Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, March 15, 2011

Wasiwasi wa kutokea upungufu mkubwa wa chakula hasa kilichokwisha pikwa nchini Japani umewafanya watu kukimbilia madukani na kununua vyakula kwa wingi tangu Ijumaa iliyopita tetemeko lilipotokea. Leo maduka mengi ya vyakula yana vyakula vichache ,hakuna maji ya kutosha ya chupa na maziwa ya paketi yamekuwa adimu. Bidhaa zilizobakia kwa wingi ni biskuti na vikaukau.
Vijikabati vya maduka ya vyakula na bidhaa nyingine ya kujihudumia ( supermarkets ) na madogo maarufu katika jiji la Tokyo kama ‘convenience vilikuwa havina bidhaa za kutosha . Bila shka msongamano wa magari umeifanya kazi ya kusambaza bidhaa za vyakula katika maduka hayo kuwa ngumu na ya kukatisha tamaa.

Tetemeko la Ijumaa pia limesababisha hasara kubwa madukani kwa bidhaa nyingi kuanguka na kupondeka hususan zilizopangwa karibu na vimimika , vinywaji baridi na moto. Ukosefu wa umeme katika baadhi ya maeneo na pia mgao wa umeme ambao unashuhudiwa kwa mara ya kwanza katika miongo mingi bila shaka umeshusha uzalishaji wa vyakula vya kusindika vinavyotumiwa sana Japani na sekta ya usafirishaji kutoka kwa wakulima hadi kwa mlaji imevurugika kwa kiasi fulani. Maji ya kunywa ya chupa yameadimika madukani , wasiwasi ukisababishwa na taarifa za kukatika kwa maji katika baadhi ya maeneo kutokana na kuvurugika kwa miundomsingi.Hata hivyo mgao huu wa umeme unafanyika kisayansi sana na ni vigumu watu wanaoutumia umeme wa kawaida kuhisi athari zake kubwa. Inakuwa mchana kwa dakika kadhaa na bila shaka kutokana na baadhi ya viwanda kusitisha uzalishaji hiyo pia imesaidia.
Katika miji iliyopo katika viunga vya Tokyo, Kyodo na chitosefunabashi , maduka mengi yalifungwa jana (J4) lakini yamefunguliwa leo na jana watu walionekana kuwa katika kasi ya kurejea nyumbani. Pengine tatizo linalowakuta wageni ni kutoelewa matangazo yanayowkwa kwenye mbao za maduka kwa lugha ya kijapani...lakini bila shaka itakuwa ni mgao wa umeme au hadhari ya tetemeko.
Watu waliekea kwa wingi katika Jiji la Ginza kununua bidhaa za vyakula na katika kipindi kifupi maduka yalibaki tupu. ‘Vyakula sasa vinahamia majumbani badala ya kukaa madukani’, mtu mmoja raia wa Marekani aliyejitambulisha kwa jina la James alimfahamisha mwandishi wa habari hizi akiwa anafanya manunuzi katika eneo la Shibuya katikati ya Tokyo

0 comments: