Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, December 15, 2010

Baada ya wakenye kusubiri kwa miezi kadhaa hatimaye Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - International Criminal Court (ICC) imetaja majina ya Wakenya sita anaowatuhumu kuhusika kupanga vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwaka 2007.


Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta, ni mmoja ya waliotajwa.Waziri wa Elimu aliyesimamishwa William Ruto, Mkuu wa uendeshaji wa Radio Kass FM, Joshua Arap Sang, katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kirimi Muthaura na Mkuu wa zamani wa jeshi la polisi Mohammed Hussein Ali, nao majina yao yametajwa na Bw Ocampo.Polisi nchini Kenya wamewekwa katika hali ya tahadhari iwapo baada ya kutangazwa majina hayo kunaweza kuibuka ghasia mpya.Kila mmoja kati ya hao sita, watatumiwa hati ya kuitwa mahakamani, lakini wakigoma au wakijaribu kuingilia uchunguzi, mathalan kuwatisha mashahidi, Bw Ocampo amesema ataomba kibali cha hati ya kuwakamata.


Katika taarifa yake baada ya tangazo hilo la Bw Ocampo, Rais Mwai Kibaki amesema ana matumaini mahakama hiyo ya kimataifa, mchakato wake utatimiza wajibu wake kwa maslahi ya taifa la Kenya.Amewahakikishia Wakenya kwamba serikali imeimarisha ulinzi nchi nzima.
Jumla ya wattu 1200 walikufa katika ghasia hizo...

0 comments: