Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 30, 2011

Hivi majuzi mdau Willy Ngoya Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa magari ya Wilna International co,iliyo na makao yake hapa Japani ambaye alikwenda Tanzania na hapo alishuhudia vituko vya barabarani vya madereva mbali na kuwepo wito kila kona kuwa 'wabadilike' kunusuru roho za watu.









(Picha na Willy Ngoya// globalpublishers)

Posted by BM. on Saturday, January 29, 2011

Posted by BM. on Saturday, January 29, 2011

Posted by BM. on Saturday, January 29, 2011

Darasa la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha kilimo , Tokyo hapa Japani...wanasema hapo wanashughulika na 'kaligrafi' , Hii ni kama sanaa ya uchoraji wa maandishi unaofanywa kwa mkono katika makundi na hapa ni maandishi ya kijapani. Maandishi yanakuwa makubwa kama mapambo kuwawesha wanafunzi kukumbuka michongo ya herufi...miongoni mwao ni watanzania wawili.unaweza kuwatambua..C. Kibona(M) na R. Kichawele (F)...safi!

Posted by BM. on Saturday, January 29, 2011

South Africa's anti-apartheid hero and former president Nelson Mandela has been discharged from a hospital in Johannesburg, where he spent two nights under intensive care. Mandela flew from Cape Town to Johannesburg on Wednesday for a medical check-up. The 92-year-old Mandela's hospital stay had stirred rumors of his death. Doctors say Mandela is fine and in good health after receiving treatment for a respiratory infection. "Medically, at present, there is no need to panic," South African military Surgeon General Vejaynand Ramlakan said. To us he is stable, but will be subject to intense monitoring,"

Mandela received thousands of messages from well-wishers while he was hospitalized.
The former president is to be under intense medical monitoring in the future, but at present, he is stable and in good spirits, the state-run BBC quoted Deputy President Kgalema Motlanthe as saying on Friday. Mandela suffers from chronic respiratory conditions, probably due to the fact that he contracted tuberculosis in prison years ago. Mandela flew to Johannesburg for his regular medical visit at Milpark hospital, but had to be admitted when doctors suspected that he needed extra intensive medical care at the hospital,
where his friends and family visited him on Thursday amid tight security measures.
Mandela served as president of South Africa from 1994 to 1999, and was the first South African president to be elected in a fully representative democratic election.
In 1962, he was arrested and sentenced to life in prison, where he served over 27 years. He spent many of those years on Robben Island. Following his release from prison on February 11, 1990, Mandela led the African National Congress party in the negotiations that led to multi-racial democracy in 1994. As president, he frequently gave priority to reconciliation. In South Africa, Mandela is often known as Madiba, his clan name, or as tata, which means father.
Mandela has received more than 250 awards over four decades, including the 1993 Nobel Peace Prize.

Posted by BM. on Saturday, January 29, 2011

Wimbi la kutaka mabadiliko ya uongozi limetanda katika Ulimwengu wa Kiarabu likitokea Tunia, linavuma Misri, Lebanon, Yemen, albania na kuna fununu Libya!
Misri...

MISRI...
Moto wa kuung'oa utawala wa miaka 30 wa rais Hosni Mubarak nchini Misri umeshika kasi, wanajeshi wameingia mitaani baada ya wananchi kupambana na polisi na kuwafanya polisi waingie mitini, Rais Mubarak amevunja ukimya wake na kutangaza kulivunja baraza lake la mawaziri. Hali ni tete sana nchini Misri baada ya wananchi kujitokeza kwa wingi mitaani kuonyesha kuchoshwa kwao na utawala wa miaka 30 wa rais Hosni Mubarak."Utawala wa Mubarak huenda ukaangushwa wakati wowote kuanzia sasa, unasimama kwa mguu wake mmoja", alisema Mohamed ElBaradei mwanaharakati aliyezawadiwa tuzo ya amani ya Nobel ambaye amerudi Misri kuunga mkono maandamano ya kuung'oa utawala wa Mubarak.Mubarak kwa upande wake ameamua kuvunja ukimya wake kwa kulivunja baraza lake la mawaziri na kutangaza kuwa baraza jipya la mawaziri atalitangaza jumamosi.
Ijumaa ilikuwa ni siku ya nne ya maandamano ya kuung'oa utawala wa Mubarak ambapo maelfu ya watu walijiunga kwenye maandamano hayo baada ya sala ya ijumaa.Ili kupunguza nguvu ya waandamanaji ambao walikuwa wakitumia mitandao ya Twitter na facebook kuwasiliana, internet ilikatwa na makampuni ya simu za mikononi yalisitisha huduma za ujumbe wa simu.Polisi walirusha mabomu ya machozi na kuwashushia kipigo waandamanaji ambapo waandamanaji nao walijibu mapigo kwa kuyachoma moto magari ya polisi na kulichoma moto jengo la makao makuu ya chama tawala cha NDP.Magari ya wanajeshi yalipoingia mitaani majira ya jioni, waandamanaji hawakupambana na wanajeshi na badala yake waliyashangilia na kusalimiana na wanajeshi huku wengine wakiyaparamia magari hayo na kupata lifti za bure.
Jumla ya watu 18 wameishafariki hadi sasa wakati maandamano hayo yakijiandaa kuingia siku ya tano.Angalia VIDEO za maandamano hayo chini ikiwemo video ya jinsi kijana mmoja wa nchini humo alivyopigwa risasi na kuuliwa na polisi.







Albania....


Lebanon
Tunisia



Yemen:

Posted by BM. on Thursday, January 20, 2011

Mwanamuziki lister Eliah , leo tulikuwa naye ndani ya studio za idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani-NHK World akitupa habari lukuki juu ya maisha yake ya kimuziki.Mwanamuziki huyu ana historia ya kusisimua sana .
Alianza kupiga piano akiwa na miaka mitano na baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari akajiunga na bendi ya King Kiki Double O ya Kikumbi Mwanza mpango Kiki, Sambulumaa, Bene Bene , Safari Sound Ochestra na baadaye M.K Group.Baadaye akajiendeleza Kimuziki huko Tanzania, nchini Austria na baadaye hapa Japani ambako sasa ameweka makazi yake.


Kukukumbusha tu wanaoujua wimbo original wa Sambulumaa Kadiri Kanshimba , kinanda kimepigwa na Lister.Tumeongea mengi na mwanamuziki huyu , hivyo ukitaka kumsikia kulia kwako kuna mitandao rafiki (Bofya NHK World) kisha angalia kipindi cha leo Alhamisi. Kwanza kuna habari zinzomuhusu mwalimu wa Iraq na ziara yake hapa Japani na baadaye mahojiano na Lister. Ilikuwa siku nzuri sana .Pata vionjo vya kinanda.

Pia unaweza kumpata kupitia mtandao wake wa : www.listerelia.com

Lister Eliah akiondoka mjengoni...

Posted by BM. on Wednesday, January 19, 2011

Tulio wengi twapenda kutafuna Chingam, wengine wakiita bazoka , Big G, n.k lakini ikiwa utaitafuna tafadhali sana ujue mambo mbalimbali yanayokukabili kiafya.

1. Utafunaji huo wa Chingam unazeesha tishu ambazo hufanya kazi mithili ya shokomzoba katika viungio vya taya lako. Eneo hili likitumika mno linaathirika na hivyo kukuletea maumivu na kukukosesha raha maisha yako yote.
2. Ufahamu kuwa unatumia misuli nane tofauti ya usoni . Utafunaji usio wa lazima wa chingamu unawezakukuletea hali sugu ya ya kukaza misuli katika misuli ya aina mbili ama tatu kati ya hiyo nane ili karibu na panja (paji la uso) lako. Hali hii husababisha msukumo katika neva ambazo zimesambaa katika eneo hili la kichwa chako na hivyo kukusababishia kipandauso (Kichwa kuuma kupita kiasi) au hali ya kukosa raha.
2. Ujue kuwa wewe una gland mate (Saliva glands) zilizopo katika kinywa chako chote ambazo huchochea utengenezaji na utoaji wa mate wakati unapotafuta chingamu. Utoaji huu wa mate kwa hakika tunaweza kuuita kuwa ni matumizi mabaya ya nishati na rasilimali ambayo ingeweza kutumika kwa shughuli nyingi za umetaboli (Metabolic activities) katika kinywa.

4. Nyingi ya chingamu unazotafuna ni tamu, na hii imetokana na kupakwa kiambato kinachoitwa aspartame. Matumizi ya muda mrefu ya aspartame yanaweza kukusababishia kansa , kisukari , kuvurugika kwa mfumo wa ( Mfumo wa neva) na hitilafu wakati wa kujifungua. Na hata kama chingamu hiyo imepakwa tu sukari unaweza kupata matatizo kama hayo kwa kuanzia na mihemko isiyo ya kawaida.

3. La msingi hapa ni kuwa unapotafuna Chingamu ujue kuwa kuna hasara zake pia na hivyo jizuie kuifanya kuwa ndio kawaida yako ya maisha …itakugharimu!
(Kutoka vyanzo mbalimbali vya mitandao ya kiafya)

Posted by BM. on Monday, January 17, 2011

Tanzanians spent a whopping TSh555 billion ($396 million) on phone calls and text messages in three months, according to a new report by the Tanzania Communications Regulatory Authority. The money was spent between July and September last year.


According to the TCRA report, the amount was spent by about 20,771,487 subscribers who were, by September 2010, receiving services from seven telecommunications firms, including Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel, TTCL, Sasatel and Benson Informatics.
The subscribers’ expenditure covered both voice communications as well as short message services (SMSs).

The amount is slightly higher than the total government revenue for September 2010, which stood at TSh502.5 billion. In the preceding quarter, Tanzanian phone users spent Sh37.475 billion less, indicating that telephone number registration and tariff battles did not have a negative impact to firms’ revenue as previously thought.
By NATION CORRESPONDENT-Kenya.

Posted by BM. on Monday, January 17, 2011

Posted by BM. on Sunday, January 16, 2011


Habari za punde kutoka Johannesburg nchini Afrika kusini zinadokeza kuwa , uvumi umezagaa jijini humo kuwa Raisi wa zamani wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela yu taabani anaumwa na hali yake ni majaaliwa.


Msemaji wa mfuko wa Nelson Mandela Sello Hatang alkanusha taarifa hizo jana jumamosi na kusema Mzee Mandela mwenye miaka 92 alikuwa katika mapumziko na mkewe Graca Machel na kwamba walikokwenda na wanachokifanya ni siri yao wawili na ni haki ya faragha.
Hata hivyo kuna habari kuwa hali ya mzee huyo imezorota mno na wengine wamekuwa wakiwasiliana wakisema kuwa amekufa ja,bo ambalo limekanushwa vikali na watu wake wa karibu.Hata hiyo vyanzo vya uhakika vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeonyesha kuanza kukubaliana na uvumi huo.
Source: www.news24.com/SouthAfrica

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Mtu mmoja mwenye miaka 52 amekamatwa jana jumatano huko Kobe hapa Nchini Japani kwa kumuandikia ujumbe binti mmoja mwanafunzi amtumie picha zake akiwa uchi mtupu , akituhumiwa kuvunja sheria inayokataza matumizi ovyo ya picha chafu.
Mtuhumiwa huyo amefahamika kwa jina la Nobuhito Mizohata, aliyetuhumiwa kutumia picha bandia inayomuonyesha kama kijana akiwa katika eneo la miadi kwa lengo la kumshawishi binti wa miaka 16 anayeishi huko Nagoya.

Taarifa za kipolisi zimebainisha kuwa ombi la Mizohata lilifanikiwa na alipokea picha za binti huyu akiwa uchi aliyoichukua kwa njia ya kamera ya mwezi septemba mwaka jana simu yake ya mkononi .
Polisi walimnukuu Mizohata akisema kuwa “Nataka mabinti wadogo na nilitaka picha wakiwa tupu kutoka kwao “Baada ya kuangalia kile alichokifanya Mizohata katika komputa yake , Pilisi waligundua picha nyingi mbalimbali na ndipo walipomuhoji ni mara nyingi kiasi gani amekuwa akifanya hivyo kabla hajaingia kwenye mtego wa polisi

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Mahakama ya hakimu mkazi katika eneo la Utsunomiya hapa Japani leo Alhamisi imemjulisha rasmi mtu aliyeachiliwa huru kutokana na kesi ya mauaji ya mwaka 1990 kuwa atapokea takriban yeni Millioni 80 (takriban (Fedha za kitanzania -1,360 millioni ) kama fidia kutokana na kuhukumiwa kwa makosa .
Mji wa Utsunomiya...

Kiasi hiki ndicho alichodai kulipwa kama fidia.Toshikazu Sugaya, mwenye miaka 64, alidai alipwe fedha hizo mwezi Septemba mwaka jana chini ya sheria ya fidia ya masuala ya kijinai kutokana na msongo mkubwa wa mawazo aliyokabiliana nao katika kipindi cha miaka 17 na nusu alichokaa gerezani.Sugaya alinukuliwa akisema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka Mahakamani kuwa “Kiwango hicho ni sawa ‘‘. Mjapani huyo, Sugaya alifungua madai ya fidia baada ya mahakama kumuona kuwa hana hatia pale kesi hiyo iliposikilizwa upya mwezi machi mwaka uliopita akihusishwa na kifo cha binti mdogo wa miaka minne huko Ashikaga, mkoani Tochigi.
Toshikazu Sugaya alikamatwa mwaka 1991 na alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2000 na ndipo alipokata rufaa na kesi yake kusikilizwa upya mwaka 2001 na kuibuka kidedea na millionea. Ingawa awali mahakama hiyo ya ilitupilia mbali ombi hilo mwaka 2008 , Mahakama ya kuu ya Tokyo iliipokea rufaa hiyo kutoka kwa mwanasheria wake akiwakilisha matokeo ya vipimo vipya vya vinasaba -DNA , May, 2009 ambavyo vilithibitisha kuwa hana hatia na wala hakuhusika kabisa na mauaji hayo. Mwezi mmoja baadaye aliachiliwa huru kutoka gerezani.

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Japani wakati huu ni wa kipindi cha baridi...watu wakiwa ndani ya majumba yao huvaa viatu vyepesi mithili ya masponji kujikinga na baridi...ndipo ubunifu unapoanzia...!

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Hapa Japani kuna maeneo mengi ya kuabudia , kando ya barabara , viwanda na hata maeneo ya kibiashara . ambapo waumini wa Kibuddah na Shinto hufanya ibada mbele ya miungu yao ...kila mtu kwa imani yake.



Posted by BM. on Friday, January 14, 2011






Posted by BM. on Thursday, January 13, 2011

Mieleka ya sumo ni mchezo maarufu nchini Japani ulioanza miaka kwa maelfu .

Mchezo huu sio tu ulianza kama njia ya kuonyesha ushujaa lakini pia ulihusiana na imani za kidini na zamani (Miaka elfu kadhaa ) ulichezwa pia katika madhabahu ya kishinto huko Ugiriki, Babylon, Misri ,Sumaria, na nchini India na mnamo mwaka 776 BC ulifanya kama njia ya kushindanisha wababe.


Mchezo unaotumia nguvu nyingi baina ya watu wawili wanaofahamika kwa kijapani kama rikishi , na mshindi anapimwa kwa kumtoa mpinzani wake nje ya ulingo ‘dohyo’ ama kumuangusha chini . Mchezo huu ulianzia Japani na hadi sasa ni nchi pekee inayoendesha ligi ya kulipwa ya mchezo huu .Mchezo huu unahusishwa na masuala ya kitamaduni ya ukale yanayoonyesha ushuja na unahusiana pia na imani za kidini za hapa Japani nah ii inajitokeza pale chumvi inapotumika kama moja ya kitendea kazi wakati wa mashindano ambapo wanamieleka huimwaga kila kona ya jukwaa lao kuondoa mikosi.
Kama ilivyo kwa michezo mingine , wachezaji wa sumo wa kulipwa hapa Japani wamewekwa katika madaraja kadhaa unaweza kuangalia huo mchoro . Daraja la chini kabisa ni Jonokuchi na la juu ndio hilo Yokozuna.

Posted by BM. on Sunday, January 09, 2011

Somalis say Islamist insurgents al-shabab have banned unrelated men and women from shaking hands, speaking or walking together.

Residents of the southern Somali town of Jowhar said Saturday that the al-Shabab insurgents threatened to whip, imprison or execute anyone found breaking the recent edicts.Resident Hussein Ali says he will no longer greet women he knows for fear of punishment.

Student Hamdi Osman says gunmen are searching buses for improperly dressed women or women traveling alone. She says she was once beaten for wearing Somali traditional dress instead of the long, shapeless black robes favored by the fighters.The insurgents have already banned women from working in public, leaving many families completely destitute.


Sheik Ali Mohamud Rage, a spokesman for the al-Shabab militia. (AP Photo/Mohamed Olad Hassan)

Posted by BM. on Saturday, January 08, 2011

Posted by BM. on Saturday, January 08, 2011

Wananchi wa Sudan Kusini wanajiandaa kupiga kura kesho Jumapili ili kuamua kama wanahitaji kuwa na taifa lao ...inavyoelekea wanataka kujitenga kama bango hapo linavyoonyesha...


Nyuso za raia wa taifa jipya linalonukia...


Wadada wa Sudani Kusini wakivinjari Huko Juba wakati wakiisubiri kesho J2 wakapige kura kuamua kama waendelee Kuwa chini ya Sudan ya Muungano au wawe na taifa lao...

Posted by BM. on Saturday, January 08, 2011