Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, December 01, 2011

Ndege ya Shirika la ndege la Japani ANA iliyokuwa isafiri kutoka Jiji la Fukuoka kwenda Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda hapa Japani ililazimika kuacha safari yake jana Jumatano baada ya kiwango cha pombe kwenye damu ya rubani kuoneyesha kuwa kilikuwa cha juu kuliko kile kinachovumilika. Taarifa zilizotangazwa na Shirika la Utangazaji la Japani na kunukuliwa na mtandao wa http://www.japantoday.com zimebainisha kuwa ndege hiyo 246 ilikuwa iondoke Fukuoka saa mbili na nusu asubuhi , ilisitisha safari yake baada ya rubani wake msaidizi mwenye umri wa miaka 55 kuchukuliwa vipimo vya pumzi yake saa moja na nusu kabla ya kuanza safari. Viwango hivi vya pombe pia vinawahusu madereva kote nchini Japani ambapo kiwango kinachokubalika hakitakiwi kuzidi 0.15 mg/L.
Kutokana na kusitishwa kwa safari hiyo abiria wapato 240 walichelewa kwa dakika 40 na baadaye kuanza safari.
Shirika la ndege la ANA limesema kuwa rubani na msaidizi wake walikuwa wakipata kinywaji pamoja wakati wa asubuhi siku ya safari hadi kufikia saa 10 na nusu alfajiri . Inaelezwa kuwa walikunywa glasi sitaza pombe ya kijapani inayoitwa “shochu.” Msemaji wa Shirika hilo amesema kuwa ANA inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

2 comments:

ray njau said...

Viwango na masharti vimezingatiwa hapa.Kila mdau achukue hii habari kama darasa tosha katika utendaji na usimamimizi wa sheria na maadili katika seheme ya kazi na familia kwa ujumla.

jigambeads said...

This blog very interesting but you can also try these ..www.jigambeads.com and ..www.tanzaniakwetu.com for popularity and more advert to advertise. Thanks