Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 29, 2011

Bado hali ya kutatanisha imetanda nchini Libya hasa kufuatia kauli ya mkuu wa Baraza la mpito la taifa (NTC) Mustafa Abdul Jalil kuwa majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato, na washirika wengine lazima waendelee kuwaunga mkono waasi dhidi ya 'mtawala wa mabavu.' kwani bado Muammar QWadhafi ni tishio japo hajulikani alipo.Waasi wanasema wako katika mazungumzo na viongozi wa kikabila wa Sirte ili kuzuia umwagikaji damu, lakini mpaka sasa hawajafanikiwa.Lakini huyu Qadhafi ni nani hasa ...fuatilia makala hii..
Historia ya kisiasa ya kiongozi huyo wa Libya inaanzia mwaka 1942 . Huyu ni mto wa mkulima-bedui aliyekuwa akihama hama . Qaddafi alizaliwa katika Jangwa la Libya katika hema na akiwa kijana mdogo alionekana kuwa mwenye akili sana ambapo alimaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Libya mwaka 1963.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume. Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.
Ndoto yake kuwa ilikuwa kuuondoa madarakani utawala wa kifalme wa Mfalme Idris wa wakati huo hivyo alijiunga katika chuo cha kijeshi na kuhitimu mwaka 1965 na akaanza kupanda vyeo jeshini huku ndoto yake ikiwa ile ile ya kukamata nchi siku moja. Tarehe 1, Sept. 1, 1969, Qaddafi alifanikiwa kumpindua mfalme Idris . Na kujitangaza kutwaa madaraka ya kuwa Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya Libya na mkuu wa Baraza kuu la utawala nchini humo.Hatua ya kwanza ilikuwa kuviondoa vikosi vya wamarekani na Uingereza kutoka nchini humo mwaka 1970 na kuendesha sera ya ubinafshaji wa mali ya wageni zilizohusu biashara ya mafuta mwaka 1973.
Kwa watanzania wanamuangalia Kanli Qadhafi kwa sura mbili. Mtu anayewapenda waafrika wenzake na pia mtu aliyewajeruhi wakati wa vita vya Kagera vya mwaka 1979. Kwa sura ya kwanza , amekuwa akizisaidia sana nchi za kiafrika kwa hali na mali kupambana na umasikini na zaidi ya hilo amejenga misikiti mingi sana barani Afrika na hivyo kuwafanya waumini wengi wa kiislamu kupata mahali pazuri pa kuabudia.

Tukiviangalia vita vya Kagera , Kati ya Uganda ya Iddi Amini Dadaa nay a mwalimu Nyerere , Qadhafi alituma vikosi vyake kumsaidia Amini ambavyo vilikuwa na mchanganyiko wa wapiganaji, wanajeshi na wanamgambo lakini hatimaye walikwama kumtikisa mwalimu…
Utawala wa miongo minne wa Qadhafi umefikia mwisho wake… haijulikani hatima ya Libya kwa sasa na nini hasa Afrika imejifunza…wacha tusubiri…


0 comments: