Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, April 30, 2011

Jana Ijumaa, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa Japani walitutembelea katika Jengo la Utangazaji la Redio Japani NHK. Walipata fursa nzuri kujionea mazingira ya kazi zetu , tukafanya mahojiano na baadaye kumbukumbu ya picha!
Picha ya chini; Kutoka kushoto waliosimama-Hiroshi Ikeuchi (Mjapani anayeifahamu vyema Tanzania), Julia Mlwilo na Eustadius Francis. Waliokaa Mie na Cornel Kibona.

Posted by BM. on Saturday, April 30, 2011

Bila shaka hayo ndio yaliyo miyoni mwao. Kushoto (Specioza Mallya) Mtanzania aliyekuwa akifanya kazi katika Shirika la Utangazaji la Japani -NHK ambaye amemaliza muda wake wa kukaa Japani na anarejea nyumbani akiwa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili , Bi. Yuko Asano muda mfupi baada ya hafla ya kumuaga rasmi.

Posted by BM. on Friday, April 29, 2011

Amepita!...

Posted by BM. on Friday, April 29, 2011

Mbilia bel ,anakamilisha album yake mpya itayokwenda kwa jina la THE QUEEN Mama huyu mkongwe katika fani amewashirikisha nguli wengine waishio Ulaya kama Nedule Santa Crus Popolipo, Popoli Mansiamina Nyboma canta danos na wengine....


Albam hiyo itabeba nyimbo kali 12 na tayari kashuti video za nyimbo 4,mbili zikiwa nchini mwake na zingine ufaransa..........Pengine ujio huu unatarajiwa kumrejeshea tena mama huyu heshima aliyokuwa nayo zamani...take five Mbilie!

Posted by BM. on Friday, April 29, 2011

Posted by BM. on Friday, April 29, 2011

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, juzi, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).


Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Danstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

27 Aprili, 2011

Posted by BM. on Friday, April 29, 2011
Posted by BM. on Saturday, April 23, 2011Posted by BM. on Saturday, April 23, 2011

Kwa moyo mkunjufu , nawatakia wadau wa uwanja huu wa Mirindimo , pasaka ya furaha. na maadhimisho mema ya Pasaka . Mungu awabariki sana . Ameen!

Posted by BM. on Wednesday, April 20, 2011

Donation of Relief Goods from the Embassy of Tanzania in Japan and the Tanzania Community in Japan

In response to the Great East Japan Earthquake, representatives of the Embassy of Tanzania in Japan and the Tanzania Community in Japan will visit the Natori City Hall in Miyagi Prefecture to donate Tanzanian instant coffee (600 cans worth 255,000 yen) and canned foods (405 cans worth 100,000 yen) to disaster-stricken people at 2 P.M. on Saturday, April 9.

The Government of Japan deeply appreciates assistance from the Government of the United Republic of Tanzania and the Tanzania Community in Japan.

Source: www.tanzanitesociety.jp/news/show/50
N.B Katika hafla hiyo Ubalozi wa Tanzania uliwakilishwa na Afisa wake mwandamizi -Ubalozi wa Tanzania nchini Japani Bi. Jilly Maleko (Picha ya Juu, mstari wa juu watatu kutoka Kushoto), na Ujumbe wa Jumuia ya Watanzania Tanzanite -Japani uliongozwa na Kaimu Mwenyekiti wake Rashidi Njenga , (Watatu kuanzia Kulia mstari wa chini.) Picha inayofuata inamuonyesha Bw. Njenga na ya chini, Mstahiki meya wa jiji la Natori, Isso Sasaki aliyepokea msaada huo kwa niaba ya Japani.

Posted by BM. on Wednesday, April 20, 2011

Posted by BM. on Monday, April 18, 2011

Posted by BM. on Sunday, April 17, 2011

Pilika pilika za uchaguzi zinaendelea kote nchini Japani wakati huu kwa staili yake ambapo leo Jumapili chaguzi katika kanda maalum hapa zinazojulikana kama (dai-jūnana-ai tōitsu chihō senkyo)zinafanyika. Japani ni nchi ya vyama vingi vya siasa.

Uchaguzi mwingine ulifanyika jumapili iliyopita ambapo magavana 13 , mabaraza ya kimkoa na mameya watano pamoja na wajumbe kutoka mabaraza 16 walichaguliwa.La ziada ni kuwa kuna mabango maalum yenye nambari ambapo kila chama hulipia kisanduku chake nchi nzima kwa kila bango ambapo hubandika picha ya mgombea na madokezo muhimu. Kama hujisshughulishi huwezi kujua...kuko shwari tu. Pilika pilika hizi zitakamilika jumapili ijayo.
Pengine jipya ukilinganisha na nyumbani...kampeni za hapa ni za kisayansi. Mitandao ya wavuti imetumika sana, magari machache yamekuwa yakipita kuwakumbusha maeneo ya kupigia kura kwa wale wenye sifa hizo.

Wagombea wamekuwa wakijitokeza maeneo ya wazi kama vile vituo vya treni na kunadi sera zao lakini watu wachache tu husikiliza kwani taarifa wanazo kupitia wavuti. Picha za wagombea hubandikwa kwa utaratibu maalum, na hulipiwa kwa mammlaka zinazohusika.

Hata miye nimepokea vipeperushi wa wagombea , lakini sina haki ya kupiga kura naangalia tu basss!

Posted by BM. on Saturday, April 16, 2011

Posted by BM. on Saturday, April 16, 2011

Mwanamke wa kiislamu raia wa Ufaransa Bi. Kenza Drider, ambaye asili yake ni Kaskazini mwa Afrika akipita nje ya jengo kanisa jijini Paris akiwa amevaa vazi la Burqa lililopigwa marufuku nchini humo. Madai yake na wenzake ni kuwa vazi hilo lina lengo la kujisteri kwanini lipigwe marufuku? Waandishi wa habari na wanausalama walikuwepo katika eneo hilo.

Posted by BM. on Saturday, April 16, 2011

Serikali mpya ya Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara inaandikisha wanajeshi wapya kuboresha hali katika mji mkuu wa kibiashara Abidjan baada ya miezi minne ya ghasia za kisiasa. Habari zaidi zinasema maisha yameanza kurudi katika hali ya kawaida ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kukamatwa kwa rais wa zamani nchini humo, Laurent Gbagbo.Katika hatua za awali Raisi Ouattara alikutana na Mkuu wa majeshi Jenerali Phillipe Mangou katika hoteli ya Golf ya Abijan.


Hivi sasa baadhi ya wanamgambo wa Ouattara wanayo nafasi ya kujiunga na serikali mpya ya Ouattara kama wanajeshi na polisi.
Mwalimu wa mafunzo katika kundi jipya la Repuplican Forces nchini Ivory Coast, Yaya Cisse, anasema hawa ni raia ambao watapatiwa mafunzo kuwa wanajeshi kamili.
Wale ambao wanataka kuwa polisi wataendelea. Wale ambao wanataka kuacha, anasema tutawaruhusu kufanya hivyo.Kuweka sawa huduma za usalama nchini Ivory Coast ni sehemu kubwa ya kurudisha tena ushwari katika mji mkuu wa kibiashara ambapo Rais Ouattara anataka kuanza haraka uuzaji wa kakao nje ya nchi, kufungua tena mabenki na kukufua tena viwanda ili uchumi wa nchi usonge tena mbele.

Hata hivyo kamatakamata bado inaendelea nchini humo , ambapo wafuasi sugu wa Gbagbo waliopo jeshini wamekuwa wakitiwa kwenye mikono ya dola...

Posted by BM. on Saturday, April 16, 2011

Mambo si shwari Bahrain. katika Jiji la Manama maandamano yamefanyika kudai mabadiliko ya uongozi. Hatimaye Jeshi la usalama la nchi hiyo likatumia mabavu kuzima harakati hizo, watu kadhaa wamepoteza maisha. Uchungu huu uliwakumba pia madaktari ...baada ya kuwahudia wagonjwa walikumbatiana na kufarijiana. (Hapo ilikuwa baada ya kumuhudumia Bw. Abdul Ridha Mohamed ambaye alijeruhiwa vibaya)

Posted by BM. on Thursday, April 14, 2011

Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ametumia paundi 20,000 (Karibia Tsh. Milioni 50) kwaajili ya kuandaa harusi ya kifahari na gauni la harusi la kifahari kwaajili ya mbwa wake wa kike. Louise Harris mwenye umri wa miaka 32 alitumbua paundi 20,000 kwaajili ya harusi ya kifahari ya mbwa wake wa kike anayeitwa Lola ambaye aliozeshwa kwa mbwa anayeshikilia taji la mbwa mwenye sura mbaya kuliko wote Uingereza anayejulikana kwa jina la Mugly.

Sherehe hiyo ya kifahari ilihudhuriwa na watu 80 ambapo gharama za kuukodisha ukumbi kwaajili ya harusi hiyo ya aina yake ilikuwa paundi 2,500.Mbwa Lola alivalishwa gauni la harusi lenye thamani ya paundi 1,000 ambalo lilitengenezwa maalumu kwaajili yake na duka la vito vya thamani la Swarovski.
Mbwa Lola pia alivalishwa cheni shingoni na kikuku mguuni ambavyo vyote viligharimu paundi 750.Maua ya kupamba ukumbi wa harusi yaligharimu paundi 1,000 wakati wapambaji wa ukumbi walilipwa kitita cha paundi 3,000.

Miongoni mwa gharama za harusi hiyo ni mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama kwenye harusi hiyo ambao walilipwa paundi 400, madansa na wacheza shoo waliolipwa paundi 500, gari la kukodisha aina ya Bentley kwaajili ya maharusi liligharimu paundi 500 wakati Dj alilipwa paundi 500."Mbwa wangu ni fahari yangu na furaha yangu ni kuwafanyia kila kilicho kizuri", alisema bi Harris.Bi Harris alisema kuwa furaha yake imetimia kwa kuona Lola amefanikiwa kupata mwenza wake wa maisha ambaye amekuwa akicheza naye wakati wote.
Unaweza kujisomea kwa kisukuma hapa na mitandao mingine; http://www.telegraph.co.uk/news/newstopics/howaboutthat/8433985/Owner-spends-20000-on-wedding-for-dog.html

Posted by BM. on Thursday, April 14, 2011

Kuna mdau kaniletea hii picha na maelezo kuwa...Mti huu ukibahatika kuuona , chimba kamzizi kake chemsha , kunywa nusu kijiko cha chai....magonjwa yote sugu yanaondoka ndani ya saa moja....lakini utakayokutana nayo usimwambie mtu duh...

Shukran mdau...

Posted by BM. on Thursday, April 14, 2011

Madaktari nchini JAPANI wameondoa viungo kutoka kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 15 ambaye ubongo wake ulikufa kwa ajili ya upandikizaji.Mtoto huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali moja katikati ya jiji la TOKYO hadi juzi Jumanne alipofariki na viungo vyake kuonekana kufaa kwa upandikizaji.
Wazazi wa mvulana huyo walisema katika tamko lao kuwa hawakuwahi kuzungumza kuhusu uchangiaji wa viungo na mtoto wao lakini wanafikiri kuwa kuwasaidia watu kuishi kwa kutumia viungo vya kupandikiza kunaweza kukidhi matarajio yake. Jana Jumatano kazi ya kuondoa viungo ilifanyika ambapo moyo, mapafu , maini , figo na kongosho viliondolewa hadi kufikia asubuhi ya jana.

Hii leo Alhamisi kazi nzima ilikuwa imekamilika. Moyo uliotolewa kwa kijana huyo umepandikizwa kwa mvulana mmoja wa umri wake aliyekuwa na matatizo ya moyo katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Osaka huko Suita , mkoa wa Osaka , mapafu yametumika kumpandikiza mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la Shinindizo la damu katika mapafu ‘pulmonary hypertension’ katika operesheni iliyofanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tohoku huko Sendai na maini yalipandikizwa kwa mwanaume mmoja mwenye miaka 20 aliyekuwa na ugonjwa wa umetaboli wa ini ‘metabolic hepatic , operesheni iliyofanywa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Hokkaido.

Moja ya figo yake na kongosho zilipandikizwa kwa mwanamke mmoja mwenye miaka 30 aliyekuwa na tatizo la sukari katika figo zake katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Fujita huko Toyoake karibu na Jiji la Nagoya mkoani Aiichi wakati figo ya pili imepandikizwa ma mwanamme mmoja mwenye miaka 60 aliyekuwa akiugua tatizo sugu la figo na operesheni hiyo imefanyika katika hosptali ya Chuo Kikuu cha tiba za wanawake jijini Tokyo.
Hivi vitakuwa viungo vya kwanza kwa ajili ya kupandikizwa kutoka kwa mchangiaji mtoto nchini JAPANI tangu sheria iliporekebishwa mwezi Julai mwaka jana inayoruhusu uchangiaji wa viungo kutoka kwa watoto wa umri wa kati kwa ridhaa ya familia zao.
Japanese Media..

Posted by BM. on Tuesday, April 12, 2011

Aliyekuwa rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo ambaye alijiapisha mwenyewe kuwa rais baada ya kushindwa kwenye uchaguzi amekamatwa na wanajeshi wa mpinzani wake Allassane Ouattarra.
Inadaiwa na vyombo vya habari vya magharibi kuwa alilia akiomba asiuwawe baada ya kuingia kwenye mikono ya mpinzani wake.Kilikuwa kipindi kigumu kwake pale alipojikuta akivamiwa handakini akiwa yeye na mke wake na mwanawe wa kiume .


"Msiniue tafadhali", hilo ndilo lilikuwa neno la kwanza la rais Gbagbo baada ya kutiwa mikononi mwa majeshi ya mpinzani wake.Gbagbo alivalishwa jaketi lisilopitisha risasi ili kumlinda kutokana na wanajeshi wenye hasira ambao walitaka auliwe wakati huo huo bila ya kumchelewesha.Alipakizwa kwenye gari na kupelekwa kwenye makao makuu ya kambi ya Ouattara iliyopo kwenye hoteli ya Golf Hotel.


Ouattara akiongea kwenye televisheni ya taifa aliwataka wananchi wa Ivory Coast washikamane baada ya kutiwa mbaroni kwa mpinzani wake mkuu, Laurent Gbagbo.Ouattara alitamba kuwa nchi yake inaingia kwenye ngwe mpya ambapo aliahidi ataunda tume kuchunguza mauaji yaliyofanyika wakati wa vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Inaelezwa kuwa mwanajeshi mmoja alimpiga kibao Gbagbo wakati wa kumkamata alipotoa majibu kana kwamba ni kiongozi wa nchi, jambo ambalo lilimuudhi mwanajeshi huyo ambaye alishajitoa muhanga hadi kumfikia hapo alipo.

Posted by BM. on Monday, April 11, 2011

Viwanja vilivyopo katika bustani ya Yoyogi karibu na jengo la utangazaji la Shirika la Utangazaji la Japani-NHK World leo vilipokea maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia maonyesho ya bidhaa, burudani na vyakula kutoka mataifa mbalimbali. Banda la Mjasiriamali kutoka Tanzania Bi. Maryam nalo lilitikisa .wajapani na watu kutoka mataifa mengine walipiga foleni kuonja 'menyu' ya Kitanzania. Upande wa Afrika kulikuwa na banda jingine la Cameroon huku wengine barani Asia wakiwa kwa wingi sana. Pitisha macho...


Posted by BM. on Monday, April 11, 2011

Burudani ilikuwepo...lie 'band' na mdundiko wa Kijapani...mboni ilipendiza!

Posted by BM. on Monday, April 11, 2011

Mabanda ya vyakula yalikuwa na wageni wengi ...tulijumuika. Afrika iliwakilishwa na mabda mawili moja la Mtanzania , picha za chini hapo na Wakameroon ...sote tulijumuika kwenye banda 'letu' hapo tukakutana na wadau.