Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, July 31, 2009


Washabiki wa Mirindimo...Baada ya mapumziko ya takriban mwezi Mzima Nyumbani Tanzania nimerejea Tokyo nikiwa na afya njema ...habari na picha za kutosha . Kuanzia Kesho J1 naahidi kuanza kupachika baadhi ya picha za Bongo..Sore kwa kuwa kimya lakini mambo yatatengemaa. Take 5 ..karibu. Hapo Osaka jana nikiwa njiani kuja hapa Tokyo..

Posted by BM. on Friday, July 31, 2009

Mipasho ya bongo...umeelewa?

Posted by BM. on Friday, July 31, 2009


Siku Moja kabla ya kurejea kibaruani..Jijini Morogoro..

Posted by BM. on Tuesday, July 14, 2009

Niko mapumziko jijini
Dar es salaam na safari ilikuwa nzuri na bila shaka mirinimo inakukusanyia matukio ya Bongo...Kila la kheri!

Posted by BM. on Tuesday, July 14, 2009

Safari ya Uwanja wa Ndege....du sijui nimechelewa ane.wey

Posted by BM. on Tuesday, July 14, 2009

Haneda Airport..Japani...

Posted by BM. on Tuesday, July 14, 2009

Kunako chombo safari ya Bongo..
Njia Moja na Afande wangu

Posted by BM. on Tuesday, July 14, 2009Kaburi la baba Mzee Rajabu Msulwa...Mapumziko yalianzia hapa Mtoto kwa mama hakui..
Na Raja jijini Moro...

Posted by BM. on Thursday, July 02, 2009


Maskofu wa kanisa Katoliki walioamua kuachana na useja wakipozi na wake zao mbele ya altare huko Nairobi nchini Kenya.Kushoto Askofu Emanuel Millingo wa Zambia na mkewe Bi. Maria Sung na Katikati Askofu Daniel Kasomo na waifu wake Maryanne akiwa kulia . Wachungaji wa kondoo wameamua mwelekeo mpya ..

Posted by BM. on Thursday, July 02, 2009


Usajili wa simu za mkononi linaanza leo nchini Tanzania.Zoezi hilo liliazimiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [|TCRA] ili kuondoa kero zote zinazohusiana na zinazotokana na simu hizo za mkononi nchini.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, John Nkoma amesema kuwa zoezi hilo litaanza leo Julai Mosi, la kusajili kadi za simu za mkononi kwa wananchi.Amesema kuwa lengo la kusajili kadi hizo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu yanayofanywa na wananchi vilevile ikiwemo na kupunguza wimbi la simu hizo ili kulinda maslahi ya mtumiaji.Amesema ili kudhibiti matumizi mabaya ya simu sasa kila mwenye simu ya mkononi lazima ajiandikishe.Amesema kila mwenye simu ya mkononi ni lazima ajiandikishe kwa kutumia vitambulisho maalumu vya kupigia kura, Passport ya kusafiria, kitambulisho cha mfuko wa pensheni, leseni za udereva.Pia kwa wenye vitambulisho vya Saccos, Benki, ajira, kitambulisho cha chuo cha elimu ya juu, barua ya mwajiri na kama hivyo vyote hana unatakiwa uwe na barua ya serikali za mitaaa.Amesema zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miezi sita na lengo la kusajili kadi hizo wananchi watakuja kutambua faida yake kwa wale ambao wanaona ni haisaidii.Amesema kuwa wananchi wamekuwa wakitukanana kwa maneno mabovu kwa kununua namba na kuitupa pia kupeana maneno ya kutishana na kumekuwa kumeshamiri sana wizi wa simu hizo.Amesema namba ya kadi ikishasajiliwa basi hata kama mtu akiiba simu hiyo hataweza kuitumia na matokeo yake ataitupa.

Posted by BM. on Thursday, July 02, 2009


Mu-Israel Yitzhak Yazdantana akiwa na tango kuubwa alilolilima shambani kwake karibu na Tel Aviv anataka kutambuliwa na kitabu cha kuvunja rekodi dunianikubwa ndilo tango kubwa kuliko yote yaliyopata kutokea duniani. Du Hivi huko Matombo hakuna kitu kama hii tuwaonyeshe...

Posted by BM. on Thursday, July 02, 2009


Ukumbi wa Mkutano -Ikulu ya Marekani...