Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, June 19, 2009

Bunge limepitisha Bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2009/10 baada ya mjadala wa aina yake . Pengine litakalokumbukwa ni vijembe miongoni mwa wabunge bilakujali vyama vyao. Ukiachia kawaida ya wapinzani kuponda bajeti ya CCM hata wabunge wenyewe wa CCM walibadilikiana pia. Mbunge wa Kasulu Magharibi Bw. Kilontsi Mporogomyi, (CCM) amesema kuwa “Kazi yetu umu ndani ya Bunge si kuisifia tu Serikali,mama yako masikini, wapiga kura wako masikini, unasifu nini, ninyi wabunge acheni utani hapa bwana, hata kule Marekani Bunge linaishauri na kuikosoa Serikali,”alisisitiza
Bw. Mporogomyi akionesha kukasirika. Alisema matatizo mengi yanayowakabili Watanzania sasa yanatokana na utendaji mbovu wa waliopewa madaraka serikalini na kuwasababishia maisha magumu Watanzania huku akitolea mfano mkataba tete ya TICTS unaoinyima nchi mapato. “Hivi sasa nchi zote zilizokuwa zinatumia bandari yetu zimehama wanatumia nchi. jirani, ni aibu leo hii tunazungumzia bandari, hakuna anayejua kiasi gani cha mafuta kinaingizwa nchini, ile mashine ukifika unaweza kuambiwa ni feki, hapana ni nzima imeharibiwa kwa makusudi kwa manufaa ya wachache!”alidai mbunge huyo. Katika mchango wake Mbunge wa Singida Kaskazini Bw. Lazaro Nyalandu, (CCM)aliwapasha wabunge wenzake kwamba si vizuri kulalamika kwa kuwa kuna maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini. “Kuna progress kubwa sana, Serikali imefanya mambo mengi sana,”

0 comments: