Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, June 29, 2009


Moja ya kazi ya kutukuka ya mwanamuziki Samba Mapangala ni hii Nyama Choma Ukiisiliza presha kama unayo inashuka.......Hebu jidunge nayo roho yako ijiachie , cheza ukitaka...Waooo!!!

Posted by BM. on Monday, June 29, 2009


Nipo na wadau wa kijapani katika mgahawa mmoja Shibuya jijini Tokyo baada ya kula chakula cha kiitaliano...

Posted by BM. on Monday, June 29, 2009


Safari ya Namtumbo, Songea...

Posted by BM. on Monday, June 29, 2009


Raisi ya wa zamani wa Zambia Fredrick Chiluba amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya fedha za umma zinazofikia takriban Paunti za kiingereza laki 5 na ushee kinyume na sheria kati ya mwaka 1991 hadi mwaka 2001 alipokuwa madarakani .Kesi hiyo ilisimama mwaka 2003 kutokana na sababu za kisheria na matatizo ya afya ya raisi huyo mstaafu. Chiluba mwenye miaka 64 alionekana katika Korti ya Lusaka akiwa na majonzi makubwa.Moja ya vizibiti muhimu katika kesi hiyo ni viatu vyake vinavyotajwa kuwa vina thamani kubwa sana .

. Mahakama iliombwa kumruhusu kusikiliza kesi akiwa nyumbani kwake kwanjia ya video lakini ilikataa ikasema lazima akalie mabechi ya mahakama. Mke wake anaonekana picha ya hapo juu akiwa katikati yao hivi sasa anatumikia kifungo baada ya kupatikana na hatia ya ubadhilifu wa fedha.

Posted by BM. on Monday, June 29, 2009


Kifo cha ghafla cha Prof. Haroub Othman, kimewashitua watu wengi nchini baada ya kufariki ghafla asubuhi ya kuamkia jana jumapili akiwa usingizini. Kimewashitua wengi kwa sababu usiku wa kuamkia jana hiyo alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliohudhuria tamasha la filamu na kabla ya hapo alikuwa mgeni rasmi aliyesoma hotuba wakati wa kuzindua kitabu huko huko Zanzibar. Marehemu alikuwa mtetea haki za binadamu na mkosoaji mkubwa wa masuala ya kisiasa, hivyo kifo chake kimeacha maswali mengi kuliko majibu. Wakati akiwa katika Tamasha la filamu, Prof alionekana mwenye afya na mwenye furaha wakati wote, hasa wakati msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akituimbuiza kwenye uzinduzi huo na alionekana akisalimiana na Profesa mwenzie wa Kenya.

Posted by BM. on Sunday, June 28, 2009


Naibu Mufti wa Tanzania , na shekhe mkuu wa Mkoa wa Lindi Allhaji Suleiman Gorogosi amefariki dunia. Chanzo cha taarifa kinasema kuwa Shekhe Gorogosi aliondoka Dar kwa ndege hadi Mtwara ambako alichukua gari akielekea Lindi njiani tairi la gari likapasuka na gari ikapinduka. Kifo kikamchukua. Taarifa zaidi baadaye. Inalillah wainah rajhuun!

Posted by BM. on Saturday, June 27, 2009

Hebu fuatilia darasa hili kwa kisukuma...kama huna muda maelezo hapo chini yanatosha .Massage ni (kukandwa) ni neno linalotokana na neno la kiarabu massa lenye maana mguso. Wakati wa kufanyiwa massage tishu zifuatazo huwa huhusika moja kwa moja klufanyiwa kazi. Muscles, tendons, ligaments, skin, joints, connective tissue na lymphatic vessels.Maasage huweza kufanyika kwa kutumia mikono, vidole,mikono, miguu na kadhalika.La kujiuliza hapa ni kuwa kuna umuhimu gani wa maasage ?Masaage ni njia muhimu ya kitibabu inayohusisha mwili na hisia.Massage huimarisha mfumo wa kinga ya mwili na huwezesha kupumua vizuri.Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na oxygen kwenda kwenye cell zote za mwili na tishu.Inasaidia kuwezesha mwili kutoa uchafu na kuimarisha misuli, huimarisha misuli ya mwili na huifanya “isigangamale” .Hupunguza mkandamizo wa mawazoyaani na kukufanya upate usingizi.Si kila mafuta yanafaa kwa massage , yanayofaa ni ,Sweet almond oil. Apricot kernel oil. Jojoba oil.Fractionated coconut oil,Sunflower oil. Avocado oil, Cocoa butter, Grapeseed oil. Olive oil na Shea butter nk Si vibaya mara moja kwa mwezi ukamwambia yule “unayemmudu” au mwenza mkafanyiana massage ili muimaarishe afya zenu na kuongeza upendo kati yenu. Usitumie nguvu wala kuibana mishipa na misuli , taratibu tu. Na Mikono laini inafaa zaidi au siyo. Tena siku kama ya leo Jumamosi inafaa kwa massage. wiki endi njemaaa!

Posted by BM. on Friday, June 26, 2009

Michael Jackson.Wakati wa utoto wake akiingia kwenye fani. Mwanamuziki Michael Jackson mwenye miaka 50 amefariki dunia huko Los Angeles nchini Marekani.Picha inaonyesha Michael akiwa katika kifaa maalum kumsaidia kupumua katika jitihada za kuokoa maisha yake. Lakini haikusaidia , maisha yake yalifikia tamati.. Jackson alipandwa na BP ya nguvu ,pumzi zikakata na mfanyakazi wake akaita gari la Ambulance lakini hadi anafikishwa hospitalini alikuwa ameshakufa. hapumui na madaktari wamesema kuwa ameshakufa. Nimekuwekea kazi za Jackson za utoto wake ,ujue alikoanzia.

Posted by BM. on Friday, June 26, 2009


Mvua zitaendelea kunyesha, Maji yataendelea kujaa katkati ya jiji la Dar na watu watahitaji kufika ofisi wakiwa wasafi na bila shaka wabebaji watahitajika..Saafi!

Posted by BM. on Friday, June 26, 2009


Kama unataka kumuoa binti huyo mrembo wasiliana na blog hii ili ikupe kontakt..

Posted by BM. on Friday, June 26, 2009


Kilipofika kile kiwango cha kupendana sanaaaa jamaa analala kitanda kimoja na farasi wake...

Posted by BM. on Friday, June 26, 2009

Wezi wanne waliotuhumiwa kuwaibia watu simu na bunduki nchini Somalia wamekatwa mikono ya kulia na miguu ya kushoto mbele ya umati wa watu 200 mjini Mogadishu.Mahakama ya kiislamu inayoendeshwa na wanagambo wa kundi la Shebbab linalotawala sehemu ya Mogadishu liliwahukumu vijana wanne kukatwa miguu yao ya kushoto na mikono ya kulia baada kuwaona wana hatia ya kuwaibia simu na bunduki wakazi wa Mogadishu.Vijana hao walikuwa wakatwe mikono yao ya kulia na miguu ya kushoto siku ya jumatatu lakini kutokana na kwamba siku hiyo kulikuwa na joto sana ilihofiwa kwamba mejaraha ambayo wezi hao wangebakia nayo yangehatarisha maisha yao na hivyo kufanya hukumu hiyo iahirishwe."Hukumu imefanyika kama ilivyopangwa" alisema afisa mmoja wa Shebabb ambaye hakutaka jina lake. "Kwa mujibu wa sheria za kiislamu, mtu yoyote anayewaibia watu huadhibiwa adhabu kama hii" alisema afisa huyo alipokuwa akiongea na shirika la habari la AFP.Wakazi wa kitongoji cha Sukahola walikusanyika kwenye eneo la wazi kushuhudia vijana hao wakiadhibiwa lakini simu na kamera zilikuwa haziruhusiwi eneo hilo.
Wanamgambo wawili wa Shebbab waliokuwa wameficha sura zao waliwakata vijana hao miguu na mikono yao kwa kutumia mabisu makali ya kisomali yanyoitwa "torey"."Kabla hukumu haijatekelezwa, madaktari waliangalia afya zao, tulitaka kuepuka kitu chochote ambacho kingeyaweka maisha yao hatarini" alisema afisa mmoja wa Shebbab.
Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea jinsi wezi hao walivyokuwa wakilia kwa kelele huku wakivuja damu wakati wanamgambo walipokuwa wakiwakata viungo vyao.
"Haikuchukua muda mrefu, ndani ya dakika tatu niliwaona tayari hawana mikono ya kulia na miguu ya kushoto" alisema Ali Mohamed mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyeshuhudia tukio hilo."Baadhi ya watu walishindwa kuwaangalia na kuangalia pembeni wakati hukumu ilipokuwa ikitekelezwa. Ni kweli ni adhabu yenye maumivu makali sana lakini nataka adhabu hii iendelee ili kutokomeza wezi eneo hili" alisema mkazi mwingine wa eneo hilo Farah Mohamed.

Posted by BM. on Wednesday, June 24, 2009


Angalia tu kwa makini...

Posted by BM. on Wednesday, June 24, 2009


Viongozi waandamizi wa Tanzania , wabunge Kutoka Kushoto Andrew Chenge, Bi. Zakhia Meghji na Edward Lowassa.

Posted by BM. on Wednesday, June 24, 2009


Kunapendeza.....

Posted by BM. on Tuesday, June 23, 2009


WAOMBOLEZAJI;Baadhi ya waombolezaji katika mazishi ya Gwizi la muziki wa Taarabu nchini Tanzania Bi. Nasma Khamis Kidogo amefariki jana Jumatatu . Picha juu ni wanamuziki Lady Jaydee , Bi. Shakila na Patricia Hillary .Mazishi yamefanyika jana Jioni katika makaburi ya kisutu, Dar . Bi Nasma Khamis Kidogo alifariki alfajiri ya Jumatatu ya Juni 22 nyumbani kwake eneo la Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.(kwa hisani ya Binti machozi -Lady Jaydee)
Kumbukumbu ya picha ya marehemu Nasma kushoto akiwa na mwimbaji wa taarabu Bi. Khadija Kopa .Marehemu ameacha watoto sita na wajukuu watatu. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, Amin.

Posted by BM. on Saturday, June 20, 2009


jamaa kachoka ...kaamua kupata hapo hapo!

Posted by BM. on Saturday, June 20, 2009


Mitaa ya Shinjuku, Tokyo wakati wa usiku...

Posted by BM. on Saturday, June 20, 2009


Picha imepigwa jana Ijumaa kutoka Carlton center, Johannesburg jengo refu kuliko yote Africa, ikionyesha madhali ya jiji hilo wakati wa usiku...

Posted by BM. on Saturday, June 20, 2009

Kitendo cha kulia na kutoa machozi ni kitu kinachokubalika na tamaduni zote duniani.Unapocheka au kulia mwili huweza kupitia mabadiliko ya kikemia na kifizikia pia kutoa machozi au kucheka vyote vina faida kihisia, kimwili na ki-emotions. Watu wote tunafahamu kwamba kulia (kutoa machozi) huweza kutufanya kujisikia ahueni. Na ndio maana katika misiba inashauriwa kuwa usimkataze mtu kulia kabisa kwani hali hiyo itampa madhara ya kimwili. Wataalamu wanatuambia juu ya aina ya machozi , kwanza kuna Basal Tears:Hii ni aina ya machozi ambayo huwezesha macho yetu kuwa na majimaji kila wakati (lubiricating tears) na kufanya macho yaone vizuri. 2. Reflex Tears:Haya ni machozi ambayo huweza kutoka pale kitu kinachowasha macho kama vile kitunguu, mabomu ya machozi huingia machoni. 3. Emotional Tears; Hii ni aina ya machozi ambayo hutoka kutokana na kuguswa hisia, au tukuto moyoni. Sasa ni machozi yapi huondoa stress? Wanasayansi wamegundua kwamba Emotional tears (aina ya tatu) huwa na kiwango kikubwa cha madini ya manganese na homoni za prolactin ambazo husaidia mliaji kujisikia ahueni baada ya kilio.Ukweli asilimia 85 ya wanawake wanakiri kwamba baada ya kutoa machozi au kulia kujisikia relief na wapo relaxed.Kulia (KUTOA MACHOZI) ni moja ya njia ya asili ya kuondoa stress ikiwa ni pamoja na kucheka, kutembea, kukimbia, kupiga kelele na pamoja na kufanya ishara mbalimbali.
Sasa niliaje?JINSI YA KULIA AU KUTOA MACHOZI; Ukishaona una stress, au umekarisika au umeumizwa au una mawazo na unajisikia kutoa machozi au kulia, tafuta sehemu ambayo ni ya siri na peke yako, sehemu yenye utulivu halafu ruhusu kilio chenye machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye cheeks (mashavu), hakikisha unaruhusu emotions zako za ndani kuhusika katika kulia kwako ili utoe machozi mengi na ya maana (content) kwani ni tiba bora zaidi na utajisikia bora zaidi na pia kujisikia kama umetua mzigo mzito ndani ya mwili wako. Na akinamama hasa tiba hii inawafaa zaidi. Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa Wavulana na wasichana wote hutoa machozi kiwango sawa (au kulia lia) hadi wakifikia miaka 12. Wasichana wakifikisha miaka 18 hulia mara 4 zaidi ya wavulana. Homoni ya prolactin ambayo imo kwenye mammary glands kwa ajili ya kuzalisha maziwa hupatikana pia kwenye damu na glands za machozi. Pia kuna tofauti ya anatomy kwenye glands za machozi kwani mara nyingi mwanamke akitoa machozi huweza kutiririka hadi kwenye cheeks wakati wanaume hata machozi yakitoka bado huishia kwa wao kujifuta bila kutiririka kama wenzao wanawake. Pia wanawake wanapokabiliana na frustration, stress, matatizo binafsi na mabadiliko ya homoni hasa yanayosababishwa na ujauzito, kuwa katika siku zake, menopause hivi vyote huweza kusababisha machozi kutiririka. Na hata kutofikia malengo ambayo kwao wanayaona ni “lazima kuyafikia”. Hebu muelezee mwenza wako linalokusumbua pengine hutalia ama ukilia kidogo tu …sawa. Na kama hulii kabisa hapo sasa unaweza kuushia kujiua kwa jambo dooogo! ...Haya nawe anza basi....!take 5 mdau , Lazaraus M.

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009


Mapambo ya watu wa nchi ya Papua New Guinea mwili mzima unashonwa kama hivyo na nyumbani kwetu Ntwara tunakarabati mapokezi. Mi Mmakonde bwana ....nadumisa mila.
Mama wa kwetu amependezaa ....

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009

...Kimekuwa kipando tena!..

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009

Watu zaidi ya 20 wameuwawa kwenye mlipuko huo katika Hoteli ya Beledweyne, kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.akiwemo Waziri wa Usalama wa ndani wa nchi hiyo Omari Hashi Aden *Pichani mwnye ndevu nyeupe”.Miongoni mwa waliouwawa ni maafisa kadhaa wa Kidiplomasia wa Somalia. Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed amelaumu kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabaab , ambalo pia baadaye lilikiri kufanya shambulio hilo. Kundi hilo linaaminika kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al -Qaeda. Siku ya jumaatano watu 10 walikufa wakati kombora liliporushwa kwenye msikiti mjini Mogadishu. Katika shambulizi la jana Alhamisi , walioshuhudia walisema mlipuaji wa kujitoa muhanga alilipua gari lililojaa mabomu kwenye hoteli ya Medina , mjini Beledweyne, yapata Kilomita 400 kaskazini mwa Mogadishu. Abdulkarim Ibrahim Lakanyo, balozi wa zamani wa Somalia nchini Ethiopia pia ameripotiwa kuwa miongoni mwa waliouwawa. Bw. Aden alihamia mjini Beledweyne hivi majuzi, mji ulioko karibu na mpaka wa Ethiopia, katika jitihada za kukomesha wanamgambo wa Kiislamu wasiendelee kuthibiti maeneo mengi zaidi.
Raisi wa Somalia akiongea na waandishi wa habari mjini Mogadishu juu ya tukio hilo.Picha ya chini hapo ni Mmoja wa wanamgambo wanaoipinga wanaoipinga serikali ya Somalia..

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009

Bunge limepitisha Bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2009/10 baada ya mjadala wa aina yake . Pengine litakalokumbukwa ni vijembe miongoni mwa wabunge bilakujali vyama vyao. Ukiachia kawaida ya wapinzani kuponda bajeti ya CCM hata wabunge wenyewe wa CCM walibadilikiana pia. Mbunge wa Kasulu Magharibi Bw. Kilontsi Mporogomyi, (CCM) amesema kuwa “Kazi yetu umu ndani ya Bunge si kuisifia tu Serikali,mama yako masikini, wapiga kura wako masikini, unasifu nini, ninyi wabunge acheni utani hapa bwana, hata kule Marekani Bunge linaishauri na kuikosoa Serikali,”alisisitiza
Bw. Mporogomyi akionesha kukasirika. Alisema matatizo mengi yanayowakabili Watanzania sasa yanatokana na utendaji mbovu wa waliopewa madaraka serikalini na kuwasababishia maisha magumu Watanzania huku akitolea mfano mkataba tete ya TICTS unaoinyima nchi mapato. “Hivi sasa nchi zote zilizokuwa zinatumia bandari yetu zimehama wanatumia nchi. jirani, ni aibu leo hii tunazungumzia bandari, hakuna anayejua kiasi gani cha mafuta kinaingizwa nchini, ile mashine ukifika unaweza kuambiwa ni feki, hapana ni nzima imeharibiwa kwa makusudi kwa manufaa ya wachache!”alidai mbunge huyo. Katika mchango wake Mbunge wa Singida Kaskazini Bw. Lazaro Nyalandu, (CCM)aliwapasha wabunge wenzake kwamba si vizuri kulalamika kwa kuwa kuna maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini. “Kuna progress kubwa sana, Serikali imefanya mambo mengi sana,”

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009


Binaadamu kila kukicha anataka kufanya kitu kipya ambacho pengine kilikuwa hakijafanyika. Wataalamu wa Shirika la anga za Juu NASA wanakiri kwamba si rahisi kufanya mapenzi huko kwenye space.Tatizo kubwa ni ila hali ya kutokuwa na force of gravity kwa maana kwamba wapenzi hawawezi kushikana na kufanikisha tukio hilo kwani kila mmoja huelea kivyake (zero gravity)
Kumekuwa na maswali kutoka kwa watu wengi wanaouliza kama wanaweza kutembelea International Space Station pamoja a wapenzi wao na kufanikiwa jambo hilo ili hatimaye kujiweka kwenye kitabu cha kumbukumbu cha matukio makubwa duniani kiitwachoGuinness.Kuna mwanaanga mmoja Richard Branson anapanga kupeleka watalii zaidi huko pia zaidi ya watu kuomba wawe wa kwanza kufanya mapenzi huko bado wapo waaoomba kwenda kufanya movie.
Wataalamu wanadhani kwamba ili watu waweze kufanya mapenzi kuna ulazima wa kutengeneza kifaa mfano wa shuttle (basi) ambalo ndani yake wataweka vifaa maalumu kuwawezesha wapenzi kufanikisha ufanyaji wa mapenzi (love handles)
Kufanya mapenzi bila nguvu ya uvutano (zero gravity) hakuna uzuri wowote kwani inaweza kusababisha kuchefuchefu kwa wahusika, na pia hatari kubwa ni kwamba watu wakiwa Space Station hujisikia kupata low blood pressure na ni wazi kuwa low blood pressure hupelekea damu kutozunguka sehemu zote za mwili na damu kutozunguka sehemu zote za mwili maana yake ile kitu haiwezi kusimama na hata kama ikisimama si kwa muda

Posted by BM. on Thursday, June 18, 2009


Raisi Barack Obama akiwa ameketi katika ngazi za ubalozi wa Marekani ulioko Paris nchini Ufaransa , huku wasaidizi wake wakimzunguka. Kijua kilimvutia. Ikulu ya Ufaransa walilishangaa tukio hilo. inapendeza!.

Posted by BM. on Thursday, June 18, 2009

Ubunifu wa watu wa India , hakuna kutupa kitu..


Hii imekaaje?

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


DAR,Mlimani city ..leo mchana..

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Kijijini Chambucha ,Kivu ya kaskazini huko DRC , wanamgambo wa Mayimayi wamejichukulia jukumu la "Kulinda raia" wakidai majeshi ya UN na ya Serikali ya Kongo hayapo hapo ..imejin...

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Miaka 17 iliyopita , Toshikazu Sugaya akiwa na miaka 45 wakati huo alikamatwa na Polisi akituhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto mdogo wa miaka minne, mwaka 1990 wakati huo akiwa anafanya kazi wa kuendesha basi la shule. Amekaa jela kizuizini miaka 17 na mwanzoni mwa mwezi huu Polisi walikiri kuwa kwa kutumia utambuzi wa vinasaba yaani DNA mtu huyo hakuhusika na mauaji hayo na ikaamua kuwa aachiliwe na Mahakama kuu ya Tokyo inatarajiwa kuidhinisha uamuzi huo wiki ijayo.
Mtu huyo amekuwa akionana na waandishi wa habari kuelezea yaliyomkuta na Jana jumatano alikutana na RPC wa Tochigi hapa Japani , Shoichiro Ishikawa ambaye alimuomba radhi na wakati wote huo wakili wake alikuwa akihaha kuthibitisha kuwa hakuhusika kabisa.
“Naomba radhi kutoka ndani ya moyo wangu kwa kukuweka katika hali ngumu kiasi hicho kwa kipindi kirefu”, alisikika Ishikawa akimwambia Toshikazu Sugaya ambaye sasa ana umri wa miaka 62 aliyekuwa akilengwa lengwa na machozi katika makao makuu ya polisi mkoa. Mwendesha mashitaka mwandamizi naye alionyesha masikitiko yake , majuto na kuomba msamaha jambo si maneno ya moja kwa moja.
Kama zilivyo tamaduni za kijapani Sugaya aliinamisha kichwa mara mbili wakati akikubali kusamehe yaliyotokea na baadaye aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri kuwa “ nimewasamehe tangu pale nilipowaona kwa dhati kabisa wakiniomba radhi na kwamba msamaha wake pia unawahusu wapelelezi na waendesha mashitaka “.Wakati huo huo Meya wa jiji la Ashikaga Minoru Omamiuda anaangalia uwezekano wa kujitolea kumpa makazi kama atapenda kuishi hapo. Inaonyesha kiwango cha uadilifu katika upelelezi, uendeshaji mashitaka na utu...Tuige basi kama tunaweza.

Kwetu Bongo inawezekana?

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Miss Tanzania 2007 Richa Adhia na mama yake Bi. Maria hivi karibuni jijini Dar.

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Umeelewa?

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Wanenguaji wa Twanga pepeta wakiwa mzigoni..hatumwi mtoto hapo..

Posted by BM. on Wednesday, June 17, 2009


Usikilizaji wa muziki huweza kuwasaidia wagonjwa walio na matatizo sugu ya mkandamizo wa mawazo (stress) na tiba ya kiwango fulani kwa maradhi ya moyo pale mishipa ya moyo inapoelekea kuziba. Utafiti wa kitiba uliofanyika nchini Marekani umebaini kuwa kusikiliza muziki uliotulia unaweza kupunguza ongezeko la msukumo mkubwa wa damu na kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wa moyo.
Wataalamu hao wanasema kuwa kuishi huku ukiwa na matatizo ya moyo ni jambo linalosumbua sana kwahiyo hali hiyo inahitaji tiba mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri wa matumzi ya vyakula, vinywaji , lakini pia kuufanya ubongo usipate mkandamizo bila sababu.
Lakini hata hivyo Dr. Joke Bradt wa kituo cha sanaa na ubora wa maisha katika kituo cha utafiti wa kitiba katika Chuo Kikuu huko Philadelphia nchini Marekani anasema ‘majaribio yaliyokwisha fanyika ni machache na hasa aina ya muziki unaofaa ni kwamba usikilizwe kwa muda gani na kwamba bado wanalifanyia kazi suala hilo. Tafiti zilizokwisha fanyika ni 23 kwa wagonjwa 1,461 kwa kuwapatia muziki maalum uliorekodiwa na kuungwa katika mishipa , na kazi hiyo hufanywa na wataalamu mabingwa wa masuala ya maradhi ya moyo na sanaa.
Tayari wanamuziki duniani kila mtu anakuna kichwa kufikiria kitu gani atunge na kukiweka katika muziki mororo ili uteuliwe kuwa ‘dawa’ na bila shaka atakuwa billionea ghafla. Penda kusikiliza muziki laini unapojikuta umetindikiwa na mawazo kibao…

Posted by BM. on Tuesday, June 16, 2009


Kumbukumbu muhimu ya uanzishaji wa makumbusho ya kabila la wasukuma Bujora, Mwanza .

Posted by BM. on Tuesday, June 16, 2009


Kuna jambo kubwa sana limefanyika huko Mwanza miaka kadhaa iliyopita ya kuanzisha kituo cha utamaduni na kumbukumbu ya kabila la wasukuma kule Bujora. Hapo kumbukumbu ya kabila hilo zinahifadhiwa ambapo wageni wa ndani na nje hufika kujionea. Miaka kadhaa ijayo mambo haya yanaweza kupotea bila kujua. Weye unakotoka kuna kitu kama hiki.; kalagabaho!
Int.Pz. Peter Omari alifika hapo majuzi tu.

Posted by BM. on Tuesday, June 16, 2009


Nyumba ya kiasili ya kisukuma..

Posted by BM. on Tuesday, June 16, 2009


Moja ya kumbukumbu muhimu ...usukumani.

Posted by BM. on Tuesday, June 16, 2009


Mdau Peter Omari akiwa juu ya kiti cha enzi cha wafalme wa kisukuma.