Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, February 22, 2011

Imoto Ayako Ni maarufu sana nchini Japani hususan miongoni mwa vijana na watu wa rika la kati na wafuatiliaji wa habari. Huonekana katika vipindi va televisheni vya burudani. Ni nguli katika ubunifu , ujasiri na uthubutu. Amesafiri kila pembe ya dunia akishiriki katika matukio mbalimbali ya kufurahisha na ya kutisha na hata kuhatarisha maisha yake huku akirekodiwa na baadaye vipindi hivyo hurushwa na kituo kimoja cha televisheni hapa Japani. Wajapani na wageni wa marika yote hapa japani wanamjua mdada huyu kwa pilika pilika zake.


Kwa sasa binti huyu Imoto Ayako ana miaka 23 na mara zote ukikutana naye au akiwa ndani ya kipindi huonyesha ucheshi na furaha . Vazi lake linalomtambulisha ni sare ya shule na usoni akiwa amejipaka wanja mzito. Bila shaka hii ni mbinu yake ya kujitambulisha.
Hapa Japani kuna kituo kimoja cha televisheni kinarusha kipindi kinachoitwa “Sekaino hatemade ittekyuu”. Hapo yeye ndiye ‘stelingi’ watu wanaangalia kazi yake na baadaye kuzjadili kwa mshangao na furaha kubwa.Itkumbukwa binti huyu ameshapanda hadi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mwaka 2009 , na kuna kipindi kilionyeshwa akiwa anacheza na mamba katika mto Nile na wakati fulani akifukuzwa na chu, achilia mbali kuruka na parachuti baada ya mafunzo ya wiki moja.

Katika kuonyesha kuwa anathubutu mambo mengi mwezi August mwaka jana alikimbia takriban kilometa 126.5 akikimbia bila kupumzika kwa saa 26 na dakika tano katika mbio za kujitolea ambapo televisheni moja inayotangaza kwa saa 24 hapa Japani ilikua ikikusanya fedha na kutoa habari zinazohusu masuala ya Kijamii , mazingira na huduma za majanga. Ameandika vitabu kadhaa vinavyouzwa kote duniani vikielezea mwenendo wa maisha yake. Unaweza kumuangalia Imoto Ayako katika clips mbalimbali za You tube kwa sasa anza na hii hapa!Kuhusu mbio hizo zilivyokuwa unaweza kubofya:http://www.japan-zone.com/news/2009/08/31/a_triple_marathon_weekend.shtml
Take 5 mdogo Imoto!

0 comments: