Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, September 11, 2011

Usiku wa kuamkia leo Tanzania imejipatia mrembo wake atakayelishikilia taji hilo kwa mwaka mmoja ujao. Sarha Israel (katikati) amejinyakulia ushindi huo unaojulikana kama MIss Vodacom Tanzania baada ya kuwaangusha wenzake katika kinyang'anyiro hicho.
Picha : Sarha akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Pili,Tracy Sospeter (kulia) na mshindi wa tatu,Alexia William mara baada ya kutangazwa usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.

Kwa ushindi huo Sarha Israel anakuwa Vodacom Miss Tanzania 2011-2012 na kunyakua gari aina ya Jeep lenye thamani ya shilinngi milioni 72 lililotolewa na wadhamini wakuu kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania na Kampuni ya kuuza magari ya CFAO MOTORS ya jijini Dar es salaam Shindano hilo limemalizika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Uganda Juliana Kinyomozi ndiye aliyekuwa akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo...




Take 5 Sarha.

0 comments: