Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, May 30, 2009

Unajua kitu kinachoitwa virusi kwenye komputa? Bila shaka kama ni mtumiaji wa komputa hicho sio kitu kigeni. Hii ni mada muhimu sana ni vyema ukaisoma kwa makini tena na tena . Pale unapoona komputa yako ikifanya vituko wengi wetu tunakimbilia programu za bure ambazo zinapatikana kirahisi kwenye internet. Lakini fahamu tu kuna programu FEKI za antivirus ambazo zitaharibu kompyuta yako. Kwanza kabla hatujaanza kuzungumzia programu hizo ni bora kwanza tukajua virusi ni nini kwa faida ya wale ambao neno hili huwa linawakanganya.Virusi ni programu ambazo watu wenye nia mbaya huzitengeneza kwa nia ya kuharibu kompyuta za watu wengine. Kompyuta yenye virusi huwa inachelewa kuwaka, inapowaka huwa inafanya kazi taratibu sana na mara nyingine hujizima na kujiwasha yenyewe bila wewe kufanya chochote.Kompyuta yenye virusi pia huwa mara nyingine inajizima kabisa na hata ukibonyeza kitufe cha kuwashia huwa haiwaki tena.Mara nyingine kompyuta yenye virusi huwa inatengeneza mafaili ya ajabu ajabu bila wewe kujua. Na mafaili hayo huifanya kompyuta yako ionekane kama vile hard disk yake imejaa wakati hujaweka chochote cha maana.Wakati kompyuta zetu tunapozihisi zina virusi kwa kuonyesha dalili kama hizo tulizozitaja hapo juu, wengi wetu tuna tabia ya kusachi kwenye google au yahoo na kutafuta programu ya antivirus ili kuziokoa kompyuta zetu.Kitendo hicho ni cha hatari kwakuwa bila kujua tunaweza tukadownload programu ambazo sisi tutadhani kuwa ni za kuondoa na kuzuia virusi kumbe hali halisi ni kinyume chake.Baadhi ya programu hizo ambazo ni feki badala ya kuzuia virusi hutuingizia virusi kwenye kompyuta zetu na hivyo kuziweka kompyuta zetu kwenye hatari. Baadhi ya programu hizo feki ambazo zinajulikana sana kuwa ni feki lakini mamilioni ya watu duniani wamekuwa wakiendelea kuzidownload ni hizi:PersonalAntiSpy, VirusGuardPlus, VirtualPCGuard, AntiMalware 2009, AntivirusProtection, Security Scanner 2008, VirusResponse Lab 2009, Antivirus Lab 2009, Antivirus Security, Micro Antivirus 2009, AntiSpyware Pro XP na XP Protector 2009. Zingine ni VirusHeat,VirusIsolator, Virus Locker, VirusProtectPro, VirusRemover2008, VirusRemover2009, VirusMelt, VirusRanger, Virus Response Lab 2009, VirusTrigger, Vista Antivirus 2008.

Kama unatumia mojawapo ya programu hizo basi ujue badala ya kuzuia virusi visiingie kwenye kompyuta yako, programu hizo zitakuwa zinavialika kwa wingi virusi ili viharibu kompyuta yako. Ufumbuzi wa tatizo hilo ni kwa wewe kuinstall programu zinazojulikana ambazo zitasafisha na kuzuia virusi vyote ambavyo vingeharibu kompyuta yako. Zifuatazo ni programu za uhakika ambazo unaweza ukainstall mojawapo na zitaifanya kompyuta yako iwe salama ziku zote.Kaspersky -- http://www.kaspersky.com/trials, Trend Micro -- http://emea.trendmicro.com/emea/downloads/sb/index.html?id=homepage_tab, Symantec -- http://www.symantec.com/norton/downloads/index.jsp, Panda -- ttp://www.pandasecurity.com/homeusers/downloads/evaluation/?sitepanda=particulares Avast -- http://www.avast.com/eng/download-avast-home.html, Antivir -- http://www.free-av.com/en/download/index.html. Makala hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Nifahamishe.
Tek keya!

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Picha hiyo juu inaonyesha wapenzi hao walivyokuwa miaka 81 iliyopita na picha ya chini hivi sasa. Jumanne wiki hii walisherehea miaka 81 wakiwa ndani ya ndoa thabiti na kuvunja rekodi nchini Uingereza kwa kukaa ndani ya ndoa kwa muda mrefu.
Mzee Frank na mkewe Anita Milford wote wakiwa na miaka 101 wanaishi pamoja katika nyumba ya kulelea wazee huko Plymouth, nchini Uingereza na rekodi inaonyesha walioana tarehe 26, Mei , 1928. Mzee Frank alistaafu miaka 41 iliyopita na bado wanaikumbuka vita ya pili ya dunia ya mwaka 1945 kuwa walinusurika mara mbili kufa kwa mabomu pale bomu moja lilipoanguka karibu ya nyumba yao. Wapenzi hao wana watoto wawili , wajukuu watano na vitukuu saba. Mtoto wao mkubwa ambaye pia anaitwa Frank kama baba yake ana miaka 74. Aisee bahati kubwa ! hebu nawe jiulize ulikaa miaka au miezi mingapi na mwenza wako wa MWISHO kabla hamjatibuana ?…....................ishakuwa tabu!

Frank na Anita

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Mdada mjasiriamali., Mtanzania anayeishi nchini Japani . jina na shughuli zake anazozifanya kwa undani unaweza kuyafuatilia kwenye mtandao wake. Bofya hapa;
www.mumyhery-jp.blogspot.com. take 5 dadake!

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Binti wa Kimursi huko kusini mwa Ethiopia akipitishwa katika pambo la mwisho la mdomo kabla ya kukabidhiwa mume.... mapambo yako mengi lakini hii mmmh!

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Mchuma umechuchumaa mbugani na kuna wanyama ...kwahiyo!Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Watoto wa madrasa ....Mikindani huko Mtwara..endeleeni wanangu!

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Msikiti wa zamani wa Mkumburu pemba...hist0ria tena ishakuwa.

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Hoteli ya Ngurudoto , mjini Arusha ..mtanzania ndiye mmilikiwa kitu hicho...hatua>>

Posted by BM. on Friday, May 29, 2009

Mwaka 2005 Raisi Mstaafu Benjamini Mkapa alipokuwa Ikulu alitembelea Rwanda kushoto kwake Risi Kagame na wake zao ..

Posted by BM. on Wednesday, May 27, 2009

KWIZ!.....Hapa wapi? Mdau P.PO Mwz-Tz alikuwa wa kwanza kutoa jibu ...Kinondoni mbuyuni. Take 5.

Posted by BM. on Wednesday, May 27, 2009

Sore kwa kisukuma kidogo!...If you can find a woman that sticks with you through thick and thin, it means she sees something broadly potential in you and will fuel your motivation. That is where the saying " Where there is a successful man, not far behind is the..... "
All a Man needs is a patient woman, to watch his dreams fall to place and to quit nagging a brother...you think she knew he would become the US president at this time?...I don't think so...but she stuck with him... Wow!...

Mwanamke mazingira!....

Posted by BM. on Wednesday, May 27, 2009

US First Lady Michelle Obama na mtu mashuhuri duniani Oprah Winfrey wakifotolewa na mapaparazi wa jarida la Time la Marekani...safii!

Posted by BM. on Wednesday, May 27, 2009

Mmoja wa waandishi wakongwe Marekani na duniani kwa ujumla wa kiwango chake mwenye makazi yake jijini New York Bi. Helen Thomas, ambaye alifanya kazi ya kuandika habari za matukio yote yaliyomuhusisha raisi wa zamani wa Marekani John F. Kennedy miaka ya 1960 na anaendelea na kazi hiyo hadi sasa . Hapa alikuwa katika Mkutano wa Bw. Obama April 29. Raisi Kennedy aliuwawa mwaka 1963, Nov. 23 akiwa bado madarakani.

Posted by BM. on Wednesday, May 27, 2009

Ushafika Unguja weye..bass lazima ushapanda kunako hicho chombo..

Posted by BM. on Saturday, May 23, 2009

Kijiji cha Hua Hin nchini Thailand , usafiri mbadala wa migongo ya tembo. Nasi bongo kwanini tusifanye jitihada ili hatimaye tusilalamike tembo wana roho mbaya bali tuwatumie.
Sasaaa!Jumapili wiki iliyopita kulikuwa na tamasha kubwa katika bustani za Yoyogi , jijini Tokyo hapa Japani. Tamasha hili lilikuwa sehemu ya maonyesho ya siku ya WaThailand ambapo bidhaa, utamaduni, vyakula , ngoma na kadhaa kadhaa za watu wa Thailand zilionyeshwa.
Nchi hii ya Thailand iliyopo barani Asia ni ndogo kwa eneo ikilinganishwa na Tanzania ingawa idadi ya watu wao ni takriban 60 millioni na hivyo wanaizidi Tanzania kwa watu zaidi ya Millioni 20. Maonyesho yalikuwa mazuri mno. Watu walifurika Pomoni, Mabanda zaidi ya 60 ya wathailand yalikuwa uwanjani hapo mengi yalikuwa ya vyakula, nguo , matunda na bidhaa nyingine. Matunda aina ya maembe yalitia fora kwa wingi wake na bei yake iliyoanzia yeni 750 kwa embe moja ikiwa ni sawa na shilingi za kitanzania elfu 11.
Kwa saa moja na nusu nilizozitumia kuzunguka katika mabanda hayo sikubahatika kumuona mtu mweusi kama mimi hadi wakati naondoka ambapo macho yangu yakagongana na jamaa mmoja mwenye ngozi kama yangu. Nilimsalimia , naye akaitikia kwa Shauku na kuniuliza , unatoka Marekani au Afrika nami nikamjibu Afrika nchini Tanzania. Akatabasamu na kunipa mkono huku akiniuliza Jambo rafiki! Tukacheka na mazungumzo yakaendelea. Huyu alikuwa Mmarekani mweusi aliyewahi kukaa Tanzania miaka ya nyuma. Alitumia muda mwingi wa mazungumzo yetu kuisifu Tanzania na rasilimali za Afrika. Lakini akasema kuwa kinachomkera zaidi ni kuwa pale linapojitokeza tamasha kama hilo kwa nchi za Kiafrika hapati kuona kile alichokiona kule Afrika. Kwa ujumla Afrika haitoi sura halisi ya kile ilichonacho.
Wakati tunaachana aliniuliza swali ; hivi unajua Wajapani wengi hawajui kuwa ugali wa Kitanzania kuwa ni chakula kitamu sana, nikajibu,,,ni kweli. Unafanyaje sasa! ….Tukacheka kila mtu akashika njia yake..Wiki iliyofuata kulikuwa na tamasha la Kiafrika katika jiji la Yokohama hapa Japani . Bahati mbaya miye sikuhudhuria. Lakini mmoja wa wadau wa karibu katika tamasha hilo alikuwa Fresh Jumbe Mkuu , mwanamuziki mwenye historia iliyotukuka. Nilimuuliza kilichojitokeza katika tamasha hilo huku kivuli cha maneno ya yule Mmarekani kikiwa kimeniinamia. Hebu hakikisha unafuatilia alichokisema Fresh Jumbe katika website ifuatayo ; http://www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili ukipata huo ukurasa subiri kesho jumapili tarehe 24 , bofya kwenye ukumbi wa jumapili. Kwa kifupi alichosema Jumbe kinafanana na Mmarekani yule, kuwa Afrika tumelala! tuna changamoto ya kujitangaza zaidi kuliko tunavyofanya sasa na sio tu kwa Japani bali katika mataifa yote yaliyoendelea …au unasemaje mwananchi?

Fresh Jumbe Mkuu...ndani ya nyumba jijini Tokyo, Japani.

Posted by BM. on Friday, May 22, 2009

Mtu anapiga hodi , unakwenda kufungua . heeh , mgeni mwenyewe huyo hapo sasa inakuaje!

Posted by BM. on Friday, May 22, 2009

Mwanamke mjamzito jijini Lima huko Peru akichorwa katni tumboni kama maandalizi ya sherehe ya uzazi salama huko Peru...hii ilikuwa tarehe 20, May 20. Kwa mujibu wa Shirika la habari la China la Xinhua sherehe hiyo ilifana.

Posted by BM. on Friday, May 22, 2009

Heeh!

Posted by BM. on Friday, May 22, 2009

Raisi wa Marekani BarackObama alikutana na Raisi jakaya Kikwete Jana Alhamisi White House. Mazungumzo hayo yanatajwa kuwa yalikuwa ya faragha na hawakutana kuongea pamoja mbele ya waandishi wa habari kama ilivyozoeleka kwa wageni wengine na Raisi Kikwete aliondoka kikwete bila kusema chochote kwa waandishi wa habari ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu kubwa. Aliwapungia tu na kuondoka. Msemaji wa Obama Bw. Robert Gibbs alisema kuwa walizungumzia masuala ya usalama na ugaidi , uchumi na afya. Bila shaka mazungumzo yalikuwa mazito. Mh. J.Kikwete naye bila shaka alijiandaa vya kutosha, naona alikuwa na kifaa mkononi akidondoa hoja. (Washington Post na Ikulu)

Kwaherini waandishi...
Duh hawa jamaa sijawaambia chochote...anyway!

Posted by BM. on Thursday, May 21, 2009

Chumba cha mtihani.

Nchini Tanzania wakati huu kunaendelea zoezi ya mitihani ya kujiweka sawa na ile ya mwisho ya kumaliza darasa la saba maarufu kwa jina la Mock. Na hii inaingia katika rekodi ya maendeleo ya mtoto. Hapa ni wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Maendeleo huko Mbagala Kuu karibu na sehemu ambako mabomu yaliliripuka wakifanya mtihani huo. Duh tutafika kweli!
Thanks -BongoPix

Posted by BM. on Thursday, May 21, 2009

Makomredi wanapokutana...

Posted by BM. on Sunday, May 17, 2009

Jumamosi ya 18/05 jijini Tokyo viwanja vya taifa Yoyogi kulikuwa na maonyesho ya bidhaa na utamaduni wa Wathailand , watu walijaa wakala na kunywa na kazalika...

Ngoma ya kithai ilikonga nyoyo za watu waliokuwepo hapo.
Shuhuda..kwa macho yangu!

Mabanda ya bidhaa na vyakula kila kona...
Mpatempate...
Kijibaridi na kijiupepo kilikuwepo...
Matunda; bei kwa tunda hiyo hapo Y eni nanihii zidisha kwa 15 upate bei ya nyumbani Ukipiga hesabu hiiyo utaishia kukodoa jicho tu .... Kama utani vile!

Posted by BM. on Sunday, May 17, 2009

Unweza kuamini kuwa huyo alikuwa mwanaume rijali wa kupewa mke akaamua kujibadilisha na kuwa mwanamke kama unavyomuona...Hii ndiyo dunia ya leo ya sayansi na teknolojia . Hebu fuatilia mashindano ya ulimbwende ya watu waliopata kuwa wanaume katika maisha yao yaliyofanyika huko Thailand hivi karibuni...

Kama ilivyokuwa miaka mingine, mwaka huu pia mashindano ya kumtafuta mrembo wa mashoga yamefanyika nchini Thailand yakishirikisha mashoga 30, huwezi amini kama hawa zamani walikuwa wanaume rijali. Picha za mashoga hao mwisho wa habari hii.Mashindano hayo kutokana na kutotambulika katika nchi nyingi duniani, kila mwaka hufanya nchini Thailand.Mashoga wanatambulika nchini Thailand kama jinsia ya tatu na wanajulikana nchini humo kama 'Katoey.'Huu ni mwaka wa 12 kwa mashindano hayo kufanyika na mashoga 30 walishiriki kutafuta mrembo kati yao katika mji wa utalii wa Pattaya nchini humo.Mashoga hao walipita mbele ya mamia ya watu waliofurika kushuhudia tukio hilo wakiwa wamevalia mavazi mbali mbali kuanzia viguo vya kuogelea mpaka vya kulalia.Mwisho wa mashindano hayo shoga nambari 26 aliyejulikana kwa jina la Sorawee Nattee aliibuka mshindi na kuvikwa taji lake la mrembo wa mashoga au "Miss Tiffany" kama shindano hilo linalovyojulikana.

Ukishitukizwa unaweza kujua kuwa hawa ni mashoga waliofanyiwa upasuaji wakawa hivyo...Duh!


Posted by BM. on Sunday, May 17, 2009

Hawa ni watu muhimu sana katika historia ya Tanzania. Bila shaka Mwalimu J.K.Nyerere anafahamika vizuri tu. Kuliakwake ni Bibi Titi Mohammed. Huyu ni mmoja wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri na pia ni kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika wakati ule , akiwa na ushujaa mkubwa kuongea majukwaani , wakati huo ilikuwa kitu cha nadra sana!
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na Mwalimu nyerere aliyekuwa Raisi wa Tanzania. Wote sasa ni marehemu lakini historia zao bado zi hai...

Posted by BM. on Sunday, May 17, 2009

Raisi wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma katika moja ya hafla ya kusherehekea ushindi wake na chama chake cha ANC.....naye yumo!.

Posted by BM. on Saturday, May 16, 2009

Leo jumamosi na kesho jumapili (tarehe 16/17 mei) kutakuwa na maonyesho ya African Festa kule Yokohama Akarenga Soko. Hivyo kama uko nchini Japani hivi sasa ,usikose burudani hii ambapo utaweza kula vyakula vya kiafrika na pia kuburudika na muziki toka nchi mbalimbali za kiafrika. Band ya kitanzania ya Tanzanite chini ya Fresh Jumbe Mkuu itakuwa inaburudisha siku ya tarehe 17(jumapili) . Kwa habari zaidi kuhusu maonesho haya tembelea tovuti hii http://www.africanfesta2009.com/

Fresh Jumbe akizikonga nyoyo za wapenzi wake hapa Japani.

Posted by BM. on Saturday, May 16, 2009

Nimebahatika kuishi na kufanya kazi za upaparazi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na majiji makubwa kama vile Dar es salaam , Arusha , Mbeya , Mwanza na Zanzibar.Nimeshuhudia tofauti fulani fulani za tamaduni, mila na hata lafudhi zilizopo baina ya watu kati ya sehemu moja na nyingine.
Lakini kuna baadhi ya mambo yanafanana kila mahali. Mojawapo ni utamaduni wa kutosoma vitabu. Si kitu cha kawaida kumuona mtu hususan aliye na umri mkubwa akiwa anasoma kitabu chake kwa makini bila kuwa na shinikizo lolote kama vile kusoma kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ama kazi za kiofisi. Tatizo hilo halipo tu kwa watu wazima , bali kwa watu wa umri wa kati, wasomi, mapaparazi, wanafunzi wanafamilia wanawake kwa wanaume na hata watoto.
Kilichoshika kasi wakati huu ni watu kuchangamkia magazeti ya udaku ama yale yaliyoandikwa kwa stairi ya udaku ambayo hayahitaji kuumiza kichwa, kufikiri ,kukariri wala kuwa na nukuu nyingi. Ama pia Redio na TV .
Sababu nyingi zinatajwa ikiwa ni pamoja na hali ngumu ya uchumi kwamba watu hawezi kununua vitabu, majarida au magazeti yanayotajwa kuwa makini ambayo bei yake ni ya juu. Sina hakika hilo lina ukweli kwa kiasi gani. Hapa Japani kwa mfano unapopanda treni ama basi huwezi kumkuta mtu kajikalia bila kufanya kitu Fulani kama vile kusoma gazeti , jarida , kitabu, kuangalia ujumbe katika simu yake na kadhalika. Na kwa maana hiyo utulivu ndani ya vyombo vya usafiri ni mkubwa. Hali kama hiyo ipo katika nchi nyingi zilizoendelea . Swali hapa ni kuwa kulikoni nyumbani hii imeshindikana?. Hususan ya usomaji vitabu ? Nilianza na kuitaja miji mikubwa nikiamini kuwa hata upatikanaji wa vitabu wenyewe ni mkubwa na mzunguko wa fedha angalau ni afadhali kidogo ikilinganishwa na vijijini . lakini bado watu wa mijini hawana tabia ya kusoma pia. Sasaaa haka ni kagonjwa au au... unasemaje!.... Tafadhali ukiwa na maoni yoyote unataka yaingie kwenye Mirindimo ya Jumamosi niandikie kwa kutumia anuani ya barua pepe; brmsulwa@yahoo.comPosted by BM. on Saturday, May 16, 2009

Haya mara ya mwisho lini kujikumbushia hesabu kama hizi? Kuti kavu magerezani....

Wacha Kipindupindu, TB, UKIMWI sasa mafua ya nguruwe na ya ndege ...itakuwaje kwenye misongamano kama magerezani?Posted by BM. on Saturday, May 16, 2009

Hali ya magereza nchini Brazil...Msongamano wa wafungwa na mahabusu. Hivi watawala kote ulimwenguni hususan katika nchi zetu ikiwemo Tanzania wanafikiria kitakachotokea pindi ukizuka ugonjwa wa mafua ya nguruwe hapo...siju!

Posted by BM. on Friday, May 15, 2009

Jana Alhamisi nilitembelea Chuo kikuu cha Kilimo jijini Tokyo nikakutana na makomredi kutoka Tanzania Jerome Mghase(Kushoto) na Emanuel Mgonja (Kulia) wakila nondo hapo Chuo. Matumaini ya watanzania katika kilimo ca Mpunga kwa waheshimiwa hawa. Take 5...

Posted by BM. on Friday, May 15, 2009

Watafiti wa kilimo cha mpunga kutoka chuo cha Utafiti Ifakara mkoani Morogoro hivi sasa wako Chuo Kikuu cha Tokyo Japani kula kitabu kuhusa aina mpya ya mpunga inayoitwa NERICA. Kuliani Jerome Mghase na Kushoto Emanuel Mgonja ...kila la kheri. Mahojiano zaidi na wataalamu hao bofya ; http://www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili/top/index.html

Posted by BM. on Friday, May 15, 2009

Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Dr. Alex Nsekela kushoto akikabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro Kulia anayetokea Dar es salaam. Bila shaka atampa situeshen ya hapo Mwz.

Posted by BM. on Thursday, May 14, 2009

Norma Stitz mkazi wa Atlanta, Georgia nchini Marekani ameingia rasmi kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness na kutambulika kama mwanamke mwenye matiti makubwa ya asili kuliko wanawake duniani, matiti yake yana ukubwa wa sentimeta 72 na uzito wa kilo 24. ViDEO yake mwisho wa habari hii.
Norma Stitz ndiye mwanamke anayevaa sidiria kubwa kuliko zote duniani akiwa na matiti makubwa ya asili ambayo hayawahi kufanyiwa operesheni yoyote ile ya kuyaongeza.Norma aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1999 wakati huo matiti yake yakiwa na kipimo cha 70-48-52 na sidiria yake ilikuwa saizi 48V.Hivi sasa Norman amezidi kujiweka sawa katika rekodi yake hiyo kwani hivi sasa akiwa na umri wa miaka 30 matiti yake yameongezeka ukubwa na saizi ya sidiria yake ni 120XXX na kila titi moja lina uzito wa kilo 12 huku uzito wa mwili wake kwa ujumla ni kilo 157 hivi sasa.Norma Stitz mwenye umri wa miaka 30 anasema kwamba anafurahia ukubwa wa matiti yake ingawa watu wengi humuuliza "kwanini hufanyi operesheni ya kuyapunguza?".Norma anasema kwamba tatizo kubwa analopata kutokana na ukubwa wa matiti yake ni wanaume anaokutana nao kushindwa kabisa kuzungumza chochote na kubaki wakiyakodolea macho matiti yake."Nataka wanaume wavutike na mimi kama nilivyo sio wavutiwe na matiti yangu tu" alisema Norma.Norma amesema kwamba amekuwa akipata mialiko kwenye televisheni mbali mbali duniani ili kuyaonyesha matiti yake.Norma hivi sasa anajishughulisha kupiga picha za ngono na anaendesha tovuti yake binafsi ambayo humo anamwaga radhi kwa mapicha yake ya ngono