Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, September 14, 2010

Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan leo jumanne amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala cha Democratic, baada ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mpinzani wake, Ichiro Ozawa, mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya chama hicho.

Ozawa alijiondoa katika wadhifa wa Naibu mkuu wa chama mwezi Juni, kutokana na shutuma za kashfa ya fedha za ufadhili wa kisiasa. Bwana Kan(Pichani anayetabasamu), ambaye amekuwa katika wadhifa huo kwa miezi mitatu, ameahidi kupunguza madeni na kubana matumizi.
Chama cha Democratic cha Japan kimekuwa kikijitahidi tangu kiingie madarakani mwaka mmoja uliopita, kikipoteza wingi katika baraza kuu la bunge katika uchaguzi wa mwezi Julai. Wakati huo huo, sarafu ya Japan, Yen imepanda kwa kiwango cha kuwahi kuonekana kwa miaka 15 iliyopiata, dhidi ya Dola ya Marekani.
Kwa ushindi huo sasa Kan ataendelea kukalia kiti cha Uwaziri Mkuu , na sasa Baraza la Mawaziri linasubiriwa kutangazwa na Bw. Kan mwenye miaka 63.
Kama angeshindwa maana yake Japani ingelikuwa na Mawaziri wakuu sita katika kipindi cha miaka mine, rekodi ambayo ni ya kipekee kwa nchi zeye chumi kubwa kama Japani. Kan mwenyewe amekuwa Waziri Mkuu kwa miezi mitatu tu basss.


Ozawa akikubali kushindwa..
Jumla ya kura zilizokuwa zikigombaniwa zilikuwa 1,222 ambapo Kan alipata kura 721 na Ozawa kura 491. Kipindi cha wiki moja hapa Japani kiliwanya watu wahemee juu juu kutokana na kampeni kupamba moto, na hasa kutokana na ukweli kuwa watu hao wawili wanatofautiana sana mtazamo wao wa kiongozi, Ozawa akionekana kuwa mkali na Kan akionekana kufuata mkondo wa kidiplomasia zaidi…Yao yameisha tusubiri ya kwetu…






0 comments: