Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, April 14, 2011

Madaktari nchini JAPANI wameondoa viungo kutoka kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 15 ambaye ubongo wake ulikufa kwa ajili ya upandikizaji.Mtoto huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali moja katikati ya jiji la TOKYO hadi juzi Jumanne alipofariki na viungo vyake kuonekana kufaa kwa upandikizaji.
Wazazi wa mvulana huyo walisema katika tamko lao kuwa hawakuwahi kuzungumza kuhusu uchangiaji wa viungo na mtoto wao lakini wanafikiri kuwa kuwasaidia watu kuishi kwa kutumia viungo vya kupandikiza kunaweza kukidhi matarajio yake. Jana Jumatano kazi ya kuondoa viungo ilifanyika ambapo moyo, mapafu , maini , figo na kongosho viliondolewa hadi kufikia asubuhi ya jana.

Hii leo Alhamisi kazi nzima ilikuwa imekamilika. Moyo uliotolewa kwa kijana huyo umepandikizwa kwa mvulana mmoja wa umri wake aliyekuwa na matatizo ya moyo katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Osaka huko Suita , mkoa wa Osaka , mapafu yametumika kumpandikiza mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la Shinindizo la damu katika mapafu ‘pulmonary hypertension’ katika operesheni iliyofanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tohoku huko Sendai na maini yalipandikizwa kwa mwanaume mmoja mwenye miaka 20 aliyekuwa na ugonjwa wa umetaboli wa ini ‘metabolic hepatic , operesheni iliyofanywa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Hokkaido.

Moja ya figo yake na kongosho zilipandikizwa kwa mwanamke mmoja mwenye miaka 30 aliyekuwa na tatizo la sukari katika figo zake katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Fujita huko Toyoake karibu na Jiji la Nagoya mkoani Aiichi wakati figo ya pili imepandikizwa ma mwanamme mmoja mwenye miaka 60 aliyekuwa akiugua tatizo sugu la figo na operesheni hiyo imefanyika katika hosptali ya Chuo Kikuu cha tiba za wanawake jijini Tokyo.
Hivi vitakuwa viungo vya kwanza kwa ajili ya kupandikizwa kutoka kwa mchangiaji mtoto nchini JAPANI tangu sheria iliporekebishwa mwezi Julai mwaka jana inayoruhusu uchangiaji wa viungo kutoka kwa watoto wa umri wa kati kwa ridhaa ya familia zao.
Japanese Media..

0 comments: