Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009


Kwahiyo...

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009

Captain Dadis Mussa Kamara...
Muungano wa Umoja wa Ulaya, umetoa wito kuwa kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kaptain Mussa Kamara afikishwe mbele ya Mahakama kukabili mashitaka ya ukiukaji wa haki za kibinadamu, wakati wa kuzuia maandamanoambayo yaliandaliwa vyama vya upinzani.Kwa mujibu wa mjumbe wa maendeleo ya umoja wa ulaya,Karel de Gucht, alisema yakuwa mkuu huyo wa jeshi,Kaptain, Mussa Kamara,anahusika na mauaji ya watu wasipungua 150, wakati walipouwawa, tarehe 28, Septemba,mwaka huu.Hata hivyo , kiongozi huyo anasema kuwa hahusiki na mauaji ya watu hao.
Vurugu za Konakri, Guinea na mabavu ya Dola!

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009



Bustani mpya ya Forodhani Zanzibar ambayo ukifika huko hujulikana kama “Bustani ya Foro” inavyoonekana hivi sasa baada ya ukarabati

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009


Bro KM akiwa katika Pozi huko South Africa...take 10.....

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009

Mwandishi wa habari Mkongwe Ali Saleh Alberto anayeifanyia kazi BBC kule Zanzibar katika moja ya darasa lake kwa waandishi wenzake.

Posted by BM. on Saturday, October 31, 2009


Shirika Moja linalohusika na masuala ya Afya la Lung Foundation limesema kuwa watu millioni 6, watapoteza maisha kutokana magonjwa yanayosababishwa na uvutaji wa sigara, ifikapo mwisho wa mwaka ujao wa 2010.Limesema yakuwa watu wengi watakao athirika ni wale wanao toka kwenye dunia ya tatu au nchi masikini duniani kwakuwa uvutaji wa sigara katika bara la Amerika na za Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea umepungua kwa kiasi, lakini uvutaji wa sigara umeongezeka katika nchi masikini. Eeeh Balaa!

Posted by BM. on Friday, October 30, 2009

Haya nakuunganisha na Dada Anyango , uone vipaji na jitihada za mdada huyu wa Kijapani . Nimekubali kuwa mambo mengi yanawezekana la msingi dhamira...

Posted by BM. on Friday, October 30, 2009

Ama kwa hakika , tumetoka mbali ..we acha tu.Leo nakuchukua hadi Rungwe Sekondari , shule iliyopo wilayani Rungwe , mkoani Mbeya kwa njia ya picha... nikuonyeshe shule niliyosoma, . picha kwa hisani kubwa ya Bro. Mwambegele. Hapo Kiwira mwankenja ni kilometa 15 tu kutoka Tukuyu Mjini. Km kama mbili tu kutoka hapo utaona kibao kinachokuonyesha njia ya kwenda shuleni kwetu!

Ehee hapo chepuka kulia moja kwa moja hadi Rungwe Sekondari ,chini ya Mlima Rungwee!
Mbele ya jengo hilo ndio muonekano wa Mbele , ambako kila asubuhi tulikusanyika hapo kuelewa majukumu ya siku, kukaguliwa usafi. "Asembli". Na mwanzoni mwa mwaka kuna wengi walikuwa wakiadhibiwa hapo kwa kuwabughudhi "Mugya" , jina walilokuwa wakiitwa wanafunzi wa kidato cha kwanza. Sijui leo pakoje hapo!

Ofisi za waalimu ghorofani na madarasa hapo chini...inanikumbusha mbaali.

Posted by BM. on Wednesday, October 28, 2009

Wale wapenzi wa Rhumba la kutotoa jasho wanaweza kubofya hapo wakaburudika na tungo za Koffi Olomide.... Jamaa kajipanga au unasemaje!

Posted by BM. on Monday, October 26, 2009

Jana Jumapili kulikuwa na Maonyesho ya bidhaa za mashambani hapa Tokyo , Japani na katika pitapita yangu nikakutana na banda lina kanga , vitenge , kahawa na bidhaa nyingine kutoka Tanzania. Banda hili ni la Polepole, kamera yangu ikapata hii...
Hapo nimekutana na Mr. Tamura , Mkuu wa banda la Polepole linalouza bidhaa za Tanzania. Tumezungumza sana akinipa hadithi za Moshi na Arusha anasema "Kule safi saaana". Watu kama hawa wanaoitangaza nchi yetu wanastahili kutambuliwa na kuheshimika sana...wahusika mnasemaje!
Kahawa kutoka umatengoni...Mbingaa aisee!
Sabuni za mwarobaini zilikuwepo!

Posted by BM. on Monday, October 26, 2009

Wikiendi kulikuwa na zoezi la jinsi ya Kujiepusha na majanga kama vile matetemeko, moto na majanga mengine lililofanyika katika Uwanja wa Yoyoygi hapa Tokyo nami nilishiriki ...
8.8 nikiwango che ukubwa wa tetemeko ...mtikiso mkali mithili ye tetemeko kutoka kwenye gari maalum. Wataalamu wakitoa maelekezo jinsi ya kufanya...du! Tetemeko linaposhika kasi unafanyaje? Sasa zoezi la moto... Huu ni mfano wa nyumba...Moto umewaka na ndani kuna moshi mwingi unafanyaje...wataalamu wanasema kuwa monyi unatabia ya kushika sana juu kwanza hivyo chuchumaa na ikibidi tembelea kifua unaweza kusalimika. Wacha nijaribu...
Nimetembelea kifua ndani kwa ndani na kutoka!

Posted by BM. on Saturday, October 24, 2009

Ensenene! Jiko sanifu!
Palee!
Nkuruma!
Du!

Posted by BM. on Monday, October 19, 2009


Ilikuwa tarehe mosi may, 1961 Pale Nelson Mandela, alipoonyesha msimamo wa kupambana na ubaguzi wa rangi na ndipo mwandishi wa habari wa shirika moja la habari la ITN Brian Widlake alipomfuata kwa minajili ya kufanya naye mahojiano. Unaweza kuona Ushupavu wa uthabiti wa viongozi wa Nyakati zile na viongozi wa sasa na nini changamoto zetu...

Posted by BM. on Monday, October 19, 2009


Ukilimudu zoezi hili la kwanza ..sema tuendelee na la Pili... lawama!

Posted by BM. on Monday, October 19, 2009


Taswira unaionaje ...supaa!

Nami nilikuwepo..

Mandhali katika Bustani ya Yoyogi hapa Tokyo. Kama naiona Mnazi mmoja vile! ...

Posted by BM. on Saturday, October 17, 2009


Waungwana mnalionaje hili!

KP!

Posted by BM. on Saturday, October 17, 2009


msg sent!

B/H

Posted by BM. on Friday, October 16, 2009


Broadcasting House':Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji la Japani -NHK ,mwonekano la Jengo upande wa Magharibi kusini leo Ij mchana ...

Posted by BM. on Friday, October 16, 2009

Disco la uhakika lilifanyika siku chache zilizopita katika ukumbi wa SAGAMINO TROPICAN PUB , uliopo karibu na kituo cha train cha Sagamino (Sotetsu line)nchini Japani. Tunakusogeza ndani ya Ukumbi huo kushuhudia baadhi ya vishangwe!









We acha tu!
Full Shangwe!

Posted by BM. on Thursday, October 15, 2009


Namleta huyu jamaa ....ametumia kipaji chake cha kuwasilisha hoja kwa njia ya vichekesho lakini kwa hekima kubwa...nawaza hivi inawezekana kumbe kuwa na vitu kama hivi kwa wasanii bila kutumia nguvu nyingi studio kama lile kundi letu nyumbani.

Jikumbushe na huyu Jamaa...

Posted by BM. on Wednesday, October 14, 2009


Ushawatambua au giza! Ok..

Posted by BM. on Wednesday, October 14, 2009


Ilikoanzia...

Posted by BM. on Saturday, October 10, 2009

Kabla ya kusoma habari hiyo kwa kina , kwanza burudisha macho kwa Picha za Raisi Barack Obama akiwa katika matukio tofauti.


Rais wa Marekani, Barack Obama, ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2009.Kamati kuu wa tuzo ya Nobel imesema kiongozi huyo ameshinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake kuimarisha uhusiano mwema kati ya watu wa dunia. Kamati hiyo ilitaja moja wapo wa juhudi za Obama katika kuunga mkono mashirika ya dunia kuafikia kuwepo na ulimwengu bila silaha. Msemaji wa Bw Obama amesema rais huyo amepokea taarifa hiyo kwa unyeyekevu. Msemaji huyo alimuamsha rais Obama punde tu habari hizo kutangazwa. Jumla ya watu 205 waliteuliwa kupata tuzo hiyo, akiwemo Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na mwanaharakati wa mageuzi nchini Uchina Hu Jia. Mshindi wa tuzo ya Nobel hupokea medali ya dhahabu, cheti cha diploma na dola milioni 1.4.Tangu kuchukua hatamu za uongozi rais Obama amesimamia masuala muhimu ya dunia ukiwemo mpango wa amani Mashariki ya Kati na kutoa nafasi ya mazungumzo kuhusu mpango wa Iran wa nuklia. Baadhi yawatu hususan wanasiasa wanahoji uamuzi wa kamati hiyo ya Nobel kuwa Obama hakustahili kwakuwa ameonyesha nia na hakuna vitendo ambavyo tayari vinaonekana vya upatikanaji wa amani duniani. Lakini Ukweli unabaki kuwa nadharia na dhamira ya dhati ya Kiongozi wa taifa kama Marekani ni muhimu kubadili mitazamo ya dunia iliyokatika uhasama na vurugu kubwa za kivita.

Posted by BM. on Thursday, October 08, 2009

BOFYA HAPO: Utapata taarifa ya kina kwa njia ya video juu ya Kimbunga cha Jana Alhamisi kilichotokea hapa Japani kutoka BBC. Kimbunga cha Melor kimepita katika maeneo mengi nchini Japani leo Alhamisi na kupoteza maisha ya watu watatu na wengine 56 wakiachwa na majeraha. Kimbunga kinachofanana na hiki kilitokea miaka miwili iliyopita lakini kile kinachokumbukwa zaidi ni cha mwaka 2004 kilichopoteza maisha ya watu 95. Hali ya leo imevuruga ratiba za ndege , reli na barabara.
Kimbunga kilianza katika mkoa wa Aichi katika rasi ya Chita alfajiri saa 11 na kuvuma kuelekea Kaskazini mashariki kuhu kasi yake ikipungua taratibu nah ii ni kwa mujibu wa Shirika l Utabiri wa hali ya hewa ya japani. Huko Minabe, Mkoa wa Wakayama Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Hiroshi Kitahara mwenye miaka 54 alipoteza maisha baada ya kuzidiwa na upepo alipokuwa juu ya baiskeli yake akisambaza magazeti asubuhi subuhi kazi zinazofanywa sana hapa Japani katika jitihada za kuharakisha habari kwa wananchi. Hiroshi alijikuta ghafla akiparamia mti ulioangushwa na upepo mbele yake kifo ambacho kinafanana na kile kilichomkuta Masaichi Kaji, 69 ambaye alipigwa na tawi la mti kichwani akiwa karibu na hekalu huko Fujimi mkoa wa Saitama dhahiri ikiwa ni kujisalimisha katika eneo takatifu.Zaidi ya safari 440 za ndege za ndani na za kimataifa zilisimamishwa na hata treni ziendazo kasi pia zilisimama kwa muda hapa Japani kupisha kimbembe cha kimbunga. Shule zote za msingi na sekondari za chini jijini Tokyo hasa za kwenda na kurudi nyumbani zilisitisha masomo leo.
Taarifa za uhakika zinabainisha kuwa hakuna raia wa Tanzania au nchi nyingine barani Afrika alipoteza maisha wala kujeruhiwa. Mwandishi wa habari hizi alisafiri mapema asubuhi katika treni kuelekea Shibuya , katikati ya Tokyo saa mbili asubuhi katika treni iliyojaa pomoni kuwahi makazini na hali ya taharuki ilionekana nyusoni mwa watu. Hata hivyo ilionekana dhahiri kuwa watu watu walikuwa nahabari za kutosha juu ya tukio hilo na jinsi ya kujikinga na madhara.