Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, June 30, 2011

Posted by BM. on Wednesday, June 29, 2011

Enzi zileee za Mwalimu kulikuwa na noti iliyokuwa ikijulikaa kama 'mmasai'. Hii ni noti ya shillingi mia. Unaweza kupima rika lako kwa kujiweka katika makundi matatu kwa kujiuliza...1. 'Nimeshawahi kuisikia noti hii?'kama jibu ni hapana...wewe bado , 2. 'Je umeshaiona noti hii?'?... kama jibu ni ndio bass wewe wa umri wa kati... 3. 'Je nimeshawahi kuitumia noti hii wakati ule?'//Kama jibu ni ndio basss ...wewe mtu mzima sasa... au nakosea mkubwa!..

Posted by BM. on Wednesday, June 29, 2011

Kwangu mimi Michelle na Mumewe Barack nawaona kama waalimu kwenye majukwaa. Sizungumzii hasa kile wanachokiamini na kukisema kila uchao lakini nazungumzia mtindo wao wa kumiliki majukwaa na kujenga hoja. Bila shaka nina mengi ninayojifunza kutoka kwao , nawe pata muda msikilize ...nadhani utajifunza kitu...!

Posted by BM. on Monday, June 27, 2011

Msichana wa kifilipino aliyeanza kuimba akiwa na miaka minne , sasa na ana miaka 19. Anatajwa kuwa ni binti mwenye kipaji cha juu kupata kutokea katika uimbaji wa nyimbo za R&B huyu si mwingine ni Charie Pempengco. sikiliza clips naamini utakubaliana na ulimwengu mzima juu ya kipaji hiki. Nasi nyumbani tuibue vipaji...

Posted by BM. on Sunday, June 26, 2011

Mwanamitindo, mtangazaji wa michezo ya kubahatisha na binti anayejipenda sana Bi.Kayo Sato (a.k.a Kayo Police)amewaacha watu vinywa wazi pale aliposema kuwa ana siri kubwa sana moyoni mwake inayohusu jinsia yake. Kufuatia maneno ya chini chini ya muda mrefu, binti huyo ambaye sasa ana miaka 23 alikwenda kwenye kituo kimoja cha Televisheni na kusema kuwa kwa hakika yeye ni mwanaume na si mwanamke ...ila anapenda kuwa katika muonekano wa kike.Kayo ni maarufu sana hapa Japani kwa kusimamia maonyesho yanayojulikana kama 'The Nico video game show.
Bi. Kayo anasema kuwa aliondoka kwenye mji wa kwao kipindi kidogo, na sio rahisi kwa watu waliokuwa wakimjua awali kujua kuwa ni mwanaume na akaanza kuishi kama mwanamke kwa kutumia majina mengine.
Alijiunga na shirika la wanamitindo na kujizolea umaarufu mkubwa kama mdada modeli wa kutumainiwa na katika kwa kipindi chote cha miaka kadhaa hakuna mtu katika shirika lake aliyewahi kumgutukia.

Anasema wala hajafanyiwa upasuaji wa ngozi na kuwekewa vipande bandia, yeye ana uzuri wa asili na amepata mafanikio makubwa katika kazi yake kwa kutumia vipodozi tu. Bi. Kayo aliandika katika blogi moja hapa Japani kuwa , "Kwa yeyote aliyepokea ujumbe wangu, asante sana kwa maoni yenu, nimetiwa moyo sana na maoni yenu, na kaa nilivyosema kwenye maonyesho yale mie nilizaliwa mvulana,niliona litakuwa jambo jema kumwambia kila mtu juu ya yale yanayonihusu , yaliyopita. Nimefarijika kwa kunipa fursa hii na , nitafanya kazi kama Kayo Sato na kuendelea mbele, na nina furaha sana kuwa watu wengi wamenikubali na kukubali mwanzo wangu huu mpya".
Tangu wakati alipoweka wazi jinsia yake kwemye blogi amekuwa akipokea ujumbe wa kumtia moyo kutoka kwa watu wengi. Source; webs za kijapani..

Posted by BM. on Saturday, June 25, 2011

A former Rwandan minister has been jailed for life for genocide and incitement to rape at the United Nations-backed court for Rwanda in Tanzania.Pauline Nyiramasuhuko, who is the only woman to be convicted by the court, was minister for family and women's affairs in the Rwandan government when some 800,000 people, mainly ethnic Tutsis, were killed in 1994.
She was accused of direct and public incitement to commit genocide and of being responsible for rape "as part of a widespread and systematic attack against a civilian population on political, ethnic and racial grounds," the International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) said.
Her son, Arsene Shalom Ntahobali, a militia leader who was jointly charged in the case, was also convicted Friday of genocide, crimes against humanity including rape and persecution and war crimes, and sentenced to life in prison.Four local officials who were accused alongside Nyiramasuhuko and her son were all found guilty of genocide and other charges. They were handed prison terms ranging from 25 years to life.Nyiramasuhuko, who was arrested in 1997 in Kenya, and taken to the U.N. court in Tanzania to await trial, was found guilty of seven of the counts she faced, ICTR spokesman Roland Amoussouga told CNN. They included charges of genocide, conspiracy to commit genocide, war crimes and crimes against humanity including rape and persecution.Two charges were dismissed, one of complicity to commit genocide and a second relating to murder and crimes against humanity. She was also cleared of two charges, one alleging direct and public incitement to commit genocide and another of inhumane acts and crimes against humanity.The Rwandan genocide was triggered by the April 6, 1994, shooting down of a plane carrying the nation's Hutu president.Ethnic violence erupted and Tutsis were killed systematically by Hutus.
Jikumbushe...


Source: CNN

Posted by BM. on Thursday, June 23, 2011

Mwanamke mmoja raia wa Brazil anayeaminika kuwa na umri mkubwa kuliko binaadamu yoyote duniani amefariki akiwa na miaka 114. Maria Gomes Valentim alifariki dunia pale ogani zake muhimu, (viungo tete vilivyo muhimu ) Kuacha kufanya kazi kwa mpigo, ikiwa ni siku chache tu hajaingia mwaka wake wa 115.Record za Guinness duniani zinathibitisha kuwa bibi huyo alizaliwa mwaka 1896 na mwezi uliopita tu alitangazwa kuwa nashikilia rekodi hiyo ya kuwa mtu mwenye umri mkubwa duniani. Siku chache kabla ya kifo chake alionekana kufurahia mlo wa Ki-Brazil unaoitwa, feijoada, and n a mapochopocho yenye sosi za pilipili.Kwa mujibu wa rekodi ya Guinness, Bi. Valentim amefariki akiwa na umri wa miaka 114 years na siku 347 days na sehemu kubwa ya maishayake alikuwa katika mji wa Carangola, uliopo mashariki mwa Brazil. Awali ilikuwa ikijulikana kuwa mtu aliyekuwa na umri mkubwa alikuwa Besse Cooper wa Georgia, nchini Marekani lakini mwezi Uliopita ilibainika kuwa Valentim alikuwa mkubwa kwa siku 48 kuliko alivyo Cooper.Bibi huyo ameacha wajukuu wanne, watukuu saba na wajukuu wa wajukuu zake watano.

Posted by BM. on Thursday, June 23, 2011

Jana Jumanne 21/06 kulikuwa na hafla maalum katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa japani iliyowajumuisha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani inayofahamika kama 'International Students Party' kwa kisukuma " (留学生 パーティー)" Party hii hufanyika kila mwaka ambapo wanafunzi kutoka nchi zisizopungua 19 wanaosoma Chuoni hapo husherekea pamoja na wenyeji wao. Ambatana nami...
Katika sherehe hizo vyakula vyenye asili ya Nchi tofauti huandaliwa na pia wanafunzi hutoa burudani mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kubadilishana utamaduni. Kwa Mwaka huu, wanafunzi kutoka Tanzania waliandaa Ndizi Nyama zilizoungwa kwa tui zito la nazi viungo mbalimbali na mchuzi saafi wa maharage yaliyoungwa kwa nazi. Chakula hiki kiliwashangaza wengi. kwani kwa utamaduni wa Japan na nchi nyingi barani Asia hutumia ndizi kama tunda tu.
Maelezo yalitolewa na kila nchi kama alivyofanya mdau hapo Eustadius Francis kutoka Tanzania -Pichani...


Kwa upande wa burudani, vijana walishusha Sebene zito ambalo liliwafanya watu kutoka nchi mbalimbali kuja Kushambulia jukwaa. Hata hivyo mwisho wa party hiyo rasmi, ulikuwa ndio mwanzo wa ''after party'',
Chanzo cha habari hii hakikuwa tayari kudadavua yaliyojiri huko pengine baadaye ...
Take 5 mdau E.F

Posted by BM. on Wednesday, June 22, 2011

Mke wa Raisi wa marekani Michelle Obama yuko ziarani Afrika kusini akiwa ameambatana na wanawe wawili , , binamu yake na mama yake mzazi Marian Robinson. Mwanzoni mwa ziara hiyo alikutana na Mzee Madiba, Mandela na na mkewe Graca.

Posted by BM. on Wednesday, June 22, 2011

Baada ya hapo Bi. Michelle akiwa na wanawe walitembelea kituo cha kijamii cha Emthromjemi, katika kitongoji cha Zandspruit, Johannesburg.


Posted by BM. on Monday, June 20, 2011

Posted by BM. on Monday, June 20, 2011

Vikosi vya waasi vinavopambana na Majeshi yanayomtii Kanali Qadhafi huko Libya. Baada ya kazi ngumu ya saa nyingi...muda wa kupumzika umefika unaweza kuona mazingira ya kulala ya mwanajeshi aliye vitani...
Hapo chini vikosi vya Canada vikiendeleza mapambano katika mashamba ya mihadarati na majengo yaliyohamwa huko kusini mwa Afghanistan. Vita kitu kibaya sana. Kinachowindwa hapo ni roho za watu tu..

Posted by BM. on Monday, June 20, 2011

Mwanaume mmoja nchini Vietnam, anahangaika kuwatafuta wasamaria wema ili aweze kufanyiwa operesheni ya kuuondoa uvimbe kwenye mguu wake wenye uzito wa kilo 80 na urefu wa mita moja. Kijana Nguyen Duy Hai wa nchini Vietnam, hawezi kufanya kitu chochote zaidi ya kukaa chini au kujilaza kwani uvimbe kwenye mguu wake umekuwa mzito sana kiasi cha kufikia uzito wa kilo 80 hivyo kuunyanyua mguu wake ni sawa na kuzinyanyua kilo 80 toka chini.
Uvimbe kwenye mguu wa Nguyen ulianza alipokuwa na umri wa miaka 14, ambapo ulipozidi kuwa mkubwa ulipelekea kukatwa kwa mguu wake lakini umeendelea kukua kila miaka ilivyoenda na hivi sasa Nguyen akiwa na umri wa miaka 31 hawezi tena kufanya chochote zaidi ya kulala au kukaa.Umaskini wa familia yake ndio sababu ya Nguyen kushindwa kwenda hospitali kufanyiwa operesheni ya kuondolewa uvimbe huo.Kilio chake cha kuomba msaada toka kwa wasamaria wema duniani kimepelekea habari kuhusiana na uvimbe wake kusambaa haraka kwenye vyombo vya habari duniani.Nguyen anatumaini kuna mtu atajitokeza kulipia gharama za matibabu yake hivyo kumuondolea mzigo mama yake mwenye umri wa miaka 61 ambaye hivi sasa ndiye anayemuuguza wakati wote.
Pole sana Nguyen...

Posted by BM. on Monday, June 20, 2011

Jumuiya makanisa ya Anglikana, Uingereza inatarajiwa kutangaza rasmi kuwa wanaume waliojitangaza wazi kuwa wao ni mashoga wataruhusiwa kuwa mapadri iwapo watatimiza sharti la kujizuia kufanya ngono.
Jumuiya makanisa ya Anglikana, Uingereza inatarajiwa kutangaza rasmi kuwa wanaume waliojitangaza wazi kuwa wao ni mashoga wataruhusiwa kuwa mapadri iwapo watatimiza sharti la kujizuia kufanya ngono.Taarifa rasmi ya kuruhusu mashoga kuwa mapadri inatarajiwa kutolewa jumatatu ambapo imetangazwa kuwa ni katika kuondoa ubaguzi katika masuala ya dini bila ya kuwabagua watu kwa tabia au matendo yao kinyume na maumbile.Sharti la kuwataka mashoga wajizuie kufanya ngono iwapo wanatakiwa kupewa nafasi hiyo kubwa ya kidini huenda ikasababisha mtafaruku kwani mchungaji mmoja shoga anapinga sharti hilo na anatishia kujitoa yeye na wafuasi wake duniani toka kwenye kanisa hilo.
Mwaka 2003, mchungaji ambaye pia ni shoga na mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Dr Jeffrey John (Pichani) alitajwa jina lake miongoni mwa wagombea wa uaskofu wa mji wa Reading hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa kwenye kanisa la Anglikana na kupelekea aamue kulitoa jina lake.Kanisa la Anglikana halitaki mgogoro wowote utokee na kuwagawa waumini wa kanisa hilo duniani.Hata hivyo, baadhi wa waumini wa kanisa hilo la Anglikana wanapinga uamuzi wa kuruhusu mashoga kuwa mapadri kwani ni kinyume na mafundisho ya kanisa

Posted by BM. on Saturday, June 18, 2011

Raisi wa zamani wa Zambia , Fredrick Chiluba amefariki dunia leo Jumamosi june 18 jijini Lusaka akiwa na miaka 68..Kwa mujibu wa Msemaji wake Emmanual Mwamba , Hadi jana ijumaa Bw. Chiluba alikuwa mzima wa afya akifanya mikutano yake ya kisiasa lakini baadaye jioni aliwaita madaktari wake akilalamika kuwa hakuwa anajisikia vyema na usiku wake akaaga dunia. Unaweza kujikumbusha safari yake ya maisha kwa njia ya video...
Chiluba aliingoza nchi hiyo kwa vipindi viwili baada ya kumshinda kwa kura mwasisi wa taifa hilo Raizi wa zamani Kenneth Kaunda aliyekaa madarakani kwa miaka 27. Siku za katikati alipata misukosuko mikubwa ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kuelezwa kuwa ametumia sivyo ndivyo Dola laki tano za kimarekani mali ya Ikulu kinyume cha Sheria lakini hatimaye akaipangua kesi hiyo. Hata hivyo wake wake Regina Chiluba alikabiliwa na mashitaka na akashindwa mahakamani na kujikuta jela hata hivo alikataa rufaa na kuachiwa...
Habari: Magazeti ya Zambia..

Posted by BM. on Saturday, June 18, 2011

Jioni ya leo Mie na mbongo mwenzangu Mr. Eustadius Francis (Anasoma Chuo Kikuu cha kilimo cha Tokyo)tulikwenda katika mgahawa wa Tsuraya eneo la Setagaya, mkabala na Chuo kikuu hicho kupata kikombe cha kahawa. Jambo lililotufurahisha sana ni kukutana na bidhaa ya tanzania ikinadiwa!

Kahawa ya Tanzania...pamoja na tangazo maalum kuelezea ubora wa bidhaa hiyo.
Kwahakika ilibidi tuinunue na kula kile cha nyumbani...tulifarijika sana. Tulitamani kusema kwa sauti kuwa 'hii kahawa inatoka kwetu! '..pengine siku nyingine! Hongereni wote waliofanikisha jambo hili...

Posted by BM. on Saturday, June 18, 2011

Mwalimu wa Chuo cha Kilimo cha Mtwara Bw. Muhaji Abdallah Lenga (Pichani)yupo nchini Japani kuongeza ujuzi wa kilimo cha mpunga, kwasasa yupo eneo la Chiba. Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani ilibahatika kuongea naye. katika kipindi chote cha kuwa hapa Japani amekuwa akijibiidisha kwa nadharia na vitendo katika kujielimisha juu ya kilimo cha zao hilo. Moja ya mambo yaliyonifurahisha sana katika mazungumzo yetu ni matumizi ya bata wakula magugu katika mashamba ya mpunga hapa Japani. angalia Picha za mabata hao wakiwa kazini.

Mwl . Lenga amesema kuwa Bata hawa ni chotara , mchanganyiko wa bata maji na bata kama wale wa nyumbani kwahiyo wanauwezo wa kuishi majini wakiwekwa huumo tangu upandaji wa mpunga hadi kuvunwa na baadaye hutumika kama kitoweo. Bata hawa wanafundishika na hawawaogopi binaadamu. Lengo la kuwatumia mabata hawa ni kupalilia mashamba kwa kula magugu na kuongeza mbolea kwa kinyesi chao. Hii ni mbinu ya kitaaluma ya kukwepa kutumia madawa ya kuuwa wadudu au kemikali. Kemikali zina athari kubwa mashambani na kwa walaji. Kwa mujibu wa Mwl Muhaji, uzalishaji wa mpunga kwa kuwatumia mabata hawa ni wa gharama ya juu ,ikilinganishwa na ule wa matumizi ya madawa ya kuuwa wadudu ya viwandani. Wajapani wanazingatia sana kanuni za kilimo na ndi maana wanapata mavuno mengi katika ekari moja..

Posted by BM. on Friday, June 17, 2011

Mdada wa Kiganda , Amani Wairimu na singo yake mpya ..Without you!

Posted by BM. on Friday, June 17, 2011

The washing machine cycle takes about 45 minutes – and George Washington comes out much cleaner in the Zimbabwe-style laundering of dirty money.Low-denomination U.S bank notes change hands until they fall apart here in Africa, and the bills are routinely carried in underwear and shoes through crime-ridden slums. Some have become almost too smelly to handle, so Zimbabweans have taken to putting their $1 bills through the spin cycle and hanging them up to dry with clothes pins alongside sheets and items of clothing.It's the best solution – apart from rubber gloves or disinfectant wipes – in a continent where the U.S. dollar has long been the currency of choice and where the lifespan of a dollar far exceeds what the U.S. Federal Reserve intends.Zimbabwe's coalition government officially declared the U.S. dollar legal tender last year to eradicate world record inflation of billions of percent in the local Zimbabwe dollar as the economy collapsed.The U.S. Federal Reserve destroys about 7,000 tons of worn-out money every year. It says the average $1 bill circulates in the United States for about 20 months – nowhere near its African life span of many years.Larger denominations coming in through banks and formal import and export trade are less soiled.But among Africa's poor, the $1, $2, $5 and $10 bills are the most sought after. Dirty $1 bills can remain in circulation at rural markets, bus parks and beer halls almost indefinitely, or at least until they finally disintegrate.Still, banks and most businesses in Zimbabwe do not accept torn, Scotch-taped, scorched, defaced, exceptionally dirty or otherwise damaged U.S. notes.
-Huffpost World

Posted by BM. on Friday, June 17, 2011


Hatua moja huanzisha safari...

Posted by BM. on Tuesday, June 14, 2011

WATU wasiofahamika wamevamia shule ya kimataifa ya Livingstone ya wilayani Njombe mkoani Iringa na kumteka mwanafunzi mmoja wa kike katika shue hiyo na kumchinja kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.Imedaiwa kuwa watu hao ambao idadi yao haijafahamika walivamia shule hiyo majira ya saa 10 alfajiri ya kuamkia juzi na kuingia katika bweni la wasichana na kufanikiwa kumteka mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Doris Lutego (12) ambaye ni mkazi wa mtaa wa shule ya Uhuru mjini Makambako wilaya ya Njombe. Wakizungumza kwa njia ya simu mtandao wa; www.francisgodwin.blogspot.com (Chanzo cha habari hii) na mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa juu wa tukio hilo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitekwa usiku wa kuamkia jumapili na kuwa pamoja na jitihada za kumtafuta zilizofanywa na wananchi na viongozi wa shule hiyo jitihada zilishindikana .“Baada ya taarifa ya kuvamiwa kwa shule hiyo na kutekwa mwanafunzi huyo wananchi tuliendesha msako mkali wa kuwasaka wavamizi hao ila hatukufanikiwa hadi leo asubuhi baada ya wakazi wa eneo la kitongoji cha Kambarage Njombe kufanikiwa kukuta mfuko wa Salfeti ambao ulikuwa na mwili wa mtoto huyo ….mfuko huo ulikutwa nyuma ya nyumba ya balozi wa kitongoji hicho na baada ya kutafuta zaidi ndipo kichwa chake kilikutwa karibu na nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho huku kikiwa kimehifadhiwa katika mfuko wa madaftari ya mwanafunzi huyo”. Hata hivyo alisema kuwa mbali ya kufanikiwa kukuta mwili wa mwanafunzi huyo ila bado hawajafanikiwa kuwakamata wahusika wa mauwaji hayo ya kinyama .Alisema kuwa mauwaji hayo yamewaweka katika maswali zaidi wakazi wa mji wa Njombe na wilaya nzima kwani inaonyesha wazi wauwaji hao wamefanya hivyo kama sehemu ya kulipiza kisasi katika familia ya mtoto huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarit Mangalla (pichani) amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo .
Kamanda Mangalla alisema kuwa taarifa zilizofika polisi mapema jana zillikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo na kukutwa kwa baadhi ya meno yake na damu katika kitanda chake na kuwa bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi na kuwasaka wahusika wa tukio hilo.Nimeshikwa na uchungu...nimehuzunika sana.