Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010

mmoja wa manusura wa tetemeko la Haiti Msichana Holleline Lozama mwenye miaka 26 akitabasamu mara baada kutolewa kwenye kifusi ..Pole sana!
Habari za Karibuni kutoka Port au Prince mji Mkuu wa Haiti zinabainisha kuwa Kijana mmoja wa kiume amenusurika baada ya kutolewa kwenye kifusi cha tetemeko la ardhi , akiwa amekaa chini ya kifusi siku 11 .Waokoaji toka mataifa mbali mbali walikuwa ndio wanajitayarisha kuondoka nchini Haiti kurudi kwenye nchi zao baada ya zoezi la uokoaji kusitishwa baada ya matumaini ya kumuokoa mtu kutoka kwenye vifusi kuonekana ni finyu.Lakini kama Kama miujiza mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Wismond Exantus mwenye umri wa miaka 26 aligunduliwa na mama yake kuwa bado yupo hai chini ya kifusi cha hoteli aliyokuwa akifanya kazi ambayo iliporomoka chini yote.Kaka yake alitumia spika kuita jina la mdogo wake na jamaa alisikika kutoka chini ya ifusi akiita.Kazi ya kuwatafuta waokoaji ambao wengi wao walishafunga virago ilianza mara moja. Watumiaji wa tovuti ya twitter walianza kutumiana meseji wakiwatafuta waokoaji. Hatimaye waokoaji toka mataifa mbali mbali ambao walikuwa bado nchini Haiti walijitokeza na kuanza zoezi la kumuokoa Wismond. Iliwachukua saa chache waokoaji wa Ugiriki na Ufaransa kuweza kumtoa Wismond toka kwenye kifusi akiwa hai ingawa taabani kwa njaa.
Wismond amekonda ghafla kwa siku 11 alizokaa chini ya kifusi kiasi cha kuhitaji kamba kuishikilia suruali yake isianguke.Akizungumza muda mfupi baadaye , Wismond anasema kuwa tangia siku ambayo tetemeko la ardhi lilitokea, alikuwa hauoni mchana wakati wote akiwa kwenye giza kama usiku.Anasema kuwa siku za mwanzo za tetemeko la ardhi alikuwa akinywa soda zilizokuwa chini ya meza ambayo alikimbilia kujificha wakati tetemeko la ardhi lilipotokea. Lakini baada ya soda hizo kuisha alianza kuunywa mkojo wake mwenyewe kila alipokojoa. Wismond ni miongoni mwa watu wachache sana wenye bahati ambao wamefanikiwa kunusurika maisha yao kwenye tetemeko hilo la ardhi. Hadi sasa inakadiriwa jumla ya watu 120,000 wamefariki kutokana na tetemeko hilo kubwa la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa 7.0. Hebu angalia video hiyo tukio la kumuokoa Wismond.

0 comments: