Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, December 21, 2008

SERIKALI ya Tanzania inaendelea na harakati zake za kuwabaini wauaji wa maalbino ambapo sasa kuna taarifa za ndani juu ya watu walio karibu na mauaji hayo.
Taarifa kutoka Mkoani Shinyanga zinabainisha kuwa wanaohusika wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga ni wafanyabiashara wakubwa ambao huwalipa wauaji mamilioni ya fedha.Mauaji hayo ya albino, yanajumuisha makundi manne ya watu, wakiwamo wale wanaoonyesha walipo albino hao, wanaochagua albino anayefaa; na wanaotenganisha nyama ili kupata mifupa.DC wa Wilaya ya Bukombe mkoani humo Magesa Mulongo alitoa maelezo ya kina katika katika kijiji cha Bunyihuna baada ya kuuawa kwa mtu mwenye ulemavu wa ngozi..Alisema kundi la wanaoonyesha palipo na walemavu hao wa ngozi wamekuwa wakilipwa kuanzia Sh 200,000 wakati wauaji hao hulipwa kati ya Sh milioni 40 endapo mifupa ya aliyeuawa itapimwa na ubainika kuwa ni yenye mali inayotakiwa.Alisema vipimo vinavyotumika kubaini mifupa yenye mali ni pamoja na wembe, sarafu ya zamani au mfupa kusogezwa kwenye radio na kama mawimbi yatacheza au radio kuzima, mfupa huo utakuwa na mali inayotakiwa.Alisema mifupa ya walemavu hao wa ngozi ikifikishwa kwa tajiri anaweza kulipwa hadi Sh milioni 75 “lakini mpaka iwe imepimwa,” alisema.Mkuu huyo wa wilaya alisema, wameyabaini hayo baada ya kuwakamata wahusika wapatao saba wanaojihusisha na mauaji hayo katika tukio la Bukombe na tukio jingine lililokwama la wilayani Kahama, ambapo waliweka mtego baada ya kupewa taarifa za siri na raia wema la kutaka kuuawa kwa albino mmoja."Tumebaini siri nzito katika mauaji haya ya albino; na hasa baada ya kuweka mtego wilayani Kahama ambapo wahusika walijipanga, wakavaa magwanda yao na kuficha sura zao na baadaye wakampigia simu tajiri yao aliyepo wilayani Igunga mkoani Tabora kuwa wako tayari kwa shughuli hiyo na walipokusanyika wote tayari kwa mauaji hayo, tukawakamata na kuanza kuwahoji," alisema.Aliongeza kuwa, katika mahojiano hayo, alikuwepo pia mganga wa jadi aliyekamatwa na viungo vya albino wilayani Bukombe, ambaye naye aliwaeleza hatua kwa hatua jinsi wanavyotekeleza mauaji hayo, malipo wanayopewa na matajiri wao na namna anavyopima mifupa hiyo ili kutambua yenye mali."Tulichokibaini ni kuwa, wachimba madini na wavuvi hawahusiki sana, bali wanachokitaja ni kwamba mifupa hiyo inatakiwa sana na matajiri wakubwa," Mkuu huyo wa wilaya alisema.Alisema katika tukio la Shilela wilayani Kahama, wakati wa zoezi la kuwatambua lililofanywa katika kijiji hicho, mama mzazi wa binti aliyeuawa alimtambua muuaji mmoja na yeye alikiri kuhusika katika mauaji hayo

0 comments: