Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, May 16, 2011

Mkuu wa fuko la fedha la kimataifa -IMF ,Domonique Strauss-Kahn amekamatwa New York
tayari kukabili mashtaka ya kumsumbuwa na kutaka kumbaka mhudumu mmoja wa kike wa hoteli mjini New-York. Mkuu huyo umri wa miaka 62 alikamatwa akiwa ndani ya ndege ,katika uwanja wa ndege wa John F. Kenndy,muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Paris.Mhudumu huyo wa kike wa hoteli ndie aliyetowa malalamiko kwamba Dominique Strauss-Kahn alitaka kumbaka. Duru zinasema Dominique Strauss-Kahn aliondoka haraka hotelini na kusahau simu yake ya mkono na vitu vyake vyengine.Mfaransa huyo,aliyekuwa akipewa nafasi nzuri ya kukiwakilisha chama cha kisoshalisti uchaguzi wa rais mwakani ,alipangiwa kukutana na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo mjini Berlin kuzungumzias mgogoro wa fedha wa Ugiriki.
Wakili wa Domonique Strauss-Kahn William Taylor amewataka watu wasitaharuki kuhusiana na kisa hicho cha kukamatwa mkuu huyo wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF. Jana jumapili Dominique Strauss Kahn alipangiwa kufikishwa mbele ya jaji mjini Manhattan.
Duh!

0 comments: