Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, March 13, 2011

Habari za hivi karibuni kutoka Shirika la Polisi la Japani zinasema kuwa watu Elfu 10 hawajulikani walipo , mawasiliano kati yao na ndugu zao hayapo, hawamo katika idadi ya miili iliyotambuliwa. Bado miili ya watu 200 na zaidi haijatambuliwa na hivyo idadi ya watu waliopotea huenda ikafikisha idadi kamili ya waliokufa kuzidi elfu 10.

Watu wengi waliokolewa wanahifadhiwa katika vituo maalum na kupatiwa maji na chakula na waokozi zaidi ya laki moja wengi wakiwa wanajeshi wa Japani wanashiriki katika zoezi hilo. Nchi 69 duniani zinashiriki katika zoezi hilo la Uokozi, ambapo Marekani inatumia ndege zake maalum za uokozi kujaribu kuwaokoa watu walionasa kwenye vifusi.
Taarifa za karibuni za mtandao wa NHK zinabainisha kuwa watu 19 wamebainika kupoteza maisha kutokana na mnunurisho wa nyuklia na jitihada zinafanywa kuzuia janga hilo lisisambae kwa watu wengi na idadi ya watu waliohamishwa mpaka sasa inatajwa kuwa ni 399.

Hata hivyo idadi kamili ya waliopoteza maisha yao, waliojeruhiwa na kupotea hadi sasa itatangazwa na vyombo vya habari vya hapa muda mfupi ujao. Polisi katika eneo la Iwagi wameonekana katika eneo lililo na kinu cha nyuklia wakiwa wamevaa barakoa(Masks).
Katika jiji la Iwaki watu anahama kwasababu kadhaa ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa vyakula madukani kulikosababishwa na maafa na Polisi wa eneo hilo wamekuwa wakiwagawia wakazi hao matonge ya wali 'maarufu hapa kama 'onigiri' na maji.
Wakati huo huo Shirika la Utabiri wa hali ya hewa la japani limesema kuwa tetemeko la Jana Ijumaa lilikuwa na ukubwa wa 9.0 na sio 8.9 kwa kipimo cha matetemeko cha richa.
Hakuna umeme wala maji. (Unaweza kuzipata habari zaidi kupitia Associated Press)

0 comments: