Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, March 08, 2011

Operesheni ya kuwasaka watu waliotaka kumuua aisi Joseph Kabila kabange wa Kongo DRC imewanasa watu 100 na hivi sasa wanashikiliwa katika kambi moja ya jeshi lenye ulinzi mkali mjini Kinshasa. Watu hao wanatuhumiwa kutumia silaha kali kyavamia makazi ya Raisi Joseph Kabila wakiwa na nia ya kumuua rais huyo na kuipindua serikali yake.
Mapambano makali yaliyodumu takribani saa moja yalizuka baina ya walinzi wa ikulu na kundi hilo ambapo watu saba toka kwenye kundi hilo waliuawa huku walinzi wawili wa ikulu nao wakipoteza maisha yao.Rais Kabila na mkewe hawakuwepo ndani ya makazi hayo wakati shambulio hilo lilipotokea. Itakumbukwa kuwa Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende alijitokeza kwenye televisheni ya taifa na kusema kuwa hali sasa iko shwari.

Picha inamuonyesha Raisi kabila akiwa Jijini Nairobi hivi karibuni ambapo alipokelewa na Kaimu Waziri wa mambo ya nje ya nchi hiyo George Saitoti.
Rais Joseph Kabila alichaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2006 na ana mpango wa kugombea tena katika uchaguzi ujao mwezi novemba mwaka huu.
Alirithi urais toka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuliwa mwaka 2001.
Unaweza kumuona Raisi Kabila anavyokubalika na sehemu kubwa ya Raia wake na hapa ni moja ya ziara zake alizozifanya katika maeneo ambayo kulitokea uasi...



source: www.topics.bloomberg.co

0 comments: