Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, March 08, 2011

Juzi Jumapili Polisi katika jiji la Kawasaki hapa Japani walimkamata mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 49 kufuatia kujivika kwake mavazi ya kike na kuingia katika bafu la wanawake linalotumiwa na watu wengi. Mwanaume huyo ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa Yoshio Okawara, alisema kuwa anafanya kazi ya ulinzi na anatokea Yokohama.
Kulingana na taarifa ya Polisi wa Kawasaki , iliyonakiliwa na magazeti mengi ya leo hapa Japani, Okawara aliweza kuingia katika bafu ya wanawake ambazo hujengwa kwa mtindo wa kijapani kwasababu alikuwa na nywele ndefu zilizoanguka mabegani na alikuwa amevaa sketi na koti pale alipoingia kwenye jengo hilo majira ya saa 9 na nusu mchana jana. Kutokana na hali hiyo mfanyakazi wa mapokei hakumgutukia kuwa alikuwa ni mwanaume , hivyo alimruhusu kuingia bafuni.
Okawara alikwenda kwenye chumba cha kubailishai nguo ambako aliondoa nguo zake na kuingia katika moja ya mabafu ambako wanawake watano kati ya sita waliokuwemo humo walikuwa wakiendelea kuoga. Mmoja wa wanawake waliokuwemo humo ndani alimgutukia kutokana na kuonekana kuwa mwangalifu kupita kiasi…na hivyo kutoa taarifa mapokezi . Muhudumu wa bafu hiyo ilibidi amzuie jamaa huyo hadi polisi walipofika na kumweka chini ya ulinzi.

0 comments: