Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Mto unaopita katikati ya jiji la Bangkok nchini Thailand umefurika hapo jana na kupasua baadhi ya kingo zake.Mto Chao Phraya ulioko Bangkok

Barabara nje ya Bangkok zimejaa magari, wakati maelfu ya watu wakiyakimbia mafuriko hayo, ambayo ni mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika nusu karne. Magunia ya mchanga yamewekwa katika majengo mbalimbali mjini humo ili ya kuyakinga dhidi ya maji yanayozidi kufurika.

Wakaazi wamekumbana na mamba na nyoka ambao wanaokimbia mashamba yaliofurika. Televisheni nchini humo zinaonyesha msongamano wa magari yaliokuwa yakiondoka mjini humo lakini idara ya trafiki imesema, haikuweza kutoa idadi kamili ya watu wanaouhama mji wa Bangkok, kwani kamera nyingi za barabarani zimefunikwa na maji.

Mpaka sasa, janga hilo la mafuriko la miezi mitatu nchini humo, limekuwepo katika majimbo ya kaskazini na ya kati. Takriban watu 400 wameuawa.

Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Chama cha waandishi wa habari za Michezo kiliwakutanisha wadau wake mjini Morogoro hivi karibuni kwa ajili ya kozi fupi...Picha inayoonyesha moja ya mishemishe za wana-sports hao wakiwa mji kasoro bahari... thanx mdau!

Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Sauti zilizopotea...Tx Moshi William, Suleiman Mbwembe, 'Kinyonga, Joseph Maina, Momba... nani atazipa pengo...
Bonyeza hapo chini ya picha ya juu usikiliza kitu mzee wa mimba!... !


Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Kijana mmoja raia wa Kenya Elgiva Bwire Oliacha amehukumiwa na mahakama moja ya jijini Nairobi kifungo cha maisha baada ya kumtia hatiani kufuatia kukiri kwake kuwa yeye ni mfuasi wa al shabaab na aliyetekeleza shambulizi la gureneti kwenye kituo cha mabasi mapema wiki hii.

Elgiva Bwire Oliacha kwa jina jingine Mohammed Seif(pichani juu) alikiri kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 20 baada ya kuwarushia guruneti.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu mkaazi Grace Macharia, alisema mahakama imeridhika kuwa alipanga kuwaua watu wengi na lazima apewe adabu kali.
"Ili iwefunzo kwa watu wengine wenye nia kama yako, mahakama imeona vyema itoe kifungo hicho cha maisha kuwazuia kupanga harakati kama zako" alisema Hakimu Macharia.

Bw Bwire pia atatumikia kifungo cha miaka 15 kwa kuwa mwanachama wa kundi la al -shabaab ambalo limepigwa marufuku nchini Kenya na miaka mengine 7 kwa kupatikana na silaha bila kibali.
Mama yake mzazi anasemaje lakini!!!!!?

Posted by BM. on Saturday, October 29, 2011

Katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa Japani leo kulikuwa na maonyesho mbalimbali yaliyojumuisha maonyesho ya kazi za idara zake mbalimbali, burudani, makongamano, uuzaji wa vyakula na michezo. Baadhi yetu tulihudhuria...
Nilikuwepo!


WaTZ (L-R)Rahel, Upendo& Francis

Shughuli ndani ya shughuli...

Posted by BM. on Thursday, October 27, 2011

Zanzibaree!nimeipenda eeh!...

Posted by BM. on Thursday, October 27, 2011

Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman ni mmoja kati ya watu wanne muhimu wanaoweza kushika nafasi ya Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.Nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Luis Moreno-Ocampo itakuwa wazi hapo mwakani baada ya Bw Ocampo kumaliza kipindi chake cha utumishi wa miaka tisa mwakani.( Picha ya juu Jaji Othman na ya chini Jaji Ocampo)
Taarifa za UN, Tanzania wagombea wengine ni pamoja na Naibu Mwendesha Mashtaka wa sasa Fatou Bensouda wa Gambia, ambaye wengi wanamwona kuwa analeta ushindani mkali.
Anaungwa mkono na Umoja wa Afrika ambao mara nyingi umemkosoa Moreno-Ocampo kwa kufungua uchunguzi wa mataifa ya Afrika pekee.Katika orodha hiyo pia yupo Andrew Cayley, mwendesha mashtaka mwenza katika mahakama maalum ya Khmer Rouge nchini Cambodia anayetokea Uingereza. Mwingine ni Robert Petit, ambaye ni mshauri kuhusu uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita katika Kitengo cha Mahakama nchini Canada.

Kamati ya iliyoundwa na nchi wanachama wa mahakama hayo awali ilikuwa na orodha ya majina 52 ya wagombea walioomba kupendekezwa katika nafasi hiyo ya juu. Kamati hiyo iliwahoji wanane kabla ya kupata wagombea wanne."Wote wana uzoefu wa kitaaluma na utaalamu na pia wana sifa binafsi muhimu kufanya majukumu ya mwendesha mashtaka katika kiwango cha hali ya juu"
Jaji Othman ameshika nafasi muhimu mbalimbali za uandamizi katika mfumo wa sheria nchini Tanzania na alikuwa mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama maalum ya mauaji ya Rwanda na pia mwendesha mashtaka katika Utawala wa Mpito wa Umoja wa Mataifa katika Timor Mashariki.
Source: BBC

Posted by BM. on Thursday, October 27, 2011

Mjasiriamali Caleb Muchungu , raia wa Kenya anayeishi Malawi alikuja jana katika Ofisi zetu za Shirika la Utangazaji la Japani kututembelea.. tulifurahi kukutana naye na pia kufanya mahojiano naye.

Posted by BM. on Sunday, October 23, 2011

Posted by BM. on Sunday, October 23, 2011

Al Shabaab militants were on the back foot on Saturday evening as they faced heavy bombardment from multiple fronts from a combined force of Kenyan troops, US drones, African Union peacekeepers and Transitional Federal Government fighters.

Reports from the battlefront indicated that Kenyan troops were advancing towards four al Shabaab-controlled towns as they launched a final push to capture the Kismayu port and Afmadow in Central Jubaland.There was progress on the diplomatic front, too, when the Intergovernmental Authority on Development (Igad) member states endorsed the military offensive against the militants during a special conference held in Addis Abba Ethiopia on Friday.The Igad Council of Ministers urged the United Nations Security Council to impose a blockade on Kismayu, a move which will effectively cut off billions of shillings collected by the militants to fund their insurgency.
Source: The Kenyan sunday Nation

A statement from the military said Kenyan security forces were advancing towards Burgavo town in southern Somalia after capturing Oddo on Friday

Posted by BM. on Sunday, October 23, 2011

Posted by BM. on Sunday, October 23, 2011

Polisi katika jiji la Suita, Osaka hapa Japani wamesema kuwa wamemkamata mwanamme mmoja akituhumiwa kuvunja sheria ya unyanyasaji dhidi ya watoto baada ya kusemekana kuwa alimlazimisha mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 11 kuomba katika mitaa ya Suita , Osaka.

Habari iliyoandikwa na moja ya magazeti ya hapa inaeleza kuwa kuwa baba huyo anayefanya kazi ya ujenzi mwenye umri wa miaka 33alimwambia mwanawe akae kando ya barabara na awaambie wapita njia kuwa amepoteza pochi yake na bila shaka wangemuonea huruma na kumpatia fedha.Baada ya Polisi kumkamata kijana huyo ,aliwaambia kuwa alikuwa akifanya hivyo mara tano hadi sita kwa siku na alikuwa akipata takriban Yeni 2000 kwa siku (zaidi ya elfu 40 za Tz) ambazo alimpa baba yake.
Hatua iliyofuata ilikuwa ni kumkamata baba wa mtoto huyo ambaye alikutwa pembeni mwa bustani moja akisubiri mwanawe kukusanya pesa na ndio alipodakwa.
Alipohojiwa baba wa mtoto huyo alikana kumwambia mwanawe aombe, na kwamba anahisi ilikuwa ni mapenzi yake tu kufanya hivyo!...Bila shaka atafikishwa mahakamani akituhumiwa kukiuka haki za mtoto na kusababisha usumbufu kwa watu wengine...

Posted by BM. on Friday, October 21, 2011


SIRTE, Libya (Reuters) - Disturbing images of a blood-stained and shaken Muammar Gaddafi being jostled by angry fighters quickly circulated around the world after the Libyan dictator's dramatic death near his home town of Sirte.
The exact circumstances of his demise are still unclear with conflicting accounts of his death circulating. But the footage, possibly of the last chaotic moments of Gaddafi's life, offered some clues into what happened.

Gaddafi was still alive when he was captured near Sirte. In the video, filmed by a bystander in the crowd and later aired on television around the world, Gaddafi is shown being dragged off a vehicle's bonnet and pulled to the ground by his hair.
"Keep him alive, keep him alive!" someone shouts. Gunshots then ring out. The camera veers off.
"They captured him alive and while he was being taken away, they beat him and then they killed him," one senior source in the NTC told Reuters. "He might have been resisting."
Further television footage showed what appeared to be Gaddafi's lifeless body being loaded into an ambulance in Sirte.

An NTC spokesman in Benghazi, Jalal al-Galal, said a doctor who examined Gaddafi when he arrived in Misrata found he had been shot in the head and abdomen.

Posted by BM. on Thursday, October 20, 2011

Makamanda kutoka baraza la mpito la Libya wamesema wamemkamata aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.Taarifa hizo zimetolewa baada ya majeshi ya baraza hilo la mpito kudai kudhibiti Sirte, mji alipozaliwa Kanali Gaddafi.

"Amekamatwa. Amejeruhiwa miguu yake yote miwili," afisa wa baraza la mpito la taifa (NTC) Abdel Majid ameliambia shirika la habari la Reuters."Amechukuliwa na gari la kubebea wagonjwa."
Shirika la habari la AFP limemnukuu afisa mwengine wa NTC, Mohamed Leith, akisema Kanali Gaddafi amekamatwa mjini Sirte na "amejeruhiwa vibaya" lakini bado anapumua.
Taarifa zaidi baadaye...
source: BBC

Posted by BM. on Wednesday, October 19, 2011

Serikali za Kenya na Somalia zimekubaliana kushirikiana ili kuwaangamiza wanamgambo wa Kisomali wa Al-shabab.
Mkutano ulifanyika jana jumanne mjini Mogadishu na kuwakutanisha Waziri wa mambo ya nje Moses Wetang’ula na wa ulinzi Yusufu Haji wa Kenya na Raisi wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed pamoja na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed na kwa pamoja walikubaliana kufanya mashambulizi makali dhidi ya al-Shabab.
Wakati mkutano huo ukiendelea , bomu limeripuka nje ya makao makuu ya zamani ya wizara ya mambo ya nje ya Somalia kujilipua .
Majeshi ya Kenya yameingia ndani ya Somalia eneo la Afmadow lililopo kilometa 120 ndani ya Somalia.
Hali ndio hiyo!...
Wakati huo huo.. Maafisa wa Ufaransa wametangaza kuwa mama raia wa kifaransa aliyetekwa nyara kutoka Kenya na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kisomali wa al Shabab mapema mwezi huu amefariki.Maafisa wa kibalozi wanasema walifahamishwa kifo cha Marie Dedieu na watu ambao wamekuwa wakijaribu kuzungumza na watekaji nyara ili wamuachie huru mama huyo. Haijulikani alikufa lini na nini kilichosababisha kifo chake, ingawa inakumbukwa kuwa afya yake ilikuwa dhaifu na kuwa hakuruhusiwa kutumia dawa,na kwamba tukio kama hili lilitarajiwa.

Bi. Dedieu mwenye umri wa miaka 66 ni mmoja wa wageni kutoka mataifa ya magharibi waliotekwa kutoka Kenya mwezi October.Mwezi September raia kutoka Uingereza David Tebbutt aliuawa na mke wake Judith kutekwa katika hoteli moja ya kifahari huko Kiwayu pwani ya Kenya.Na mwezi jana wanawake wawili raia wa Uhispania wafanyakazi wa misaada walitekwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.Wanawake wote watatu waliotekwa bado hawajulikani walipo.
Somalia imekabiliwa na mapigano ya mwenyewe kwa wenyewe kwa miongo miwili, hili limesababisha silaha kupatikana kwa urahisi na kuna makundi mengi ya watu wenyewe silaha ambao pia wanaweza kuwa walihusika na utekaji huo.
Al-Shabab wamekanusha kuhusika na utekaji nyara wowote na wameonya kuishambulia Kenya ikiwa wanajeshi wake hawataondoka. Tusubiri tuone hatima ya Kenya kuivamia Somalia!

Posted by BM. on Wednesday, October 19, 2011

Ni tafakuri tu...: Nilikutana na mwanafunzi mmoja anayesoma Chuo Kikuu kimoja mkoani Hokkaido hapa Japani, ambapo pamoja na mambo mengine tuliyoongea aliniambia jambo moja ambalo imebidi nilitafakari. Alisema kuwa inamuia vigumu sana kuongea mbele ya kadamnasi. Ana aibu sana, na hali hiyo inamkera. Udhaifu huo humpata pia hata akiwa katika kundi dogo hususan hususan likiwa na mchanganyiko wa jinsia. Katika tafakuri hii, najaribu kuiangalia aibu kama haiba ya kipekee ya binaadamu.

Nilijiuliza kwani aibu ninini? nikajijibu; Aibu ni mhemko ambao unaathiri hisia za mtu na hali hiyo kujitokeza mbele ya watu wengine. Kuona aibu kuna tafsiri nyingi moja wapo inaweza kuwa kutojisikia vyema ,upweke , kuwa na wasiwasi, uoga au kujihisi kutokuwa salama. Watu wengine hushikwa na aibu pale wanapokuwa na fadhaa, hawana cha kufanya , hawajiamini , hujihisi udhaifu kimwili au kiakili au kukosa nguvu kwasababu ya tukio Fulani lililomtokea.
Aibu ni kinyume cha kuwa na utulivu , amani au furaha ya wazi mbele ya wengine. Inajitokeza kuwa mtu anayejisikia kusita kusema au kufanya kitu anachodhamiria katika nafsi yake kukifanya .Pengine swali linabaki kuwa , kwanini baadhi ya watu wana aibu na inatokana na nini?
Aibu ni sehemu ya jini (genes) . Hii ni sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile Fulani ambapo mtu huzirithi kutoka kwa wazazi au kizazi chake. Kuna watu ambao hawana ‘chembe ya aibu’ na wengine huwa na aibu ‘inayochusha’ na hiyo hujitokeza wakati Fulani kwenye kizazi chake. Wakati mwingine hali hii hutokana na tabia alizojifunza au tajiriba ya maisha yao. La kujua hapa ni kuwa jini (Genes) zetu ‘huamua’ juu ya mienendo ya tabia zetu, rangi ya macho, rangi ya mwili, aina ya mwili wako n.k Lakini pia jini huwezesha aina Fulani ya haiba ya mtu ikiwa ni pamoja na kuwa na aibu.

Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa baadhi ya watu huchukia kuwa na aibu. Lakini kuwa na aibu ingawa kwa upande mwingine kuna faida za kuwa na aibu pia. Baadhi ya watu wenye aibu na wenye maarifa mengi vichwani mwao, hutumia muda mwingi kusikiliza na kuzungumza machache. Na kutokana na kuwa natabia hiyo , hujikuta wakizungumza kile kilichomo ndani ya mioyo yao bila kurudia na aghalabu hupenda kujibu kwa mkato. ‘Sitaki’, ‘ndio’, ‘No’ au ‘Ok’ na kadhalika. Inaelezwa kuwa watu wa namna hii huguswa sana na hisia za wenzao na kwasababu hupata muda mwingi wa kusikiliza, hupenda kuwasaidia wenzao na kwa kawaida huwa marafiki wazuri sana.

Lakini pia watu wa namna hiyo mara nyingine hubadilika badilika , wakati mwingine huzungumza kwa sauti na kujiamini na kwakuwa fursa hiyo huipata kwa nadra huitumia vilivyo. Wengine huwa na maamuzi yasiyotarajiwa na huumia sana wanaposalitiwa. Baadhi yao hufanya maamuzi nyuma ya pazia kama kisasi na hujiandaa ‘kwa lolote’ bila woga , bila kutumia kusema maneno mengi. Aibu pia hutumika kama sehemu ya urembo kwa akinadada wanaochipukia, huanza kama mtindo na baadaye hubakia kama sehemu ya tabia. Huitumia kuisoma hali na kufanya maamuzi sahihi. Lakini yaelezwa kuwa aibu ikizidi kupita kiasi huelezwa kuwa ni ugonjwa unaohitaji tiba ya kiakili, ama ya kisaikolojia na ikibidi kupata dozi ya ‘ tembe’.

Posted by BM. on Tuesday, October 18, 2011

Idhaa ya kiswahili ya Redio Japani-NHK imepata mtangazaji mpya Bi. Upendo Kimaro, na alianza kuwa hewani 'Live' kuanzia jana na hii leo J4. Katika siku ya kwanza Mirindimo ilipata picha zake , wakati akisoma habari na baada ya....Take 5 dada U. Unaweza kumsikiliza kwenye mtandao wa NHK-Swahili.


Huuuuuf ....!

Posted by BM. on Tuesday, October 18, 2011

Posted by BM. on Monday, October 17, 2011

Wanajeshi wa Kenya wamevuka mpaka na kuingia Somalia kuwasaka wapiganaji wa kiislamu wa Al-Shabaab, ambao wanawalaumu kwa utekaji nyara wa wageni kadha katika ardhi ya Kenya.

Hii inafuatia na tukio moja ambapow wafanyakazi wawili kutoka Uspania wa Shirika la msaada la kimataifa, walitekwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab siku ya Alkhamisi, na wanawake wengine wawili walitekwa karibu na Lamu, mwambao wa Kenya, na inaaminiwa wamepelekwa Somalia. BBC ilisema kuwa wanajeshi wa Kenya waliingia Somalia Jumapili asubuhi na kwamba wanajeshi hao wa Kenya wakiwa na vifaru wameingia hadi kilomita 90 ndani ya Somalia.

Taarifa kutoka Liboi, kaskazini mwa Kenya,zinabainisha kuwa wanajeshi walionekana wakielekea Somalia.Hatua hiyo inafuata baada ya Waziri wa Usalama wa Kenya, George Saitoti kusema kuwa Kenya itachukua hatua yoyote kudhibiti mipaka na usalama wake, baada ya wanawake wawili wa shirika la msaada la kimataifa, kutekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab-BBC

Posted by BM. on Thursday, October 13, 2011

Mmoja wa viongozi wachache duniani aliyeshika madaraka akiwa na umri mdogo... Mheshimiwa Joseph kabange Kabila. Fuatilia baadhi ya majukumu yake ndani ya nchi yake DRC Kongo na juu hapo ni mke wake ...hongera sana Mr. Presiddent.

Posted by BM. on Wednesday, October 12, 2011

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ukrain Yulia Tymoshenko amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela, baada ya Jaji kumpata na hatia ya kutumia vibaya madaraka alipokubali na kutiliana saini mapatano ya gesi na Urusi mnamo mwaka 2009.

Akitoa hukumu Jaji alisema kua Bibi Tymoshenko ameisababishia Ukraine kupoteza takriban dola milioni mia mbili, na kumuamuru alipe fedha hizo.Ndani ya mahakama iliyofurika Bibi Tymoshenko aliitaja kesi nzima kama maonyesho ya kisiasa na kusema kua atakata rufaa.Akiwa mahakamani Bi Tymoshenko mara kwa mara alimkatiza Jaji aliyekuepo, Rodion Kireyev, wakati akimsomea hukumu, akinadi ''itukuzwe Ukraine'. Pamoja na kifungo cha miaka saba jela alitozwa faini ya takriban dollar mia mbili.

Alituhumiwa kwa kukiuka mamlaka yake kwa kutia saini mapatano ya gesi na Waziri Mkuu wa Urussi Vladmir Putin mnamo mwaka 2009. Ikumbukwe kuwa mapatano hayo ndiyo yaliyokomesha vita vya gesi baina ya nchi hizo mbili.Bibi Tymoshenko aliutaja mchakato mzima wa mahakama kama maonyesho ya kisiasa akiongzea kuwa ni kulipiza kisasi kwa sababu alimpinga Rais Viktor Yanukovich. Kesi hiyo ilifuatiliwa kwa karibu huko Marekani na Ulaya, ambako wana balozi wamekubaliana na madai yake.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameonya kua iwapo Bibi Tymoshenko atahukumiwa basi mahusiano ya Ukraine yanaweza kuathirika. Nje ya jengo la mahakama Kiev ya kati wafuasi wa Bibi Tymoshenko walikusanyika na hofu ilitanda kua wanaweza kuzusha ghasia.(Picha ya chini Tymoshenko wakati akiwa madarakaniakiwa na Waziri Mkuu wa Urussi Vlamir Putin)

Posted by BM. on Tuesday, October 11, 2011

Jana Jumatatu hapa Jijini Tokyo, Japani kulikuwa na sherehe ya kufana katika jengo la Shirika la Utangazaji la Japani -NHK ambapo studio mpya ya kisasa ilifunguliwa.Idhaa ya Kiswahili nayo haikuwa nyuma , tulikuwa na mwanamuziki wa kijapani anayeimba nyimbo za kiafrika Erico Mukoyama , maarufu Anyango. na nyinginezo ambaye aliwaburudisha watu waliopita kushuhudia tukio hilo. fuatilia picha na video inayoeleza kwa muhtasari juu ya tukio hilo...

Posted by BM. on Monday, October 10, 2011

Usifurahie tu mdundo ...fahamu na maneno anayosema pia... haya tuanze sasa: Ipupa anasema; "Lakini tunakwenda kusubiria wapi?
Subiri….”Wako wapi sasa wale waliokuwa wakisema kuwa kitu mapenzi hakipo kabisa, Sasa hayo unaweza kuyaita nini?Kitu gani kimenipata, unaona nimekutana na wewe na moyo wangu ukatingishika!
Nimekua nikiwa mtu mwenye haya nyingi hata wazazi wangu wakitumai kuwa nitakuwa Kasisi siku moja ,wewe umeubadilisha mpango mzima wa maisha yangu,
Lepe zito la mapenzi limenizingira hadi katika nywele kichwani mwangu, unaweza kuwa na wasiwasi juu ya chochote lakini si wasiwasi juu ya mapenzi niliyonayo kwako. Mapenzi yameniweka katika hali ya kustaajabisha , kama vile kuangusha kilio bila ya kupigwa,
Chorus: Ni kwa umbali gani, mapenzi yako yamenisukumuma kwenye kaburi langu, ona nywele zangu za mvi zimeanza kurudia weusi wake tangu ulipoanza kunipenda!
Mtu anaposubiri boti huenda gatini,
Mtu anaposubiri ndege huenda Airport,
mtu anaposubiri treni huenda stesheni ya treni,
lakini pale mtu anaposubiri mapenzi anatakiwa aende wapi?
Si Ulianiambia nisubiri eti kwasababu mapenzi yanasubiwa…kweli!
…Nashangaa kama hilo bunge lililo katika moyo wako tayari limekwishaitisha mkutano kujadili suala letu , wewe Josee Mapwata…”
du shairi limetulia..

Posted by BM. on Monday, October 10, 2011

Sekunde moja iliyopita...Mechi ya Tanzania Taifa Stars imemalizika huko Rabat na Timu ya Tanzania imefungwa kwa tabu magoli 3 kwa moja . Haabari ndiyo hiyo!
Mchezo huo ulikuwa wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Guinea ya Equator na Gabon. Mchezo huo ulifanyika katika kwenye Uwanja wa Marraketch.

Stars ilikuwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D baada ya kujikusanyia pointi tano, iko nyuma ya vinara Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati, zenye pointi nane kila moja na ziko katika nafasi ya kwanza na pili na kwa mechi hii Morroco inapanda kileleni. Stars ilihitaji ushindi wa angalau kuanzia bao 2-0 dhidi ya wenyeji wao Morocco,ndoto ambazo hazikutimia.
Tayari timu za Senegal, Ivory Coast, Botswana na Burkina Faso
zilikuwa zimejihakikishia tiketi ya kucheza fainali hizo za Mataifa ya Afrika, na kuziacha timu zingine zikigombea nafasi 10 zilizobaki.
Pambano hilo la Stars na Morocco lilichezeshwa na waamuzi kutoka Gabon, ambao ni Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, walioteuliwa na CAF wakati Kamishna wa Mchezo ni Zoumaro Gnofame kutoka Togo. Dakika ya mwisho kipa wa Taifa stars alifanya kazi ya ziada kuzuai michomo kuingia langoni vinginevyo yangelikuwa mengii tu. lakini vijana wamejaribu!

Posted by BM. on Sunday, October 09, 2011

Kizazi kipya cha wanamuziki nchini DRC-Kongo... African Diva...Barbara..

Posted by BM. on Sunday, October 09, 2011


Maswariiii!

Posted by BM. on Saturday, October 08, 2011


Posted by BM. on Saturday, October 08, 2011

Leo nilikuwa mitaa ya Kawasaki hapa Japani...nilipata mwaliko maalum wa kutembelea kampuni moja ya magari inayoitwa Phenix. Kilichonivutia kwenda hapo ni kuwepo kwa Mtanzania , huyu ni Mmoja wa Mameneja wasaidizi wa mauzo, Cornel Kibona. Hatua kwa hatua...

Raisi wa Kampuni hiyo anasema kuwa wana matawi zaidi ya 20 ya kuuzia magari nchini Japani, wakiwa na akiba kubwa ya magari. Na sasa wanajiandaa kufungua matawi mengine katika nchi za Zimbabwe, Zambia na Tanzania na wanasema wanachokifanya ni kuweka bei ya chini ya magari yao hasa katika kipindi cha uzinduzi wa biashara...kazi kwako mdau ..lete oda...teh teh tehee!...du!Marafiki tuliokutana nao Phenix..

Kibona ( Aliyepiga suti)katika majukumu-take 5 bro!: