Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, October 31, 2010

Mwanamuziki huyu Malkia Nvannungi ni moto wa kuotea mbali kule nchini Uganda unaweza kusikiliza nyimbo zake hizo mbili....ya kwanza Doctor na ya pili hapo chini ameimba na Q-Chillar kutoka Tanzania ... kama wewe ni mpenzi wa rumba la taratibu naamini utasuuzike......take 5, Nvannungi nakukubali...

Nakupenda...

Posted by BM. on Sunday, October 31, 2010

Kocha maarufu kwa jina la Super Coach Sylversaid Mziray 'Mwanangu' amefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya AgaKhan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwasiku kadhaa zilizopita.
atakumbukwa na wapenzi wa soka kwa mchango wake mkubwa wa mawazo na wa kivitendo . Amewahi kuzifundisha timu za simba na Yanga pamoja na Taifa Stras kwa nyakati tofauti. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Aiweke roho ya Mziray peponi , Amin...

Marehemu Syllersaid Mziray, enzi za uhai wake.

Taarifa ya MAKAMU Mkuu WA Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly S.A. Mbwette, kwa niaba ya Menejimenti yote ya Chuo,imetoa tamko juu ya msiba huo wa mkufunzi wake wa michezo, Syllersaid Mziray.

"Mziray alifariki dunia alfajiri ya kuamkia leo Jumamosi katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa karibu wiki mbili kutokana na Malaria na baadaye matatizo ya figo.Taratibu za Mazishi zinaendelea nyumbani kwake Tabata Magengeni. Mziray atazikwa Jumatatu kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Mazishi hayo yatatanguliwa na utoaji wa heshima hapa chuoni.Mungu ailaze roho ya marehemu Syllersaid Mziray Pema Peponi Amen!", taarifa hiyo ilimaliziwa na kusainiwa na KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO kwa niaba ya Chuo hicho

Posted by BM. on Sunday, October 31, 2010


Unaweza kuiangalia hiyo pia na ukagundua usanii hapo?

Posted by BM. on Sunday, October 31, 2010


Hapo hakuna usalama..!Kijana wa Kisomali aliyejeruhiwa kwenye mapambano...Al sabab...shughulini..

Posted by BM. on Tuesday, October 26, 2010

Hebu angalia kwa makini hayo matunda na anza kutaja majina yake , ukiweza kutaja yote kwa usahihi niandikie kwenye comment....ukiuliza utakuwa umeibia mtihani.

Posted by BM. on Monday, October 25, 2010

Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Evance Mhando yupo nchini China hivi sasa aking'arisha CV yake katika fani..Darasa linaanza kwa lugha ya kichina...du shughuli.(Pichani) Yupo na wanafunzi wenzake


Kaza buti mkubwa...one day!

ya kumbukumbu....frashiii pwaa!

Posted by BM. on Monday, October 25, 2010

Mdau Evance Mhando akipata msosi wa kichina sehemu....take 5 bro..

Msosi wa Kichina.....

Posted by BM. on Sunday, October 24, 2010


Sema!

Posted by BM. on Sunday, October 24, 2010

Kimbunga ache (Megi)kikitishia kung'oa uhai wa watu na viumbe vingine wacha uharibifu....Hii ni kaskazini yua Ufilipino...Usiombe kushuhudia, kusikia tu inatosha..

Posted by BM. on Sunday, October 24, 2010

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Ufaransa wakimchukua juu juu kijana mmoja ambaye alikuwa mmoja wa waandamanaji huko Lyon kupinga mipango ya serikali ya nchi hiyo kuongeza umri wa kustaafu na kusogeza mbele muda wa kuchukua mafao ya wazee. Hii inakuaje!

Posted by BM. on Friday, October 22, 2010

Mtangazaji wa Redio Japani Bi. Anna Kwambaza hivi karibuni alipata fursa ya kutembelea eneo la kihistoria la Hiroshima ambako bomu la atomiki lilidondoshwa na majeshi ya Marekani mwaka 1945 , mwishoni mwa vita vya pili ya dunia.
Hii ni sehemu pekee duniani ambako silaha ya maangamizi ya atomiki imetumika...unaweza kufuatilia historia hiyo kwa muda wako hapo chini.
Mdau hapo akiwa mbele ya Kuba la bomu la atomiki Hiroshima. Lilidondoshwa hapo na kuacha mabaki hayoSafari ya kileleni kwa kutumia rope car huu ni mlima Misen ili kuuona mji wote wa Hiroshima kutoka Juu

Watangazaji wa Redio Japani; Anna kwambaza na Chiho Yamada wakiwa Hiroshima , Japani....Baada ya kazi...msosi...chakula kinaitwa okonomiaki inataka uvumilivu ulozoea pilau na samaki wa tui bubu

Posted by BM. on Wednesday, October 20, 2010

Vimbwanga vya mzee Yusuf...."Nataka paja mie sitaki kipapatio...

Watu bwana Uuuh!

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


Mtangazaji wa Idhaa ya Kiajemi anayetokea Tehran Bw. Afshin , Iran amemaliza mkataba wake wa kuifanyia kazi Shirika la Utangazaji la Japani NHK na sasa anarejea kwao...Picha ya kumbukumbu .Take 5 bro!

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


Mke wa Raisi w Iran Mahmoud Ahmadinejad, Azam Farahi (wa pili kutoka kulia), Mke wa raisi wa Lebanon Bi. Wafa Sleiman (watatu kutoka kulia ) na mke wa Spika wa Bunge la Lebanon Nabhi Berri, Bi. Randa (Kulia), katika Chakula cha Usiku kilichoandaliwa huko Beirut , Lebanon ambako Raisi Ahmed Nejad anafanya ziara!

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


Binti wa Ki-Australia Sally Pearson akishangilia kwa kulia ushindi wake wa mbio za mita mia moja na kujinyakulia medali ya dhahabu katika michezo ya Commonwealth iliyomalizika hivi karibuni huko India.

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


Raisi Sebastian Pinera wa Chile katika picha ya pamoja an wachimbaji 33 waliokolewa kwenye migodi baada ya kufukiwa na udongo , hapo wapo katika hosiptali moja ya Copiapo nchini humo

Mchimba madini aliyeokolewa nchini Chile Osman Araya akimfariji mkewe baada ya kuvutwa kutoka ardhini . yeye alikuwa mtu wa sita kati ya 33 kuokolewa baada ya kukaa chini ya ardhi kwa siku 69. Hebu fikria nyoyo zao zilikuwa zikiwaza nini hapo!

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010

Muda mfupi uliopita tumetoka kwenye tamasha la kijadi la kila mwaka la wajapani huko Saitama eneo la Kawagoe-shi ambapo tulialikwa Nyumbani mwa mhadhiri wa lugha ya Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Soka hapa Japani na ndugu yangu Edward Kadilo Mtangazaji mwenzangu wa NHK hapa Tokyo pamoja na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili.
Safari ilianza kwa uopigaji wa picha...

Tulipigwa picha kwanza ...Ni Haluka nakamura na Melisa..


Kadilo, Ruci,Mie,Haruki...

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010

Tamasha lilihanikizwa kwa ngoma , Ndipo nilipojua kumbe wajapani wanapenda ngoma kuliko kwetu matombo!
blogspot.com/_MXa6ko8VRQM/TLnGAtPqmqI/AAAAAAAAFQs/wHZ5IYk3eyk/s1600/DSC00691.JPG">Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


Mwendo huu umetufikisha hapa...

Mlo

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010

Baada ya kushuhudia tamasha la ngoma za kijadi za kijapani...tukaalikwa nyumbani kwa Bi. Midori Uno na dada yake Lumiko Uno kwa ajili ya chakula cha mchana...Haruki , na Melisa...

Chiazzz, Ruci,Kadilo na Haruki...

Kabla ya kufunga menyu kwa kahawa tulikula hili tunda...Watambuzi tambueni laitwaje hilo tunda?

Posted by BM. on Sunday, October 17, 2010


giza limetanda ...lakini shughuli inaendelea...

Tuangalie kama imo...!

Posted by BM. on Saturday, October 16, 2010

Tulikwenda kutembelea mnada wa magari katika mkoa wa Gumna , eneo la Ooyama kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya MAEJI ya uuzaji wa magari yenye makao yake hapa Japani ambayo Mkurugenzi wake mkuu ni Mkenya Jeff Musyoka. Fuatilia picha hizi na baadaye ukitaka kuijua kampuni hiyo bofya; www.maeji-kaiho.com


Tumeshuka Mushashi-Urawa kuanza safari ya kwenda Mkoani Gumna kwenye huo mnada wa magari, kipande cha safari , takriban saa moja na nusu kwa gari inayotimua mwendo.

Magari ya watu wanaokuja mnadani hupaki hapa...


Tuanzie hapa kwenye pikipiki...


Mwenyeji wetu Jeff Musyoka akituongoza tuangalia vifaa ...

Imetulia au!


Posted by BM. on Saturday, October 16, 2010

Huwa kuna vyumba maalum ambavyo wanunuaji wa magari wanaotambuliwa na Makampuni ya uuzaji magari huingia ambako kuna komputa maalum zenye taarifa zote juu ya kila kitu kilicho kwenye mnada ...wao wanauwezo wa kujua bei na kufuatilia...Ugeni tena nilishindwa kupiga picha ndani nikatoka nje...


Baadhi ya wanachama wa minada hii na waalikwa hukaa jengo la nje kufuatilia aina za magari na bei na hutoa taarifa kwa njia ya mtandao kuwa wako tayari kuchukua kifaa hicho...Mabango hayo ndio huttoa picha na bei..