Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, September 24, 2010

Kila fani ina undani wake. Nidokeze tu kitu....Ukiwa mwandishi wa habari na ukapewa jukumu la kupiga picha matukio yanayofuatana na yanayofanana , na picha hizo pengine unahitaji kuzichapisha kila siku ili wasomaji wazione unahitaji ubunifu na umakini wa hali ya juu. Pia yule anayefuatiliwa na kamera lazima naye ajue jinsi ya kukurahisishia kazi yako kwa kukupa kitu kipya...Hivyo ndivyo anavyofanya Dr. Jakaya Kikwete.Na si upande huo tu hata kwenye utangazaji pia. Hotuba ikiwa ni ile ile , pozi ni zile zile , Maikrofoni yako utaihamisha ili kupata kitu kipya...

Nakupa picha zilizonifurahisha katika msafara wa JK , (Kitaaluma na si kiitikadi, japo nami pia nina upande kama mdau)



Amekaa chini na mlemavu bi. Sara Mageni wilayani Makete , Iringa pale bibie huyo alipomuomba amnongoneze kitu fulani...

Tete tee na Bi. Halima Abdallah, mwenye miaka 102 mkazi wa kata ya Kerege wilaya ya Korogwe...


Na Mlemavu Bi. Jacquline Paulo , eneo la Rusahunga akitokea Ngara akitokea Kibondo...


Na mwanafunzi Nicholaus Haba wa Shule ya sekondari Dongobesh , Arusha...


Akiwa na wananchi wa Lupembe huko Ludewa...
(Shukrani waandishi katika Msafara)
Mdau wa MIRINDIMO kama una picha unayotaka tuiweke humu tafadhali nitumie kupitia email hii; brmsulwa@yahoo.com )

1 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mambo ya siasa pembeni, picha hizi zinaonyesha kiwango cha juu cha ubinadamu na zinagusa hisia sana.

Nadhani huyu ni rais wa kwanza kufanya hivi na kwa hili anajiweka karibu na wananchi wake kwani anaonekana kuwa ni mtu wa kawaida na mwenye kujali shida zao.