Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, November 30, 2009


Mama Salma Kikwete katika majukumu yake ya kawaida ya kuwasaidia akinamama wa Tanzania. Taswira inayopendeza au siyo!

Posted by BM. on Monday, November 30, 2009

Mh. John Pombe Magufuli akitunukiwa shahada yake ya uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Balozi Fulgence Kazaura baada ya kukamilisha nondo zake katika fani ya sayansi ya kemia . Du hapo nakubali.
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye fani ya kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.
Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Fulgence Kazaura akiwa mmoja wa wanafunzi 19 wa shahada hiyo. Mbali na hao katika mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo wanafunzi wengine 4,331 walitunukiwa vyeti, stashahada na shahada mbalimbali. Picha hiyo inamuonyesha mama mazazi wa Dr. Magufuli akiwa na mwanawe katika hafla hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akitambuliwa kama Dr. Magufuli alisema kuwa baada ya kufanya utafiti huo, maganda ya korosho badala ya kutupwa kama zamani kwa kuonekana kama takataka sasa yatatumika katika kuzuia kutu. Alisema kuwa kutu ni tatizo linalokumba dunia na kuongeza kuwa nchi ya Marekani huingia gharama za dola milioni 100 kwa ajili ya kuzuia kutu. Eeh kweli penye nia pana njia , hongera Dr.PJM.(habari/picha -Daily News)

Posted by BM. on Saturday, November 28, 2009

Kuna aina takriban saba za upishi wa pilau. Kwasasa angalia hizo ; umegundua tofauti yake?

Posted by BM. on Friday, November 27, 2009


Waislamu takriban kote duniani kesho Jumamosi watasherehekea sikukuu ya Eid el Hajj, baada ya kumalizika kwa ibada ya Hijja huko Mecca. Mamilioni ya mahujaji walimiminika katika Mlima Arafa kukamilisha sehemu ya mwisho ya Hija ambayo ni nguzo ya tano ya dini ya Kiislamu. Wakati Waislamu wengi wanasherehekea siku kuu ya Eid leo , kwa wengine ni hapo kesho. Taarifa Kutoka Tanzania kutoka kwa Kaimu Mufti wa Tanzania, Shekhe Ismail Habib imesema kuwa swala na Baraza la Idd Kitaifa zitafanyika katika msikiti wa Al Farouq uliopo Makao Makuu ya Bakwata, Kinondoni, Dar es Salaam. Wakati huo huo , Zaidi ya mahujaji millioni mbili wamewasili katika nyanda za Arafat katika siku ya pili ya ibada ya Hijjah huku mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na dhoruba kali ikinyesha mwanzoni mwa ibada hii takatifu siku ya Jumanne na kusababisha uharibifu katika maeneo matakatifu na vifo kadhaa kuripotiwa. Hatahivyo hali ya hewa inaonekana kutulia na mamilioni ya mahujaji wamekusanyika katika nyanda za Arafat. Kwa mahujaji wengi huu ni wakati wa msisimko mkubwa unaozingatiwa kuwa ni kilele cha hijjah takatifu. Hapa ndipo mtume Muhammad(SAW) alisimama karne 14 zilizopita na kutoa hotuba yake ya mwisho.Tangu wakati huo kila mwaka waislamu wamekuwa wakikusanyika hapo kusali na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu.
Mirindimo inawatakia Sikukuu Njema , Eid Mubarak!

Posted by BM. on Friday, November 27, 2009

Ze comedy!

Posted by BM. on Thursday, November 26, 2009


Saa kumi na moja kasorobo tu giza limefunga !

Posted by BM. on Thursday, November 26, 2009


A team of scientists has discovered a new species of chameleon in Tanzania. Dr Andrew Marshall, from the Environment Department at the University of York, first spotted the animal while surveying monkeys
Vinyonga wapya wagunduliwa TanzaniaMwanasayansi mmoja wa Uingereza aliyekuwa akifanya utafiti wa viumbe hai katika msitu wa Magombera huko Tanzania ametangazwa rasmi kugundua aina mpya ya vinyonga ambao hawapatikani sehemu nyingine duniani isipokuwa Tanzania.
Dr Andrew Marshall kutoka chuo kikuu cha York nchini Uingereza alimgundua mnyama huyo ambaye hatimaye alipewa jina la ni Kinyongia magomberae, miaka minne iliyopita, lakini sasa ndiyo amethibitishwa rasmi na wataalam wenzie. Dr Andrew Marshall, mwanaikolojia kutoka chuo kikuu cha York, amesema kuwa alikuwa akifanya utafiti wa mbega wekundu, ndipo siku moja alipokumbana na nyoka ambaye alishtuka na kumtema kinyonga huyo miguuni mwake na kukimbia. Ingawa mwenzake alimshauri asimguse kutokana na wasi wasi wa kuathirika na sumu ya nyoka, Dr Marshall alihisi kiumbe huyo alikuwa mpya machoni mwa wanasayansi akampiga picha na kuwatumia wenzake ambao walithibitisha aliyokuwa akifikiria. Kinyongia magomberae, ikiwa na maana ya "kinyonga wa Magombera", ni matokeo ya mkasa huo na akaieleza BBC kwamba haikuwa rahisi kwake kumtambua ndiyo maana akavutiwa kumchunguza. "Unajua, rangi si kigezo kizuri kuwatofautisha vinyonga, kwasababu wanabadilika rangi kutokana na mazingira. Kwa kawaida hutambuliwa kutokana na maumbile ya vichwa vyao, na mpangilio wa magamba. Kwa tukio hili ilikuwa ni magamba yaliyotuna juu ya pua yake." Kwa bahati njema, Dr Marshall alifanikiwa kumwona kinyonga wa pili akiwa hai na alifanikiwa kumpiga picha. Viumbe hao walipatikana umbali wa kilometa 10 kutoka kila mmoja, jambo linalomfanya aamini inaweza kuwa umbali halisi wa eneo linalokaliwa na Kinyongia magomberae. Ingawa aliwagundua viumbe hao mwaka 2005, nyaraka zake za utafiti zilizochapishwa Novemba 2009, zinatambulisha rasmi uvumbuzi huo. "Inachukua muda mrefu kuzishawishi mamlaka kuwa umevumbua aina mpya ya viumbe," alieleza."Tulipowasilisha matokeo ya ufafiti wetu kwa wanakijiji wa eneo hilo walifurahishwa kwamba dunia sasa inatambua mnyama huyo kwa jina la kienyeji Magombera," alisema. Magombera ni msitu wa asili ulioko eneo la hifadhi ya Udzungwa mpakani mwa mikoa ya Morogoro na Iringa

Posted by BM. on Thursday, November 26, 2009

Kingston;...

President Jakaya Kikwete greeting Jamaican Prime Minister Bruce Golding after the former touched down at the Norman Manley airport in Kingston yesterday.

The Jamaican Prime Minister greeting the Tanzanian ambassador to Jamaica Dr Joram Biswalo.

President Jakaya Kikwete and his wife looking at a cassava called Jamaica sweet when they visited the St Catherin agriculture and livestock research center in the second day of his visit in Jamaica. On the right side of the president is Ms Clandette McKenzie, the director of crops research at the center and the first right is the Jamaica minister of agriculture and fishing Jamaica Dr Christopher Tufton

President Jakaya Kikwete and his wife, Salma Kikwete and Minister for Tourism in Jamaica, Mr Edmund Bartlett (right) and Chairman of the Mystic mountains conservation, Mr Horace Clarke, touring the hills facing the tourist attractions in St. Ann region, in Jamaica.
Kikwete calls for tourism sector revamp
PRESIDENT Jakaya kikwete has said Tanzania's tourism sector was underperforming compared to the natural heritage the country is endowed with and called for radical measures to revamp the industry.Speaking after exploring natural and created attractions at Jamaica's Ocho Rios tourist hub in St. Ann region today, the president envied achievements registered by the Caribbean country. "You have done very well in this area. We will be interested to learn how you do it," he told Jamaica tourism minister Edmund Bartlett, who accompanied him on the tour. Jamaica, which has 2.8 million inhabitants, receives some 2.6 million tourists annually mainly from the US, Canada and some European countries while Tanzania, with its abundant wildlife and other attractions, is still struggling to achieve the one million visitors mark. Officials here say their hotels have 65 per cent occupancy rate with each visitor spending an average nine days. Tanzania is talking about 53 per cent hotel occupancy while visitors stay for six to seven days. Tourism and other services account for more than 60 per cent of Jamaica's economy. President Kikwete attributed Tanzania's dismal earnings from tourism to poor infrastructure and service quality. Local tourism promoters will need to improve product branding and blend wildlife safaris and beach tourism with historical and cultural attractions. "Our hoteliers should also learn better ways of attracting and retaining visitors," he added. Earlier today, Mr kikwete, who was on the second day of his state visit here, called on the Governor-General, Sir Patrick Allen, at the King's House.
He later inspected agricultural and livestock research at Bodles Research Station in St Catherine Region, where he called for cooperation between the Jamaican station and Tanzanian research institutes. President Kikwete is tomorrow scheduled to hold bilateral talks with Prime Minister Bruce Golding and address a joint session of the Houses of Parliament. Picha na habari/Daily news

Jamaa akiwa katika mgongo wa Dolphin akimuonyesha JK ni kwavipi wanyama hao wanaweza kukwamua uchumi wa nchi wkifundishwa na kufundishika...

Posted by BM. on Wednesday, November 25, 2009

Niwakumbushe watazamaji wa MIRINDIMO mbinu za kampeni za Raisi Kabila zilizomfanya apate ushindi mkubwa katika mbio za kuwania uraisi nchini DRC mwaka 2006. Alikuwa karibu na wanamuziki wenye majina nchini humo. Hebu fuatilia muziki wa mwanamuziki Mbilia bel utajua maana yake! namkubali huyu mdada , we unasemaje!

Posted by BM. on Monday, November 23, 2009

Mtoto mmoja wa Kijapani mwenye miaka miwili hivi ana kipaji cha ajabu sana cha kupiga kifaa cha muziki kwa kuzingatia mapigo ya vyombo vingine ...tabiri ukubwani atafikia kiwango gani...changamoto kwa wazazi kutambua vipaji vya watoto wao au sivyo!
Mdau Jonas Songora akila pozz na mtoto huyu mwenye kipaji cha ajabu.

Mtoto akipiga chombo hicho cha muziki bila tabu!

Posted by BM. on Monday, November 23, 2009


Tyson na familia yake mitaani...

Posted by BM. on Monday, November 16, 2009


huna haja ya kusema niko bafuni tutajua tu...

Posted by BM. on Monday, November 16, 2009


Kutokana na migogoro isiyokwisha kati ya wenza katika baadhi ya familia na kuhatarisha maisha ..ubunifu unahitajika kwa mafundi wa kutengeneza fenicha. Dawa hapo ni hiyo tu ...au unasemaje!

Posted by BM. on Monday, November 16, 2009

Raisi Barack Obama wa Marekani anaendelea na ziara yake barani Asia. sasa yuko Singapore kabla hajaelekea China. Ilikuwaje alipokuwa hapa Japani..!
Mkutano wa Bw. Obama na Bw. Hatoyama , Waziri Mkuu wa Japani. Kilichonifurahisha hapo ni kuwa waziri Mkuu wa JP muda wote alikuwa akizungumza kijapani kwa ajili ya watu wake Millioni 128. Afrika sijui inakuaje pale viongozi wa nje wanapokuja ..na hata wanapotembelea vijiji..!

Wakubwa wanapokutana. Marekani na Japani ni mataifa yanayoongoza duniani kwa kuwa na chumi kubwa. Katika meza kama hiyo ni kama wenye dunia yao ya kiuchumi wanapokutana.

Pale Raisi Obama alipokwenda kwenye kasri la kifalme kumuona Mfalme Akihito na Malkia Michiko wa Japani. Kwa wajapani hawa ni watu wenye hadhi kubwa kuliko maelezo. Historia inaonyesha kuwa zamaani walikuwa wakiabudiwa kama miungu ya wajapani. Sasa mambo yamebadilika kidogo.Na kwa kukudokeza tu Wajapani huwa hawataji jina lake hadharani na hata kuliandika katika maandishi rasmi huishia tu..mtukufu Mfalme! ni tamaduni na mila za Wajapani!

Posted by BM. on Tuesday, November 10, 2009

Labda hili!
Kijana mmoja aliyekuwa anatafuta kazi alifanikiwa kupata kazi katika zoo ya wanyama. Kijana huyo ilimbidi afanye hiyo kazi japo ni ngumu lakini alikuwa hana jinsi. Kazi hiyo ilimtaka kijana huyo kuvaa ngozi ya sokwe na kurukaruka kwenye banda la sokwe ambae alifariki ghafla, kwa kuwa watalii wengi walimpenda huyo sokwe, ilibidi mmiliki wa zoo amfundishe huyo kijana staili zote ambazo Yule sokwe alikuwa akiruka. Kijana alifanikiwa mbinu hizo na kuanza kazi mara moja huku watalii wakimiminika kuona sokwe wao karudi. Siku moja kijana huyo katika kurukaruka kwake kwa sifa alijikuta amedondoka kwenye banda la simba. Simba huyo alimkimbilia huyo kijana na kumuinamia huku watalii wakishangaa kuona nini kitatokea. Kijana alianua mdomo kwa kutaka kupiga kelele mana alishaona maisha yake yako hatarini lakini cha ajabu alisikia simba akimnong'oneza ''Acha kelele tutafukuzwa kazi''Kumbe ..

Posted by BM. on Saturday, November 07, 2009


Unasemaje hapo

Posted by BM. on Saturday, November 07, 2009


Ugunduzi wa eneo jipya la kuchorea tatoos. Wasasa mnaweza kuendelea!

Posted by BM. on Saturday, November 07, 2009


Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamadi, Ikulu Mjini Zanzibar . Kulia ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Ismail Jusa.Bw. Shariff alikwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Raisi Karume Ikulu. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu)

Posted by BM. on Thursday, November 05, 2009


KIKAO CHA VIONGOZI WA Jumuia ya TANZANITE-JP.
Viongozi wa juu na wana kamati za Jumuiya ya watanzania wanaoishi nchini Japani (Tanzanite Society) wanatarajia kukutana Jumapili ya tarehe 8/11 katika ukumbi wa Odasaga Plaza uliopo karibu na kituo cha reli cha odakyu Sagamihara kuanzia saa 12 jioni. Baadhi ya ajenda ya kikao hiko ni kupitia na kuweka sahihi fomu za kuomba kusajiliwa kwa jumuiya kuwa NPO. Zoezi hili ambalo litasimamiwa na Mwanasheria Kijima ni hatua ya mwisho katika taratibu za usajili.Baada ya zoezi hili fomu hizi zitawasilishwa rasmi kwenye ofisi za Mkoa wa wa Tokyo.
Ajenda zingine katika mkutano huo itakuwa ni kutathmini zoezi la ulipaji wa michango ya mwezi na kuandaa ajenda za mkutano wa wanachama wote utakaofanyika tarehe 6 mwezi 12.Viongozi wote wanaombwa kufika kwenye kikao kwa wakati unaotakiwa.

Uongozi
Tanzanite Society.

Posted by BM. on Sunday, November 01, 2009

Sichemi!
Nyavu za Yanga zilitikishwa katika dakika ya 25 na Mussa Hassan Mgosi, na kuufanya mwanzo kuwa mbaya kwa Kocha mpya wa Yanga Kostadin Papic baada ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa jana Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa wa Uhuru .
Mgosi alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa krosi safi ya Danny Mrwanda kutoka wingi ya kulia aliyopiga baada ya kumpiga chenga beki Amir Maftah wa Yanga.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, Yanga ilijitahidi kucheza kufa na kupona lakini jitihada za washambuliaji Boniface Ambani, Mrisho Ngassa na Kiggi Makassy hazikuweza kusaidia kupata bao la kusawazisha hadi timu zinakwenda mapumziko.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini haikuweza kubadili matokeo ya awali licha ya Yanga kuwatoa Ambani, Makassy na Abdi Kasima na kuwaingiza, Jerry Tegete, Moses Odhiambo na Mike Barasa.Simba sasa imefikisha pointi 30 na kuendelea kujichimbia kileleni huku Yanga ikiwa ya pili na pointi 18 ilizopata katika michezo 10 iliyocheza ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, haya fungua ukurasa mwingine.