Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Mto unaopita katikati ya jiji la Bangkok nchini Thailand umefurika hapo jana na kupasua baadhi ya kingo zake.Mto Chao Phraya ulioko Bangkok

Barabara nje ya Bangkok zimejaa magari, wakati maelfu ya watu wakiyakimbia mafuriko hayo, ambayo ni mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika nusu karne. Magunia ya mchanga yamewekwa katika majengo mbalimbali mjini humo ili ya kuyakinga dhidi ya maji yanayozidi kufurika.

Wakaazi wamekumbana na mamba na nyoka ambao wanaokimbia mashamba yaliofurika. Televisheni nchini humo zinaonyesha msongamano wa magari yaliokuwa yakiondoka mjini humo lakini idara ya trafiki imesema, haikuweza kutoa idadi kamili ya watu wanaouhama mji wa Bangkok, kwani kamera nyingi za barabarani zimefunikwa na maji.

Mpaka sasa, janga hilo la mafuriko la miezi mitatu nchini humo, limekuwepo katika majimbo ya kaskazini na ya kati. Takriban watu 400 wameuawa.

0 comments: