Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 31, 2009


Chama kikubwa cha Upinzani nchini Japani cha DEMOCRATIC kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Baraza la chini la Bunge, uchaguzi uliofanyika jana Jumapili. Baraza hilo ndilo linalomchagua Waziri mkuu wa JAPANI. Ushindi huu umekiondoa madarakani chama cha LIBERAL DEMOCRATIC cha waziri Mkuu TARO ASO kilichokaa madarakani mwa miaka 54 mfululizo. DEMOCRATIC Kimekusanya viti 308 kati ya 480 na bila shaka sasa Raisi wa chama Yukio Hatoyama hapo juu, katikati anayeonekana vyema…anakuwa Waziri Mkuu. TARO ASO amekaa madarakani kipindi kifupi sana chini ya mwaka mmoja lakini mambo yake ya kisiasa yamekuwa ndivyo sivyo. Angalia heka heka za uchaguzi za jana Napiga kura sasa...Mshindi utamsikia tu!
Fasta tupeleke..
haya tuhesabu
Hatimaye Waziri Mkuu Taro Aso , kura hazikutosha...Ameshasema atajiuzulu uongozi wa Chama .

Posted by BM. on Monday, August 31, 2009

Jana nje ya jengo la NHK hapa japani na bustani za Yoyogi kulikuwa na tamasha la Ngoma na burudani nyinginezo . Ilipendeza. Shughuli hiyo ilikwenda sammbamba na upigaji wa kura . Hebu suuza macho
Kwa raha zao..
shuhuda

Mpatempate..

Posted by BM. on Saturday, August 29, 2009

Unamfahamu Mzee Nelson Mandela Vizuri?.Tabia na maisha yake binafsi?. Ninini nafasi ya wanawake kuwafanya waume zao kuwa wakutumainiwa..Fuatilia maelezo haya ya Mkewe Mama Graca Mandela katika mahojiano maalum na Kituo cha TV za Aljazeera..

Posted by BM. on Saturday, August 29, 2009

Raisi barack Obama na familia yake wakiwa katika mapumziko Martha's Vineyard, Mapumziko ya wakubwa chini ya Ulinzi mkali, hakuna nanihii..

Rais Obama akiendesha baiskeli huku akimwangalia binti yake Sasha akijiandaa kupanda baiskeli yake Hii ilikuwa mapuzikoni Martha's Vineyard wiki hii.
Ulinzi kila upande..

Posted by BM. on Thursday, August 27, 2009


Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mke wake mama maria Nyerere Enzi za ujana wao.

Posted by BM. on Wednesday, August 26, 2009



Mmoja wa vijana wanaounda Bendi ya "Ochestra Udzaugale" akiwa ameshikilia redio ambayo hutumika kama spika wakati walipokuwa wakitumbuiza katika hafla moja huko kwetu Nkoogwe, Ntanga.Bendi ina gita moja na Redio kama spika. Wangekuwa na vyombo hapo wangekuwa mbali.

Posted by BM. on Wednesday, August 26, 2009

Wanenguaji wa Msondo Kutoka kushoto ni Amina Said (Queen ), Saidi Kinacho na Mama nzawisa wakiwa kibaruani katika viwanja vya leader.Mnenguaji wa bendi ya muziki wa dansi ya MSONDO NGOMA Kinacho Said ( mama nzawisa)akichezea kwa umahuiri huku akiwa amemwekea mguu juu ya mabega Mwimbaji na mpiga trampeti wa Bendi hiyo wake Romario Mng”ande
Mugongo mugongo He!

Posted by BM. on Tuesday, August 25, 2009


Wakuu...

Posted by BM. on Tuesday, August 25, 2009

Mazishi ya kaburi moja kwa miili ya wanafunzi 12 yamefanyika leo jumanne katika shule ya wasichana Idodi mkoani Iringa baada ya Bweni lao kuteketea kwa moto. serikali imetangaza kuifunga shule hiyo huku ikiitaja hasara iliyopatikana , mbali na roho za watu kuwa ni shilingi milioni 105, Tukio la kusikitisha Ni wakati mgumu kwa kila mtu. Naomba tuhudhurie tukio hilo kwa njia ya picha hizi. Picha nyingine za kutisha lakini nahitaji kukupa picha halisi.
KUMRADHI, Pole sana kwa kustuka.... Naomba tugawane majonzi ya vifo hivi ; Pole sana mtazamaji. Haya ni baadhi ya Mabaki ya watoto wetu walioteketea kwa moto.;
Inauma lakini kazi ya Mungu haina nini makosa...
Mwl. mkuu akielekea kuonana na Waziri Mahiza kutoa taarifa ya tukio hilo...simanzi
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Idodi Bw Raymond Mlasu, akiangusha kilio mbele ya Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantum Mahiza mara baada ya kumaliza kutoa taarifa kamili kwa waziri juu ya mkasa huo. Picha zote na FrancGod kutoka Iringa..

Posted by BM. on Monday, August 24, 2009

Illuminata kutoka Tz kura hazikutosha.
Msikilize hapo....
Illuminata aukosa ushindi wa Miss World Universe lakini aliliwakilisha vizuri taifa la Tanzania...
Miss Tanzania Illuminata Wize, katikati and Miss Australia Rachael Finch, kulia huko Bahamas nyumba wakifuatiwa na miss Miss Lebanon Martine Andraos na Miss Jamaica Carolyn Yapp.Kura hazikutosha za majaji.

Posted by BM. on Monday, August 24, 2009


Usafiri eneo la Niger Delta , Nigeria...

Posted by BM. on Monday, August 24, 2009

Mmoja wa waliopiga kura Janet Metcalfe katika maombi mafupi kabla ya kuendelea na mchakato
Mashoga wakiwa wameshikana mikono wakiwa katika maandamano ya kudai haki yao kutambulika na kanisa hilo , hatimaye wamefanikiwa.
Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani limepiga kura na kuruhusu wasagaji na mashoga kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini humo.
Uamuzi huo wa kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini Marekani unaonekana kuzusha mzozo na unaweza kuwagawanya wanachama wake milioni 4.6 waliopo nchini humo.
Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani (ELCA) ambalo lina dayosisi zipatazo 10,000 nchini Marekani, lilipiga kura ijumaa jioni kubadilisha baadhi ya vipengele na kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na pia kuwapa nafasi za kuwa na vyeo mbali mbali kwenye makanisa.Baada ya majadiliano makali, wawakilishi wa kanisa walipiga kura 559 za kuunga mkono kulinganisha na kura 451 zilizokuwa zikipinga wazo hilo, alisema mkurugenzi wa habari wa kanisa hilo John Brook.Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani sio la kwanza nchini Marekani kutoa uamuzi huo wa kuwapa mashoga na wasagaji nafasi za uchungaji na uongozi katika makanisa. Kanisa la Episcopalian la nchini Marekani lilishawahi kutoa uamuzi kama huo.Hata hivyo uamuzi huo wa kanisa la kilutheri la Marekani haukupita kirahisi, kwani kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa wachungaji mbali mbali akiwemo mchungaji Richard Mahan wa dayosisi ya Maryland magharibi, Virginia.

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009


Kituo cha treni cha Kyodo nikiwa njiani kuelekea Wait Haus ..

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009


Viwanja vya Yoyogi Park leo vilichangamka , Muziki wa Hip Pop, maonyesho ya magari na vilaji...hebu fuatilia kilichotokea kwa njia ya Picha..

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009

Pamoja na maonyesho ya Hip Popp kula na kunywa kwa wanaotaka pia kulikuwa na maonyesho ya magari , japo machache lakini watu waliyazungukia ...
Hebu tulikague hili aina ya HAMMER..

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009

Leo ilikuwa Mshike mshike katika Viwanja vya Yoyogi Park , Tokyo vijana walipokusanyika kujiburudisha kwa muziki wa Hip Pop , Hebu fuatilia nawe usuuze macho..



Mzuka

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009

Kila mtu na Kijitaulo a .. Ruhsa...

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009

Usiulize kuna nini ndani ...soma hapo
Wataalamu

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009


Jamaa anaonyesha umahiri wake wa kuchora akipata tena hayaa!

Posted by BM. on Sunday, August 23, 2009


Dereva kakamatwa maeneo ya Shibuya , Tokyo baada ya kucheza rafu barabarani ...hakuna majadala ni faini tu.

Posted by BM. on Saturday, August 22, 2009

Rais Barack Obama wa Marekani amewatakia waislamu wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao umeanza leo sehemu nyingi duniani. "Kwa niaba ya Wamarekani, waislamu wa Marekani na waislamu duniani kote nawatakia Ramadhan njema , Ramadhan Karim" alianza kwa kusema rais Obama. "Mwezi wa Ramadhani ndio mwezi ambao waislamu wanaamini quran tukufu iliteremshwa kwa mtume Muhammad (S>AW) kwa kuanzia na neno Iqra" anasema Obama. Katika ujumbe huo Rais Obama anasema mwezi wa ramadhani unawakumbusha waislamu kufanya mambo mazuri ambayo pia wakristo katika dini yao wanatakiwa kuyafanya.Salaam za Raisi Barack Obama kwa waislam..

Posted by BM. on Saturday, August 22, 2009

Huu ni msikiti wa madina wakati ambapo hakuna pilikapilika za hijja. Waislamu nchini Japani wameanza kufunga kama ilivyo kwa waislamu wengine kote ulimwenguni.Tangazo limetolewa kwa waislamu waliopo Japani huduma ya futari na daku itakuwepo katika mgahawa uliopo karibu na Club ya zamani ya Masaya iliyopo iliyopo Odakyu Sagamihara .Chakula kitaandaliwa na Ma-cheff waliobobea Bi. Tatu Bwela na Sabina Itambiko. Kwa mujibu wa waandaazi vyakula vitakavyohudumiwa ni pamoja na FUTARI-Muhogo wa nazi na samaki,nyama ya mbuzi,kuku,muhogo wa nazi(sukari) ,viazi vitamu, tambi za nazi za kukaanga,--Maandazi ya maua,vibibi, vipopo,tende halua.-Viazi mviringo na nyama ya kusaga na uji wa pilipili.Kwa mkazi wa Japani anaweza kuwasiliana na wahusika kwa simu ya viganjani kupata ramani na utaratibu. Kila la Kheri.
-

Posted by BM. on Saturday, August 22, 2009

Mwezi mtukufu ukiwa umewadia , wauzaji wa vyakula maalum vya futari na daku nao wanachangamkia soko. Maboga yakiwa tayari katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.

Posted by BM. on Saturday, August 22, 2009

Mmoja wa watu akiwa akasakata rumba eneo la ruaha Mbuyuni Kilolo, Iringa usiku wa kuamkia jana ...eti akivunja jungu , kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani ..hii imekaaje.
...Na kondom tena mkononi?...ndio kuvunja jungu huko au kufanya mas-hara!Photo na FrancIbra.