Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, February 24, 2009

Rio Carnival imeanza rasmi jumatatu baada ya kufunguliwa rasmi na rais wa Brazili aliyeamua kugawa kondomu ili washiriki na wahudhuriaji wajilinde na ugonjwa wa ukimwi.Rais wa Brazili ameamua kuonyesha jinsi anavyounga kampeni za kupunguza ugonjwa wa ukimwi nchini Brazili kwa kuwagawia kondomu watu wanaoshiriki na wanaohudhuria Rio Carnival.Rais Luiz Inacio Lula da Silva aliwarushia kondomu watu waliohudhuria Rio Carnival wakati wa ufunguzi wa Carnival hilo maarufu na kubwa duniani.Msemaji wa rais huyo alisema kwamba Rais Silva alitaka kuonyesha umuhimu wa kampeni ya Brazili ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.Mwezi huu pekee Brazili itagawa jumla ya kondomu milioni 65 ikiwa ni zaidi ya kiwango cha kawaida cha kondomu milioni 45.Brazili mwaka huu in mpango wa kununua kondomu bilioni 1.2 na kuifanya iwe serikali inayoongoza kwa kununua kondomu nyingi duniani.Carnival la Rio linalofanyika kila mwaka kwa siku tano mfululizo limeanza rasmi jumatatu likishirikisha vikundi kadhaa vya ngoma na maonyesho na kuhudhuriwa na watazamaji zaidi ya 80,000 katika uwanja wa Sambadrome jijini Rio de Janeiro.

0 comments: