Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, October 27, 2011

Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman ni mmoja kati ya watu wanne muhimu wanaoweza kushika nafasi ya Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.Nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Luis Moreno-Ocampo itakuwa wazi hapo mwakani baada ya Bw Ocampo kumaliza kipindi chake cha utumishi wa miaka tisa mwakani.( Picha ya juu Jaji Othman na ya chini Jaji Ocampo)
Taarifa za UN, Tanzania wagombea wengine ni pamoja na Naibu Mwendesha Mashtaka wa sasa Fatou Bensouda wa Gambia, ambaye wengi wanamwona kuwa analeta ushindani mkali.
Anaungwa mkono na Umoja wa Afrika ambao mara nyingi umemkosoa Moreno-Ocampo kwa kufungua uchunguzi wa mataifa ya Afrika pekee.Katika orodha hiyo pia yupo Andrew Cayley, mwendesha mashtaka mwenza katika mahakama maalum ya Khmer Rouge nchini Cambodia anayetokea Uingereza. Mwingine ni Robert Petit, ambaye ni mshauri kuhusu uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita katika Kitengo cha Mahakama nchini Canada.

Kamati ya iliyoundwa na nchi wanachama wa mahakama hayo awali ilikuwa na orodha ya majina 52 ya wagombea walioomba kupendekezwa katika nafasi hiyo ya juu. Kamati hiyo iliwahoji wanane kabla ya kupata wagombea wanne."Wote wana uzoefu wa kitaaluma na utaalamu na pia wana sifa binafsi muhimu kufanya majukumu ya mwendesha mashtaka katika kiwango cha hali ya juu"
Jaji Othman ameshika nafasi muhimu mbalimbali za uandamizi katika mfumo wa sheria nchini Tanzania na alikuwa mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama maalum ya mauaji ya Rwanda na pia mwendesha mashtaka katika Utawala wa Mpito wa Umoja wa Mataifa katika Timor Mashariki.
Source: BBC

0 comments: