Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, September 30, 2008

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania wanaoishi Japani Dr. Simba Ally (Kulia) na mwenyekiti wa Jumuia ya watanzania waliopo Italy Bw. Abdulrahaman A. ali wakiwa katika mazungumzo ya kiuongozi huko Italia ambako Dr. Simba anafanya ziara rasmi ya kikazi.

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Maonyesho ya waIndia, Tokyo jamaa wanapata msosi na vinanihi pembeni .

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Leo katika viwanja vya taifa vya Yoyogi viunga vya Tokyo kulikuwa na maonesho kabambe ya vitu, watu, matukio na kazalika kutoka kwa watu wa India. Ilikuwa haine haine ya aina yake. Jamaa walijitangaza vilivyo.

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Tembo wa Serengeti unaweza kumkalia namna hiyo..subutu! lakini mie nimeweza, kizibiti hicho.

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Akina mama wachoraji kutoka Bombay walikuwepo.

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Miaka ile majumba ya avalon, Starlight , Cameo na mengineyo yalikuwa dili. eksibisheni leo ilikuwa laivu

Posted by BM. on Sunday, September 28, 2008

Moja ya kivutio katika maonyesho haya ni baiskeli hizi ambazo zina injini ukichoka kunyonga unakanyaga mafuta!

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Viti vikiwa tayari kwa ajili ya Mwenyekiti wa EU na Raisi wa Tz..MhJK.

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Mh.Raisi Jkaya kikwete alitupa fursa wadau wa NHK kupiga picha naye akitokea kwenye mkutano wa G8 Hokkaido hapa Japani.

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Mhariri wa makala ya habari Gazeti la Mwananchi Rashid Kejo -katikati asiye na koti-akiwa katika pozi. Siku hiyo hakutinga mkoti, lakini shingoni ilikuwepo(Picha na Mwananchi)

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Ridhwan JK akiwa na waifu wake siku walianza nyu laifu kama wanandoa..take 5.

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Picha baada na mazungumzo ya kidiplomasia na Mhishimiwa Meyor.

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Mkude Meya wa Tokyo akichakarika.

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

hapo hapo!

Posted by BM. on Saturday, September 27, 2008

Mtaani kwa bm setagaya-Chitosefunabashi asubuhi ya leo kijua kikalii

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Watu walio wengi nchini Japani wanapenda sana kutumia usafiri wa baiskeli kwa safari za hapa na pale kwasababu nyingi tu ikiwa ni pamoja na kuchangamsha kifua. Si unaona inavyopendeza.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe...hapo sasa.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Mdau Khalifa akiwa ndani ya pozi waiti haus -yake keptauwn. S.A

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Leo Tokyo, nyuzi joto ni 30 kwa kipimo cha selisyasi . lazima ubebe kipepeo.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Wengine wanacheza , wengine wanauza vitu vyao vidogovidogo kwa bei poa!

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Majira ya joto yanaelekea ukingoni sasa na majira ya pukutizi ndio yanapiga hodi. Wananchi wa Tokyo wakifurahia kwa ngoma majira hayo wakati wa wikiendi.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Mdau Reginald Ndesika wa NHK akiwa katika duka moja huko Akihabara leo asubuhi alifanya manunuzi.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Jiji la Akihabara ndipo nyumbani kwa vifaa vya electroniki nchini Japani. Hakuna kukosa kitu hapa hata spea ya miaka ya 50.

Poa

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Nami nipo...

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Anga la Tokyo saafii. Lakini mvua ikianza hapo balaa.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Waalimu hapa Japani wakirekodi kipindi cha Runinga cha mazoezi ya mwili. Ukiwa na dishi unaweza kuiona siku moja hiyo shughuli.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Goma la Samba katika maonyesho ya Ki-Brazili ilikuwepo lakini ilikuwa kwa ajili ya kusikiliza tu si kama ile ya kuunguka mitaani na kivazi fulani hivi. Ilipendeza.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Brazili walifanya maonyesho yao hapa Tokyo. Walijiandaa vilivyo . Moja ya mabango ya utambulisho.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Waalimu wa mazoezi yaliyofanyika Kinshi-cho nje ya Tokyo wakinipongeza kwa kutrai .

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Tulikutana na mzee wangu huyu mazoezini ana miaka 88 na amefanya mazoezi kwa miaka 60 mfululizo . Afya njema na anaendesha baiskeli masafa marefu tu bila tabu. Haya nyumbani nasi tujaribu angalau,

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Unaona , nami nilikwepo.

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Kuna utaratibu hapa Japani wa kufanya mazoezi kwa watu wa rika zote , hapa ilikuwa eneo la Kinsi-cho pembezoni kabisa ya Tokyo. wazee wakijiandaa kuanza mazoezi

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Hili Jengo lipo Tokyo , hapa ndipo ilipofanyika baadhi ya michezo ya Olyimpiki ya 1964. Sasa linatumika kama jumba la maonyesho ya wasanii na kazi nyingine za sanaa. Mhmm! kwa wenzetu kulipambazuka mapema!

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Maeneo jirani na Shirika la Utangazaji la Japani NHK. Mji mazingira!

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008

Siku za wikiendi hususan majira ya joto wasanii mbalimbali hapa Japani hujimwaga kwenye viunga mbalimbali kikiwemo hiki cha Yoyogi nesheno Park jijini Tokyo kuonyesha vipaji vyao kama mdada huyu aliyekuwa kivutio kikubwa kwa sauti yake hivi majuzi . Hata kama wewe ukiwa na zeze lako unaweza kutumbuiza na watu wakakufahamu...lakini hamna kiingilio!..buree

Posted by BM. on Friday, September 26, 2008
Wakati wa usiku eneo la Shibuya katikati ya Tokyo pilikapilika sana .Imetulia.

Posted by BM. on Wednesday, September 24, 2008

Wajapani wakiyaanga majira ya joto kwa nderemo.