Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, May 30, 2009

Unajua kitu kinachoitwa virusi kwenye komputa? Bila shaka kama ni mtumiaji wa komputa hicho sio kitu kigeni. Hii ni mada muhimu sana ni vyema ukaisoma kwa makini tena na tena . Pale unapoona komputa yako ikifanya vituko wengi wetu tunakimbilia programu za bure ambazo zinapatikana kirahisi kwenye internet. Lakini fahamu tu kuna programu FEKI za antivirus ambazo zitaharibu kompyuta yako. Kwanza kabla hatujaanza kuzungumzia programu hizo ni bora kwanza tukajua virusi ni nini kwa faida ya wale ambao neno hili huwa linawakanganya.Virusi ni programu ambazo watu wenye nia mbaya huzitengeneza kwa nia ya kuharibu kompyuta za watu wengine. Kompyuta yenye virusi huwa inachelewa kuwaka, inapowaka huwa inafanya kazi taratibu sana na mara nyingine hujizima na kujiwasha yenyewe bila wewe kufanya chochote.Kompyuta yenye virusi pia huwa mara nyingine inajizima kabisa na hata ukibonyeza kitufe cha kuwashia huwa haiwaki tena.Mara nyingine kompyuta yenye virusi huwa inatengeneza mafaili ya ajabu ajabu bila wewe kujua. Na mafaili hayo huifanya kompyuta yako ionekane kama vile hard disk yake imejaa wakati hujaweka chochote cha maana.Wakati kompyuta zetu tunapozihisi zina virusi kwa kuonyesha dalili kama hizo tulizozitaja hapo juu, wengi wetu tuna tabia ya kusachi kwenye google au yahoo na kutafuta programu ya antivirus ili kuziokoa kompyuta zetu.Kitendo hicho ni cha hatari kwakuwa bila kujua tunaweza tukadownload programu ambazo sisi tutadhani kuwa ni za kuondoa na kuzuia virusi kumbe hali halisi ni kinyume chake.Baadhi ya programu hizo ambazo ni feki badala ya kuzuia virusi hutuingizia virusi kwenye kompyuta zetu na hivyo kuziweka kompyuta zetu kwenye hatari. Baadhi ya programu hizo feki ambazo zinajulikana sana kuwa ni feki lakini mamilioni ya watu duniani wamekuwa wakiendelea kuzidownload ni hizi:PersonalAntiSpy, VirusGuardPlus, VirtualPCGuard, AntiMalware 2009, AntivirusProtection, Security Scanner 2008, VirusResponse Lab 2009, Antivirus Lab 2009, Antivirus Security, Micro Antivirus 2009, AntiSpyware Pro XP na XP Protector 2009. Zingine ni VirusHeat,VirusIsolator, Virus Locker, VirusProtectPro, VirusRemover2008, VirusRemover2009, VirusMelt, VirusRanger, Virus Response Lab 2009, VirusTrigger, Vista Antivirus 2008.

Kama unatumia mojawapo ya programu hizo basi ujue badala ya kuzuia virusi visiingie kwenye kompyuta yako, programu hizo zitakuwa zinavialika kwa wingi virusi ili viharibu kompyuta yako. Ufumbuzi wa tatizo hilo ni kwa wewe kuinstall programu zinazojulikana ambazo zitasafisha na kuzuia virusi vyote ambavyo vingeharibu kompyuta yako. Zifuatazo ni programu za uhakika ambazo unaweza ukainstall mojawapo na zitaifanya kompyuta yako iwe salama ziku zote.Kaspersky -- http://www.kaspersky.com/trials, Trend Micro -- http://emea.trendmicro.com/emea/downloads/sb/index.html?id=homepage_tab, Symantec -- http://www.symantec.com/norton/downloads/index.jsp, Panda -- ttp://www.pandasecurity.com/homeusers/downloads/evaluation/?sitepanda=particulares Avast -- http://www.avast.com/eng/download-avast-home.html, Antivir -- http://www.free-av.com/en/download/index.html. Makala hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Nifahamishe.
Tek keya!

0 comments: