Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 31, 2010

Kuna siku maalum wajapani wanakusanyika mahali kama hapa na kuuza vitu vyao mbalimbali kwa bei ya chini vipya na vilivyotumika...Siku kama hiyo hutumika kukutanisha watu na kuonyeshana vitu vya mitindo mbalimbali..leo ilikuwa katika bustani ya Yoyogi Koen hapa Tokyo . Shughuli za wikiendi...za wajapani Mnada wa vitu binafsi
Mpate-mpate, ukitulia hukosi kivalo hapo! sagula-sagula ya Kijapani...
Pozi la leo...Kijua kimetoka lakini kibaridi kipo...!

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010

Maneno ya mwalimu...

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010


Impossible Things To Say when Drunk
THINGS THAT ARE DIFFICULT TO SAY WHEN DRUNK:
1. Innovative
2. Preliminary
3. Proliferation
4. Cinnamon
THINGS THAT ARE VERY DIFFICULT TO SAY WHEN DRUNK:
1. Specificity
2. Anti-constitutionalistically
3. Passive-aggressive disorder
4. Transubstantiate
THINGS THAT ARE DOWNRIGHT IMPOSSIBLE TO SAY WHEN DRUNK:1. No thanks, I'm married.
2. Nope, no more booze for me!
3. Sorry, but you're not really my type.
4. Taco Bell? No thanks, I'm not hungry.
5. Good evening, officer. Isn't it lovely out tonight?
6. Oh, I couldn't! No one wants to hear me sing karaoke.
7. I'm not interested in fighting you.
8. Thank you, but I won't make any attempt to dance, I have no coordination. I'd hate to look like a fool!
9. Where is the nearest bathroom? I refuse to pee in this parking lot or on the side of the road.
10. I must be going home now, as I have to work in the morning.
Try If You Dare...!
haa haaa ...kweli ...si kwelii? Take 5 Rwey...

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010

Nchini DRC kuna jamaa alikuwa ktika bendi mbalimbali za zamani na sasa ameanzisha kasi ya kuzipiga nyimbo za wakati huo./// Kwa wapenzi wa rhumba la taratibu , wale wa Sendema ya moto...enzi ya Dekule Kahanga Maquiz wanaweza kupata hisia ya kile ninachoongea. Sikiliza mpini wa kiutu uzima. Bila shaka wa miaka ya 80s /90s kiwingu. Hya wanaweza kubofya hapo ukajizungusha kidogo!

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010


Furaha ya ushindi....
Misri wameitandika Algeria mabao 4-0 na kufuzu kuingia fainali ya kombe la mataifa barani Afrika. Misri watakutana na Ghana ambao, hapo awali, waliitimua Nigeria kwa bao 1-0.Fainali itachezwa Jumapili mjini Angola. Algeria walianguka kwa kishindo kikubwa baada ya wachezaji wake watatu ikiwa ni pamoja na kipa wao Faouzi Chaouchi kuonyeshwa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu. Wapenzi wa timu ya Algeri walipowasili kwa mbwembwe katika uwanja wa ndege wa Bangwela huko Angola lakini hatimaye walipoa na kuondoka nchini humo kimya kimya.

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010


Moja ya uwanja utakaotumika kwa mikimiki ya kombe la dunia huko Capetown nchini Afrika Kusini siku ya ufunguzi wake. Siku hiyokulikuwa na mechi kati ya Santos na Ajax

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010

Raisi Jakaya Kikwete akizungumza na Raisi mstaafu wa Marekani Bill Clinton pembeni mwa Mkutano wa Baraza la uchumi wa dunia huko Davos , Uswisi juzi...

Posted by BM. on Friday, January 29, 2010


Raisi Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili Tripoli nchini Libya hivi karibuni, kuanza ziara rasmi. Viongozi wa nchi hiyo wakiwa pamoja na wale wazee wa nchi hiyo walivalia mavazi ya kijadi wakati wa mapokezi...

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010

mmoja wa manusura wa tetemeko la Haiti Msichana Holleline Lozama mwenye miaka 26 akitabasamu mara baada kutolewa kwenye kifusi ..Pole sana!
Habari za Karibuni kutoka Port au Prince mji Mkuu wa Haiti zinabainisha kuwa Kijana mmoja wa kiume amenusurika baada ya kutolewa kwenye kifusi cha tetemeko la ardhi , akiwa amekaa chini ya kifusi siku 11 .Waokoaji toka mataifa mbali mbali walikuwa ndio wanajitayarisha kuondoka nchini Haiti kurudi kwenye nchi zao baada ya zoezi la uokoaji kusitishwa baada ya matumaini ya kumuokoa mtu kutoka kwenye vifusi kuonekana ni finyu.Lakini kama Kama miujiza mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Wismond Exantus mwenye umri wa miaka 26 aligunduliwa na mama yake kuwa bado yupo hai chini ya kifusi cha hoteli aliyokuwa akifanya kazi ambayo iliporomoka chini yote.Kaka yake alitumia spika kuita jina la mdogo wake na jamaa alisikika kutoka chini ya ifusi akiita.Kazi ya kuwatafuta waokoaji ambao wengi wao walishafunga virago ilianza mara moja. Watumiaji wa tovuti ya twitter walianza kutumiana meseji wakiwatafuta waokoaji. Hatimaye waokoaji toka mataifa mbali mbali ambao walikuwa bado nchini Haiti walijitokeza na kuanza zoezi la kumuokoa Wismond. Iliwachukua saa chache waokoaji wa Ugiriki na Ufaransa kuweza kumtoa Wismond toka kwenye kifusi akiwa hai ingawa taabani kwa njaa.
Wismond amekonda ghafla kwa siku 11 alizokaa chini ya kifusi kiasi cha kuhitaji kamba kuishikilia suruali yake isianguke.Akizungumza muda mfupi baadaye , Wismond anasema kuwa tangia siku ambayo tetemeko la ardhi lilitokea, alikuwa hauoni mchana wakati wote akiwa kwenye giza kama usiku.Anasema kuwa siku za mwanzo za tetemeko la ardhi alikuwa akinywa soda zilizokuwa chini ya meza ambayo alikimbilia kujificha wakati tetemeko la ardhi lilipotokea. Lakini baada ya soda hizo kuisha alianza kuunywa mkojo wake mwenyewe kila alipokojoa. Wismond ni miongoni mwa watu wachache sana wenye bahati ambao wamefanikiwa kunusurika maisha yao kwenye tetemeko hilo la ardhi. Hadi sasa inakadiriwa jumla ya watu 120,000 wamefariki kutokana na tetemeko hilo kubwa la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa 7.0. Hebu angalia video hiyo tukio la kumuokoa Wismond.

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010

Hokkaido kaskazini kabisa mwa Japani ilivyo hivi sasa.
Mwanamke mmoja mtu mzima alikutwa amekufa katika eneo la wazi katika jiji la Sapporo nchini Japani akiwa amefunikwa na theluji na polisi wanasema kuwa alionekana akiwa na majeraha katika mwili wake.Watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo waliuona mwili wa mwanake huyo mwenye miaka 72 katika eneo la Kita saa nane mchana na kuita Polisi. Mwili huo ulikuwa umefunikwa kwa theluji kwa maki ya sentimenta 10 .
Mwanamke huyo anaaminika kuwa ni mwenyeji wa maeneo hayo na kwamba alipotea siku nne zilizopita na familia yake pamoja na polisi walikuwa wakifanya jitihada za kumtafuta.
Kamera za ulizi katika eneo hilo zinamuonyesha mama anayefanana na huyo akiingia katika duka la jirani alfajiti ya saa 11 na nusu siku hiyo aliyopotea na upelelezi unaendelea. Bila shaka kuwepo kwa kamera katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Japani inarahisisha sana masuala ya upelelezi. Agharab kila unapopita sura yako hubaki kwenye kamera na polisi huzitumia kuunganisha mwenendo wako wa siku.

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010


Mwanamke mmoja mwenye miaka 36 ameshikiliwa na Polisi chi ya sheria ya kuwalinda watoto na ponografia , baada ya kukamatwa siku tatu zilizopita akituhumiwa kuuza picha za binti yake ambaye wakati huu ana miaka 14 mkanda wa picha chafu za video kwa mwanamume mmoja mwenye miaka 46 mkazi wa jiji la Tokyo.
Mwanamke huyo ambaye anafanya kazi katika klabu moja ya starehe katika jiji la Tome anatuhumiwa kuuza mkanda huo –DVD mwezi Juni 2008 na tangu wakati huo Polisi wamekuwa wakikusanya taarifa za kutosha na sasa wamefikia uamuzi wa kumtia mbaroni.
Polisi inasema kuwa mwanamke huyo alikusanya picha hizo kwa kutumia kamera ya dijitali ya nyumbani kwake na baadaye kuzihamishi katika mkanda wa DVD.
Hatua ya kukamatwa imekuja baada ya mkazi mmoja wa kitongoji cha Kita hapa Tokyo kwa kushitakiwa kwa shauri lingine na polisi wakabaini DVD na vifaa vingine vinavyohusiana na picha za ponografia. Polisi wanadai kuwa mwanaume huyo na mwanamke anayeshikiliwa walikutana katika mtandao wa intaneti ambao unauza nguo za ndani. Mtaa huo pichani ndio anaokaa ..!

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010


Mkurugenzi wa kampuni ya Magari ya Wilna international Bw. Willy Ngoya mchana huu J2 amefanya mahojiano mafupi na Shirika la Utangazaji la Japani NHK juu ya uzingatiaji wa sheria za barabarani nchini Japani ukilinganisha na Afrika mashariki. Unaweza kusikia sauti yake tembelea mtanadao huo hapo chini;
http://www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili/top/index.html

Posted by BM. on Friday, January 22, 2010

Barani Yuropa hivi sasa kuna kibaridi kikali ile mbaya. Eeeh kibaridi hiki lawama mkubwa au nadanganya! Kibaridi kimekolea..
Pale taa za barabarani zinapozongwa na kibarafu... Maji yanapozidi unga...inabidi uvae nyenzo
Hapa Tokyo kibaridi nacho kinavuta kasi leo kimefikia digrii 7 . Kumetulia lakini kinapuliza. Hapo ni bustanini karibu na jengo la Matangazo NHK . Wajapani wanatunza mazingira , ukiwa ndani ya bustani hiyo utadhani uko Ngorongoro. Wanyama tu wakali hawapo ni vijindege na vijisungura!

Posted by BM. on Wednesday, January 20, 2010

Aisee tuma salamu bass!
Napenda kutuma salamu za mwaka mpya na krismas ya mwaka jana kwa wafuatao; Karuwa,Kimario,Kimambo,Mlimira,Mboya,Kissamo,Tarawia,Mghase,Mariki,Ndetirimisho,
Masoyi,Lelo,Nkya,Kiwia,Mawalla,Masawe,Mangi,Mushi,Kilasara,Kavishe,Mamuya,Mosha,Muro,
Mariale,Manka,Keku,Shirima,Lyimo,Ngowi,Lyatuu,Temba,Munuo,Mtei,Mmari,Kirumbuyo,Mkonyi,Tarimo,Munisi,Lema,Lauwo,Kessy,Mtuy,Kisomo,Moshy na Mkonyi.Eliringia,Otaru,Orotha,Lekule,Matemu,Ndetegetso,Mashingo,Mashingia,Shose,Ndakidemi,Sillayo ,Malewao,Mlay,Lauwo,Tairo,Mrosso,Shoo,Maeda,Swai,Mauki,Shayo,Kimaro,Soka,Mkenda,Makundi, Mangesho,Tilya,Kinabo,Mtei,Ulomi,Njau,Sirili,Materu,Minja,Kiwali,Maro,Ndossy,Kway,Meela,Mallya,Ndanshau,Shio,Asenga,Olomi,Macha na wale jirani zenu watani wenu wa enzi na enzi Wapare wanaosifika kwa ubahili. Yesu na Maria thijui nimemsahau Mrema!!Jamani kama thijamsahau thalamu zake thimfikie kapisa lanye. UJUMBE:Tudumishe mila setu na safari hii ndugu sangu hakuna kisingsio eti,vijana wa Majembe wanafanya kasi sio mcheso ,nauli sitakuwa bure kabisa hapo mpo jamani?? Aika Molyi,
aika mao,aika mae,aika ngoso,aika ndao aika mbee kanyi!!!!!
lete yako nawe....

Posted by BM. on Wednesday, January 20, 2010


A mother and a father were arguing on who is the most coward between them. After a long argument they decided to ask their two kids, who they think was the most coward between them. The first one says: Dad is the most coward, he scared of women. Whenever he sees a beautiful lady in town he closes his one eye. The second kid goes; that is peanut. Mom is so scared to sleep alone. When Dad work nightshifts, mom sleeps with the man next door, sometimes invites the gardener to sleep with her. Eeeh! Watoto weshaharibu…hebu kisia ilikuaje !

Posted by BM. on Monday, January 18, 2010

Mvua kubwa zilizonyesha Kilosa Kusini Mkoani Morogoro zimewaletea fadhaa watu wa maeneo hayo. Nyumba, vyakula, mifugo vyote vimekwenda..hali bado tete.
Bado hali ya sintofahamu huko Kilosa...Mvua imeondoa kila kitu...shughuli zimesimama.
Daraja katika njia ya Reli linalounganisha Morogoro na Dodoma limeondoka , miundombinu imevurugika . Wataalamu wanasema waatahitaji shillingi Billioni sita na miezi sita kushughulikia dhahma hiyo.
Photos (Baraka/Maduhu).....................
Katika hatua nyingine Raisi Muammar Gaddafi wa Libya ametoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko Kilosa pamoja na kuahidi kujenga Nyumba 200 zenye thamani ya Shillingi Billioni 1.5 kwa ajili ya waathirika hao. Du jamaa kweli ana moyo wa huruma ! Gaddaffi akiwa ziarani nchini Italia. Kwa Kisukuma sasa; Qaddafi arrives at Rome’s Ciampino airport with the usual retinue of 40 virgin bodyguards—all in lipstick and nail varnish—but without the camel that he transported to Paris on an official visit., Italy’s prime minister, Silvio Berlusconi, left, must have welcomed the arrival on Italian soil of a man with even more obviously dyed hair who made him look positively somber and statesman-like. By Alessandra Benedetti/Corbis

Posted by BM. on Sunday, January 17, 2010

Rais Barack Obama wa Marekani amewaomba Maraisi wastaafu wa nchi hiyo Bill Clinton na George W.Bush kusaidia kukusanya fedhaza kuisaidia Haiti iliyokubwa na tetemeko la Karne. Na katika kuonyesha umoja wao walionekana katika Mkutano wa pamoja na mapaparazi katika IKULU ya Marekani wakitangaza kuwa wataifanya kazi hiyo. Mshikamano huu ni mzuri au unasemaje....
Rais Barack Obama , Maraisi wastaafu Bill Clinton na George W.Bush wakijongelea eneo la mkutano White House... Tayari kuonana na mapaparazi...
Wameanzisha Obama alichokiita Clinton Bush fund kwa ajili ya Haiti

Shughuli imeisha..

Posted by BM. on Sunday, January 17, 2010

US First Lady... Safari ya Kimajukumu. Mr and Mrs Obama.
Usafi unapoendelea katika Ofisi ya Raisi Obama.

Posted by BM. on Friday, January 15, 2010


Ubalozi wa Tanzania nchini JAPANI kupitia mtanadao wake rasmi imetoa tangazo kwa umma kuwa imefungua kitabu cha maombolezo ambapo wale wanaohitaji kusaini kitabu hicho wanaweza kufika ubalozini Ijumaa (15/1)na Jumatatu 18/1) kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita na baadaye saa nane hadi saa kumi jioni. Unaweza kusoma tangazo halisi hapo chini.
The Embassy would like to inform the general public with deep sorrow the passing away of Honorable Mr. Rashidi Mfaume Kawawa, former Prime Minister and Second Vice-President of the United Republic of Tanzania, in Dar es Salaam on 31st December 2009.
Due to prior unavoidable circumstances, the Embassy has just now opened a book of condolences for signing at the Embassy on 15th and 18th January 2010 from 10:00 to 12:00 and from 14:00 to 16:00 hours. All are welcome for signing.
Tanzania Embassy, Tokyo

Posted by BM. on Wednesday, January 13, 2010

Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 limeikumba haiti saa chache zilizopita na na maelfu ya watu inasemekana wamekwama kwenye vifusi wengi wakiwa hai bado. Operesheni kubwa inaendelea kuwaokoa maelfu ya watu waliozikwa hai na vifusi vya majumba kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti ambalo halijawahi kutokea katika visiwa vya Caribbean.
Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 lilibomoa hospitali na majumba katika mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince na kusababisha maafa makubwa huku kila mtu aliyesalimika akihaha kumuokoa ndugu yake au ndugu zake waliofunikwa na vifusi.
Mamia ya watu wapo chini ya vifusi wakipiga kelele za kuomba msaada.
Tafadhali baadhi ya picha humu ndani ni zaa kutisha kidogo ...jiandae kisaikolojia... Unaweza kukadiria mtikisiko ulivyokuwa!...
Miili ya watu ikiwa imezagaa katika mji huo ambao mawasiliano ya simu yamekatika.
Matrekta yalionekana mitaani yakisaidia kufukua vifusi vya majumba mbali mbali yakiwemo makazi ya wanadiplomasia na wafanyakazi wa umoja wa mataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema Marekani tayari imeanza kutuma misaada ya dharura na Raisi Obama ametoa hotuba ya Pole kwa wa-Haiti.Wanajiolojia nchini Marekani wanasema tetemeko hilo la ardhi ndilo mbaya zaidi kwahi kuikumba Haiti kwa miaka mia mbili. Wataalamu hao pia wametoa tahadhari ya Tsunami.
Hali inapofikia hapo!

Posted by BM. on Monday, January 11, 2010

Usiku wa kuamkia leo J3...Jan.11 kulikuwa na mnuso wa haja jijini Tokyo katika Viunga vya Chofu kwa Comrade KK. Yaliyojiri ni mengi lakini kwa muhtasari nenda sambamba na kamera ya MIRINDIMO. mwenyeji wetu Dr. Kamu K na Katibu Mkuu wa Tanzanite Mr. MwombekiJnr. Katibu Mkuu wa Chama cha watanzania wanaoishi japani TANZANITE katika hafla hiyo.
Abby na mwenza Jamila na pembeni mdau Job Msuya kwa pembeni ..imetulia! Kamati ya ufundi. Kutoka kushoto Jonas Songora, Herman Mpangile na Mr. Donald Faustine...shughuli ilidhibitiwa... href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhiXzYQutZKo2Td_sl0fnYlrFKCQ8OC5AJiFAIcHBRjItsqGbGA40uS3MdvLeLwrdy4A9OzQdtDoSu_c1gb56-f3U7KuDS44PjdUnJQbyh2ImSsuVDlOYrnaS7jrl55cUPM-epyaOIkakk/s1600-h/FORCE+1+025.jpg"> Dr. KK timu mwenyeji ...na wageni waalikwa ...Kulia kwake Bw. Francis Mussongo aliyefanikisha mijadala ... imependeza! Benchi la Ufundi Kamarade Ndesika na mie, kamera imebidi niipokeze nami nifotolewe..... shughuli ni watu...Kushoto mamdogo Kavishe , kulia Bi. sabina!....imetulia.
Mweka hazina Msaidizi Tanzanite Mrs.Fatma Simba na Katibu Mkuu Mr. Mwombeki Jnrwalikuwepo.. Job Msuya , Mama Koku na Bi. Koku . Dah ! take 5.Ma Koku tumekubali! No Komenti...Hai tebo; Leticiz, Jamila Fatty Simba Hoja inapojengwa , hakuna linaloharibika...! Mrs.Singu, katika eneo tete la hafla hii... @Kwani ilikuwaje Jamila?..(Anza L-R; Leticia, Jamila..Mabesti wanapoteta...nahisi tu au nimechemsha? Itifaki imezingatiwa...Ninachosema!
Bro Amani Paul akitoa hoja ya kuunga mkono hoja ya uanzishaji wa mradi kabambe wa ...naniii!!
Hoja inapojengwa hakuna linaloharibika......Donald haya yanazungumzika tu...!. Ameelewa. Wageni waalikwa tabasamu la mjadala...!Herman Mpangile! hapo