Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 31, 2009


Chama kikubwa cha Upinzani nchini Japani cha DEMOCRATIC kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Baraza la chini la Bunge, uchaguzi uliofanyika jana Jumapili. Baraza hilo ndilo linalomchagua Waziri mkuu wa JAPANI. Ushindi huu umekiondoa madarakani chama cha LIBERAL DEMOCRATIC cha waziri Mkuu TARO ASO kilichokaa madarakani mwa miaka 54 mfululizo. DEMOCRATIC Kimekusanya viti 308 kati ya 480 na bila shaka sasa Raisi wa chama Yukio Hatoyama hapo juu, katikati anayeonekana vyema…anakuwa Waziri Mkuu. TARO ASO amekaa madarakani kipindi kifupi sana chini ya mwaka mmoja lakini mambo yake ya kisiasa yamekuwa ndivyo sivyo. Angalia heka heka za uchaguzi za jana Napiga kura sasa...Mshindi utamsikia tu!
Fasta tupeleke..
haya tuhesabu
Hatimaye Waziri Mkuu Taro Aso , kura hazikutosha...Ameshasema atajiuzulu uongozi wa Chama .

0 comments: