipaji vyao. Onyesho hili lilinivutia kwasababu...linaanza kuwajenga watoto wenye vipaji vya muziki, na kuwafanya wajiamini wakati wa maonyesho. Jiunge nami ...


Posted by BM. on Thursday, November 17, 2011

Rais Robert Mugabe ameisifia Hong Kong kwa kumlinda binti yake kutokana na kudhalilishwa na waandishi wa habari wa Uingereza, chombo cha habari cha taifa cha Zimbabwe kimeripoti.

Bw Mugabe alitoa kauli hiyo alipohudhuria mahafali ya binti yake Bona katika chuo kikuu cha City huko Hong Kong. Walinzi wa binti huyo, mwenye umri wa miaka 22, walishutumiwa kwa kuwadhalilisha waandishi wa habari mwaka 2009, lakini hawakushtakiwa.Mwaka huo huo, mke wake Bw Mugabe Bi Grace hakushtakiwa baada ya madai ya kumbughudhi mpiga picha Hong Kong.Maafisa walitaka kinga ya kidiplomasia katika kesi ya Bi Mugabe.

Msemaji wa chuo hicho cha City Karen Cheng aliwaambia waandishi wa habari kuwa Bw na Bi Mugabe, ambao wanamiliki nyumba Hong Kong, walihudhuria sherehe za mahafali hayo siku ya Jumanne.Alisema Bw Mugabe na familia yake walipiga picha na wahitimu wengi "kama mzazi mwengine tu wa kawaida".Alisema "baadhi walikuwa wakiwatazama" lakini wazazi wengi hawakujua ni akina nani.Bw Mugabe anatarajiwa kuelekea Beijing katika ziara yenye nia ya kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China.

Posted by BM. on Sunday, November 13, 2011

Posted by BM. on Saturday, November 12, 2011

. Jioni ya leo nilifika katika hospitali iliyopo katika viunga vya jiji la Sagamihara, nchini Japani kumjulia hali Katibu Mkuu wa Umoja wa watanzania wanaoishi Japani-TANZANITE ambaye amelazwa hapo akipatiwa matibabu. Tuliongea kwa zaidi ya saa moja na nusu na anaeleza kuwa hali yake inazidi kuimarika na kwamba anatarajia hatua inayofuata ni kufanya mazoezi ya kitiba ili kuuweka mwili katika hali nzuri zaidi.



Uchunguzi wa hospitali hiyo umeoyesha kuwa ajali hiyo aliyoipata ilitegua sehemu inayounga mguu wa kulia na nyonga na ameshafanyiwa upasuaji katikati ya mwezi uliopita wa oktoba ili kuziba mifupa iliyoachiana. Mwombeki aliniambia kuwa yuko kwenye hali nzuri sasa na ameacha kutumia dawa za kuondoa maumivu kwa muda kutokana na maumivu hayo kupungua ukali wake, kauli iliyoungwa mkono na mkewe anayemuuguza.Pole sana bro. Mwombeki Jr.

Nje ya hoospitali...

Posted by BM. on Friday, November 11, 2011

Posted by BM. on Wednesday, November 09, 2011


Kampuni ya kutengeneza magari ya HONDA nchini Japani imetoa modeli mpya ya roboti iliyo mfano wabinaadamu ambayo sasa inaweza kuwasiliana kwa kutumia lugha ya ishara.

Roboti hiyo ya ASIMO inayotumia ving’amuzi inaelewa mazingira ilipo na hufuata maelekezo kwa haraka bila kuchelewa.

Iliwaonyesha waandishi wa habari jinsi ya kufungua kizibo cha chupa pale ilipoamuriwa kufanya hivyo.Katika mkutano huo na waandishi wa habari ambapo ilitambulisha , iliweka saini kwenye kitabu baada ya kuelekezwa kufanya hivyo.Hebu tujumuike tuone hatua hii ya kisayansi..( Bofya katikati ya picha hapo juu)

Posted by BM. on Tuesday, November 08, 2011

Mtanzania Willy Ngoya na raia mmoja Japani wameanzisha mradi wa kukusanya baiskeli na kuzipeleka Afrika Mashariki kutoka hapa Japani ambako wanaziuza kwa bei nafuu kama njia ya kurahisisha usafiri na usafirishaji hasa maeno na vijijini (Mashinani) wenzetu wanasema.




Mirindimo ilitembelea kazi zake na kuchukua picha kadhaa.Na kwa upande mwingine Shirika la Utangazaji la Japani pia nalo limevutiwa na hatua hiyo na kufanya mahojiano naye ambayo yatasikika siku ya Alhamisi, Nov, 10, 2011.


Unaweza kusikiliza mahojiano hayo ya Radio Japani-kwa kupitia kwenye kolamu ya marafiki, kwenye mtandao huu , angalia Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani NHK bofya hapo utakupeleka kwenye ukurasa ambao utaona picha za kazi zake na kusikiliza mahojiano. Au kwa kukurahisishia bofya hapa; http://www3.nhk.or.jp/nhkworld/swahili/top/index.html

Posted by BM. on Tuesday, November 08, 2011

Wanasayansi nchini Japani wamevumbua teknolojia ya kutengeneza bidhaa za plastiki kwa kutumia mwani …ule usioliwa ambao hutanda baharini .
Hatua hiyo itawezesha mabaki hayo ya plastiki kuoza ikiachwa ardhini. Hatua hiyo imekwenda mbali zaidi ambapo sasa wapo kwenye hatua za mwisho mwisho za majaribio ya kimaabara ambapo mwani huo utatengeneza nyuzi za kushonea miili ya binaadamu (Surgical threads) ambazo zitaoza sambamba na kukauka kwa kidonda.

Mwani umekuwa ukitumika pwani ya Afrika Mashariki kama mlo aghalab zaidi kwa wageni lakini hapa Japani hutumika sana katika maakuli, mbolea mashambani na sasa unataka kuumika katika hatua hii mpya.. Unaweza kufuatilia makala hii ya kusisimua kwa kusikiliza kipindi cha cheche za teknolojia kupitia mtandao huu; http://www3.nhk.or.jp/nhkworld/swahili/top/index.html Ukifika ukurasa huo angalia vipindi vya Jumanne, Nov,8 , bofya hapo na anza kusikiliza.

Posted by BM. on Sunday, November 06, 2011

Ninachokuuliza mwenzangu uliye na mtoto...umeshabaini vipaji alivyonavyo mwanao ...na je unaviendeleza. Usiache talanta aliyonayo ikapotea tu ...sawa mh...!

Posted by BM. on Sunday, November 06, 2011

Ujumbe wa leo...

Kwa waislamu wenzangu mnaweza kubofya hapa kusikia ibada ya Eid el hajj huko Iringa:
http://tunein.com/tuner/?StationId=145818&http://tunein.com/tuner/?StationId=145818&

Posted by BM. on Sunday, November 06, 2011



take 5 Karanga...!

Posted by BM. on Saturday, November 05, 2011

Eid Mubarak. Nawapeni mkono wa Eid wote mliofungua ukurasa huu. Ni siku njema kwetu sote. Nawatakia mapumziko mema , afya njema na kila lililojema. Eid Mubarak! Swala ya Eid kitaifa itafanyika kesho jijini Dar es salaam .

Kwa mujibu wa Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Muhidini Mkoyongore, Swala ya Eid Kitaifa itaswaliwa katika Masjid Al Farouq iliyoko BAKWATA Makao Makuu, kuanzia saa 1.30 asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid.Hii leo waislamu wa madhehebu ya Sunni walifanya ibada yao nchini humo..
Huko Makkah na Madina kwenyewe....Zaidi ya mahujaji milioni tatu, wakiwa wamevalia nguo nyeupe, wanaendelea kumiminika kwenye viwanja vya Mlima Arafat hivi sasa, ikiwa ni sehemu muhimu ya ibada yao ya Hijja. Inaripotiwa kuwepo hali ya usalama wa kiwango cha juu. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia, Mansour Al-Turki, ameliambia gazeti la Kiarabu la Asharq Al Awsat, kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyotegemewa, na kwamba hakuna kitisho chochote kwa usalama wa mahujaji, wala kwa nchi.

Katika miaka iliyopita, kulikuwa na matukio yanayohatarisha usalama kwenye ibada hii, hasa kutokana na msongomano mkubwa wa watu, vurugu na moto. Mwaka 1987, mahujaji wa Iran waliandamana, na kusababisha ghasia zilizomalizika kwa vifo vya watu 400. Mwaka 2006, mahujaji 346 wa mataifa tafauti walikufa, baada ya msongomano katika tukio la kurusha mawe kwenye mnara, kama ishara ya kumlaani Ibilisi.
Mlima wa Arafat ni sehemu ambapo kiongozi wa umma wa Kiislamu, Mtume Muhammad, alitoa hotuba yake ya mwisho kwa wafuasi wake, karne 14 zilizopita. Hijja ni nguzo ya tano katika Uislamu, ambayo humlazimu kila muumini mwenye uwezo kuitekeleza, angalau mara moja maishani mwake.

Posted by BM. on Saturday, November 05, 2011

Viongozi wa nchi tajiri, G20 walikutana kwa siku mbili Cannes chini Ufaransa wakiwa na hofu kuu kuhusu athari za mzozo wa madeni barani ulaya kwa uchumi wa dunia.Picha ya Juu Kansela wa ujerumani Angela Merkrl na Raisi wa Ufaransa Nicolas Sakozy na picha ya pili chni Raisi Barack Obama wa Marekani akizungumza na Kansela Angela Merkel na Raisi wa Argentina..Fernendez Kirchner.

Posted by BM. on Saturday, November 05, 2011

Wakazi wa jiji la Bangkok , nchini Thailand bado wako kwenye hekaheka za mafuriko baada ya maji kuvamia makazi yao.Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi.Yingluck Shinawatra (Pichani mwenye blauz nyeupe)amewahakikishia wakazi wa mji mkuu wa nchi hiyo Bangkok kuwa serikali inakabiliana na mafuriko ambayo yameuwa watu takribani mia mbili themanini na tisa na kusababisha hasara ya takribani dola bilioni tatu .
Waziri Mkuu Bi.Yingluck Shinawatra alitumia ndege ya jeshi kukagua mafuriko hayo na baadaye akafika kwenye eneo hilo na kuwafariji waathirika (Moja ya picha akiwapa mikono)

Mji wa Bangkok ambao unapatikana mita mbili pekee kutoka usawa wa bahari unaendelea kuwa hatarini kutokana na kuongezeka kwa maji kutoka vyanzo vya maji Kaskazini mwa mji huo ambavyo vinasababisha kufurika kwa mto Chao Phraya.Baadhi ya wananchi walionekana wakihamisha mali zao na kuzipeleka katika maeneo ambayo hayajaathiriwa.Huku wengine wakiwa taabani kwa uchovu!

Posted by BM. on Friday, November 04, 2011

Nimefuatilia habari hii nikaishia tu kujiuliza Whyiii!. Aah tusaidiane bana kuwaza. Inakuawaje hii..

Posted by BM. on Friday, November 04, 2011

Usiku huu nimepita mtaa mmoja hapa Tokyo , nikaliona duka lenye picha ya mmasai, huku midundo ya kibongo ikirindima... Nikaingia na humo ndani nikakutana na Wajapani wanaoongea kiswahili fasaha. Wanasema kuwa wanauza nguo na bidhaa za kitamaduni kutoka Afrika Mashariki. Eeh nikaondoka nikiiwaza ile picha inayolitambulisha lile duka...kuwa 'eeh kumbe mmasai dili eeh!'

Posted by BM. on Friday, November 04, 2011