Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, May 28, 2010

Ilikuwa taarifa ya kushitusha kuwa mwanamuziki Fredy Mayaula Mayoni amefariki dunia huko Ubeligiji jana Ijumaa kwa ugonjwa wa kansa ya Ubongo. Alikuwa na miaka 64 alipoacha kuvuta pumzi. Kwa kipindi kirefu kulikuwa na taarifa za kuugua kwa mwanamuziki huyo na inasemekana alipata ugonjwa wa kupooza miaka miwili iliyopita na baadaye hali ikatengemaa.


Mie binafsi taarifa hiyo iligusa kwasababu ya kumtambua kupitia nyimbo zake kama vile Mbongou yaani pesaaa pesaa ,Mwanamuziki hyu pia aliwahi kuichezea timu ya Yanga ya Tanzania mbali na kuwa mtaalamu wa kutumia komputa.Kwa wakazi wa dar hasa wanaokaa Magomeni Mikumi watamkumbuka vyema maana alikaa maeneo hayo wakati fulani wakati baba yake akiwa ubalozi wa DRC nchini Tanzania. Moja ya nyimbo ninayoipenda sana ni Othman, kwahakika sijui maana yake , lakini nahisi wimbo huu una ujumbe mzito sana. Mungu aiweke peponi roho ya mayaula Mayoni , Amen.

Posted by BM. on Tuesday, May 25, 2010

Katibu Mkuu Msaidizi wa jumuia ya watanzania wanaoishi nchini Japani Tanzanite Bw. Abby Senkoro(Pichani) ametoa taarifa inayowakumbusha wanachama wa jumuia hiyo kuwa tafrija ya kumuaga ofisa ubalozi Bw. Maleko na kumkaribisha Mh. Balozi Mama Salome Sijaona, Balozi mpya wa TZ hapa JP. Bw. Senkoro Kushoto na Kulia Bw. Prosper...


Hafla hiyo itafanyika siku ya Jumapili tarehe: 30/05/2010 huko Yamatoshi-Kinroufukushi-Kaikan Ni dakika 5 kutoka Tsuruma Station)na nikuanzia saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku.
Bw. Sankoro amesema kuwa uongozi unawaomba wale wote waliojiandikisha kufika siku hiyo kufika kwa muda unaotakiwa ili tuweze kumaliza shughuli kwa muda tunaotakiwa. Na kwa wale waliojiandikisha na kupatwa na dharura tafadhali tunawaomba kutoa taarifa kwa viongozi walioandikisha majina yao haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa wale ambao hawajajiandikisha hawataruhusiawa kuingia ukumbini. Hivyo basi wale wote ambao hawajafanya zoezi hilo wanaombwa wafanye hivyo mpaka kufika tarehe 26/05/2010.
Maelezo ya jinsi ya ukumbini : Kutokea Shinjuku inachukua takriban saa moja kwa treni ya haraka (Odakyu line). Badirisha treni ukifika Sagamioni station upande wa Katase Inoshima line na ushuke Tsuruma station. Ukumbi uko dakika 5 toka kituo cha treni.Angalia Ramani


Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani Bw. Elibariki maleko (Pichani) anayetarajiwa kuagwa siku hiyo baada ya Kumaliza kipindi chake cha Utumishi hapa nchini pamoja na kumkaribisha Balozi mpya wa Tanzania hapa nchini Mh. Salome Sijaona.

Posted by BM. on Friday, May 21, 2010

Ubunifu na jitihada za msanii zimemuwezesha msanii huyu kutoka na kibao hiki......shoga. Bofya hapo , burudika.

Posted by BM. on Sunday, May 16, 2010

jana Jumamosi katika eneo la Chofu hapa Japani kulikuwa na kikao cha kifamilia cha kumuaga Kamarade Ndesika anayerejea nyumbani baada ya kukamilisha kipindi cha Mktaba na Idhaa ya kiswahili Redio Japani. Shughuli ilifanyika kwa mdau nambari moja Mr. Kamu na kuhudhuriwa na baadhi ya wanafamilia hapa Tokyo. unaweza kupitisha macho kuona kilichojiri kwa njia ya picha.
Chofu ...kaskazini kabisa mwa picha hii ...picha kutoka juu....eneo la tukio.

Kaka yetu Elibariki Maleko ,Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania hapa Japani alikuwepo kutunasihi!....

Abbya na Proper ...walikuwepo...


Wadau...

Posted by BM. on Sunday, May 16, 2010

Moja ya mambo ya kufurahisha ilikuwa uwekaji wa kumbukumbu za matukio kwa kupiga picha...


Posted by BM. on Sunday, May 16, 2010


Benchi la uundi , Kamu na Willy...


Pande za kushoto ..tulikuwepo...


Kona ya wandamizi..


F. Simba, Specioza Amani...


Mr. Maleko, Simba, Abby


Hai tebo, Jamila na fatma.


Grace Maleko...akizungumza na wanafamilia...

Posted by BM. on Saturday, May 15, 2010

Ijumaa ya tarehe 14 , May , wafanyakazi wa Redio Japani waliwaaga watangazaji wa Idhaa ya kiswahili Ruth Ndungu na Reginald Ndesika waliomaliza kipindi chao cha mkataba na NHK. Ilikuwa hafla ya kupendeza na ya kusisimua mno. Unaweza kufuatilia kilichotokea kwa njia ya picha..




Viongozi waandamzi wa NHK walikuwepo katika hafla hiyo..


Eneo la tukio...


Kamarade Ndesika , Fundi Mitambo wa NHK reiko Iwami na miye...


Bahati iliyoje kupiga picha muhimu kama hii na Mkuu wangu wa kazi>>>.


Mtangazaji Ruth Ndungu ndani ya kimono katika hafla ya kuagwa


Jirani yangu Bongo; mama Frank naye aliagwa leo hapa Tokyo baada ya kukaa nchini Japani kwa miaka sita mfululizo...katika hafla hiyo alitoa hotuba yake kwa kijapani...


Watangazaji wa Idhaa ya Kiarabu ambao wote wanatoka nchi za Misri na Morocco Kaskazini mwa Afrika walikuwepo na Mkuu wa idhaa hiyo kushoto kabisa!

Picha ya pamoja

Posted by BM. on Saturday, May 15, 2010


Ilikuwa zamu ya Wakuu wa Idhaa ya Kiswahili kuongea ....haikuwa rahisi hivyo...


Pamoja na simanzi ya kuwaaga makomredi...Kiongozi Mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili Yuko Asano aliendelea kuelezea juu ya tabia za kila mtu katika kipindi cha kuwepo kwao Redio Japani, Mchango wake katika kusukuma gurudumu la idhaa na jinsi tutakavyowamiss waheshimiwa..Kilikuwa kipindi cha utulivu ukumbini..



...Utulivu>>>>>>>


Kula na kusikiliza; Bi. Fatma Mohamed na Chiho Yamada katika meza kuu...<


Ilikuwa wakati muafaka wa kutoa hoja zinazowiana na masuala ya Oktoba kuo TZ...Dr. Kamu..Mkinichagua!...


Mmoja wa watangazaji wa RJ Mareen Waweru akifurahia simulizi za Mkubwa ,Dr. Kamu.

Posted by BM. on Saturday, May 15, 2010


Watu mashuhuri; (L-R)Grace Mossongo, Specioza Amani na Anna Kwambaza , hakuna kitakachoharibika!


Menyuuu ilizingatiwa pia...>>>>>


Nipo karibu na kamarade Ndesika katika mnuso<



Mtangazaji anayechukua nafasi ya Reginald Ndesika, Bi. Anna Kwambaza naye alikuwepo katika hafla hiyo...


Edward kadilo,(Kushoto) mmoja wa watangazaji wa RJ akisisitiza jambo mbele ya Kiongozi mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili Kaori Note.


Kila mtu alimwandikia lake kwenye kadi ya zawadi!

Posted by BM. on Thursday, May 13, 2010

Jumuia ya watanzania wanaoishi Japani TANZANITE inawataarifu kuwa kuwa imeandaa tafrija ndogo ya Kumkaribisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sijaona sambamba na kumuaga Ofisa Ubalozi mwandamizi, Bw Elibariki Maleko ambaye anatarajia kurejea nyumbani Tanzania hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba wake wa kikazi hapa Japani.
Jumuia hiyo imetoa taarifa za kina juu ya hafla hiyo kuwa; itafanyika Siku ya Jumapili, tarehe 30 Mei 2010.
Muda: Kuanzia saa kumi jioni mpaka saa mbili usiku (16:00 - 20:00).
Mahali: Ukumbi wa Tsuruma.Taarifa ya jinsi ya kufika kwenye ukumbi itatolewa baadaye.
Ili kurahisisha shughuli za maandalizi, kama chakula na vinywaji, tunaomba wale wote watakaotaka kuhudhuria kuandikisha majina yao kwa kwa viongozi wafutao:

1. Abby senkoro: mail: ewsenkoro@yahoo.com, Simu: 090-9801-4433
2. Juma Kipya: 080-3414-4460
3. Upendo Mwimbage: 080-1326-9700
4. Mariam Yazawa: 090-4422-8555
5. Yasir Kiluke: 090-4203-3340
6. Bagilo Jumbe: 090-1733-7447
7. Amani Paul: mail: amani.paul@gmail.com, simu:080-4200-0684

Siku ya mwisho ya kujiandikisha ni tarehe 22/5/2010. Pia tunaomba kusisitiza kuwa wale ambao hawatajiandikisha majina yao hawataruhusiwa kuingia ukumbini siku ya tafrija. Na wale watakaohudhuria wazingatie muda kwasababu ukumbi umekodiwa mwisho saa 2 kamili usiku hivyo tunawaomba wafike kwa muda unaotakiwa.

Balozi wa TZ hapa JP Mh.Sijaona alipowasili hapa Japani na kupokewa na Bw. Maleko , Afisa mwandamizi wa Ubalozi huo hapa Tokyo.

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

Miaka mitano iliyopita , mwezi kama Huu nilipanda mlima Kilimanjaro nikiambatana na Viongozi waandamizi akiwemo Generali Mirisho Sarakikya wapili Kulia. Mie nimevaa jaketi jekundu. Ilikuwa safari ngumu lakini ya kuikumbuka...Wa kwanza kushoto ni paparazi ni Asiraji Mvungi wa ITV na watatu Kulia ni Paparazi Daniel Mjengwa wa Mwananchi katika msafara . Safari ilikuwa safi.

Kilele cha Mlima Kilimanjaro...

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

Mkurugenzi wa bendi ya Bwagamoyo Sound Internationale Prince Muumin Mwinjuma akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akielezea maendeleo ya bendi yake iliyokuwa imepiga kambi mkoani Tanga huko Chumbageni.


Prince Muumin Mwinjuma amesema tayari bendi yake imeshajiimarisha na inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 4 Juni mwaka huu kwenye ukumbi wa Vatcan City Sinza jijini Dar es salaam ili kuonyesha kazi yao iliyowafanya kuwepo kambini Tanga kwa muda mrefu.
Ameongeza kwamba katika uzinduzi huo kutakuwa na bendi ya Taarab ya Jahazi Molden Taarab inayoongozwa na Mwanamuziki mashuhuri nchini katika muziki wa taarab Mzee Yusuf, pia kutakuwa na bendi kongwe nchini ya Msondo Music Band na burudani nyingine lukuki.
Amesema kuwa katika onesho hilo pia wanatarajia kumtambulisha mwanamuziki wao mpya Kalama Legesu (Pichani Kushoto)ambaye wamemchukua kutoka bendi ya Mlipani Park Orchestre (Sikinde)ya jijini Dar es salaam ili kuimarisha kikosi chao na akaongeza kwamba kabla ya kuondoka mkoani Tanga watafanya onesho moja la kuwaaga wakazi wa mkoa wa Tanga.Amemalizia kuwa Albam yao mpya katika bendi hiyo ina nyimbo 6 na imepewa jina la “Nafsi haina Urithi”

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

Nchini Japani kuna utaratibu ambao nauona ni mzuri. Kuna siku ambayo watu hujiandikisha majina yao katika ofisi ya NGO fulani halafu husambazwa maeneo fulani fulani kufanya usafi kwa kujitolea. Utaratibu huu ungefanyika kwentu Afrika Mashariki ungependeza sana , au unasemaje mdau!

Shughuli za usafi jiji Tokyo leo J2.

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

A woman leaves with her dogs after voting in a caravan turned polling station in Cornwall, England.

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010


Mfyotoaji anapofyotolewa!

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010


Wabunge wa Bunge la Ukraine wakitwangana makonde baada ya kutofautiana katika mjadala tete wa uhusiano wa nchi yao na Urusi katika masuala ya bahari. Inashauriwa kuwa kabla hujaamua kugombea ubunge kama uko nchini humo ujiunge na chuo cha masumbwi au karate kwanza. Na-imagine ndio ingezuka kwetu ingelikuaje....

Posted by BM. on Sunday, May 09, 2010

A woman wanted to reach her husband on his mobile phone but discovered that she was out of credit, She instructed her son to use his own phone to pass across an urgent message to his daddy who was on site.
After junior had called, he got back to mummy to inform her that there was a lady that picked up daddy's phone the three times he tried reaching dad on the mobile.
( Women !! ?)
She waited impatiently for her husband to return from work and upon seeing him in the driveway, she rushed out and gave him a tight slap,and she slapped him again and again, kicked him, and spat in his face for good measure.


People from the neighbourhood rushed around to find out what the cause of the commotion was. The woman asked junior to tell everybody what the lady said to him when he called. Junior said "The subscriber you have dialled is not available at Present. Please try again !!" EEEhhh sasa!

Posted by BM. on Monday, May 03, 2010

Erico ni binti wa kijapani anayemudu kucheza kifaa cha Muziki wa kiasili wa Kabila la Wajaluo -Afrika Mashariki. anaongea na kuimba kwa Kijaluo. Leo alikuja katika studio za NHK kurekodi vipindi kama sehemu ya tamasha la maadhimisho ya 75 tangu matangazo ya NHK World kwenda hewani kabla ya kuwepo kwa Idhaa ya Kiswahili. Tumempenda kwa jinsi anavyotupenda Waafrika na mila zetu na jitihada zake za kuitangaza Afrika nchini Japani.Arigato Gozaimashita!

Anyango akiwa katika tumbuizo la wazi katika studio za NHK leo.


Tupo na Bi. Anyango , msichana wa Kijapani anayemudu vyema kucheza chombo cha Nyatiti cha kabila la wajaluo kule Kenya na anaongea kijaluo na Kiswahili kwa ufasaha...take five Anyango!...anadumisha mila yetu..

Tupo hapo mie na mwenzangu Edward Kadilo na wachezaji wa bendi ya Warembo ya Anyango , muda mfupi baada ya onyesho lao...