Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, August 28, 2010

Kenya imeandika historia mpya ya utawala nchini humo kwa kuidhinisha katiba mpya, iliyotungwa na wananchi wenyewe, baada ya ile iliyokuwa ikiitumia kabla ya kupata uhuru wake mwaka 1963. Rais Mwai Kibaki, aliwaongoza maelefu ya raia wake walioshuhudia akitia saini katiba mpya ya nchi hiyo katika sherehe zilizofanyika viwanja vya Bustani ya Uhuru mjini Nairobi jana Ijumaa.

Mh. Kibaki akitia saini katiba mpya..

Baada ya kutia saini nakala sita za katiba hiyo, wimbo wa taifa la Kenya ukapigwa na kufuatiwa na mizinga 21 ya heshima. Rais Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga, Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Spika wa bunge na wabunge wamekula kiapo cha kuilinda, kuitetea, na kuiheshimu katiba hiyo mpya kwa manufaa na ustawi wa taifa la Kenya na watu wake.Katiba hiyo mpya inabadili namna madaraka yanavyogawanywa na kusimamiwa nchini humo.
Katiba hiyo imepangwa kuzuia aina yoyote ya vurugu kama zile zilizofuatia baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, wakati zaidi ya watu elfu moja waliuawa kutokana na mgogoro wa kupinga matokeo yaliyompa ushindi Rais Kibaki. Pia ina udhibiti mkubwa kuhusu madaraka ya rais, na inatoa madaraka kwa serikali za majimbo na kuwaongezea uhuru wananchi. Miongoni mwa viongozi wa mataifa ya kigeni waliohudhuria ni Rais Omar Al Bashir wa nchi jirani ya Sudan ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita, kwa tuhuma za kuendesha mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Alikuwepo..

Akizungumzia wito wa kuitaka Kenya kumkamata Rais huyo wa Sudan, Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Moses Wetangula, amekaririwa akisema, Rais Bashir yupo nchini hapa kwa mwaliko uliofanywa na serikali ya Kenya kwa jirani zake wote kuwaomba kuhudhuria tukio hili la kihistoria., Wetangula amesema, "Huwezi kumdhuru au kumfedhehesha mgeni wako, huu si utaratibu, desturi na maadili ya Kiafrika."
Inaelezwa kuwa hafla ya kuipokea siku hiyo zilifanyika pia katika ofisi zote za balozi za Kenya zilizopo ughaibuni...hebu tuiangalie Tokyo...

SHEREHE ZILIZOFANYIKA TOKYO

Balozi wa Kenya Nchini Japani Mh. Benson Ogutu akiwahutubia waalikwa waliokusanyika katika Ubalozi wao hapa Tokyo. Ilikuwa hotuba ya kuelezea kule Kenya ilikotoka , ilipo na matarajio yao. Kulikuwa na kunywa , kula na kubadilishana maoni...fuatilia kwa njia ya picha.


Waalikwa katika hafla ya Tokyo...

Uwakilishi ulikuwepo...strong>

Wadau muhimu..strong>


Tupo na mmoja wa washiriki wa hafla hii ni mkongwe wa fani ya utangazaji kutoka Kenya Bw. Ally Attasi mwenye shati jeusi. Huyu aliwahi kuitangazia KBC miaka ya nyuma na baadaye akaifanyia kazi NHK-Japani . Hivi sasa anaishi hapa Japani akifanya shughuli zake binafsi...Take 5 Bro.

Picha ya kumbukumbu; Na Mh. Balozi wa Kenya hapa Japani Mh. Benson Ogutu .(katikati)Pamoja naye ni Mie na Mtangazaji mwenzangu wa Redio Japani-NHK, Edward Kadilo ambaye pia ni mwajiriwa wa KBC.


Mmoja wa wadau wa NHK Bi. Maureen Waweru naye alikuwepo katika hafla hiyo; hapa ni kwenye ushoroba wa Ubalozi wa Kenya hapa JP

0 comments: