Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, November 27, 2009


Waislamu takriban kote duniani kesho Jumamosi watasherehekea sikukuu ya Eid el Hajj, baada ya kumalizika kwa ibada ya Hijja huko Mecca. Mamilioni ya mahujaji walimiminika katika Mlima Arafa kukamilisha sehemu ya mwisho ya Hija ambayo ni nguzo ya tano ya dini ya Kiislamu. Wakati Waislamu wengi wanasherehekea siku kuu ya Eid leo , kwa wengine ni hapo kesho. Taarifa Kutoka Tanzania kutoka kwa Kaimu Mufti wa Tanzania, Shekhe Ismail Habib imesema kuwa swala na Baraza la Idd Kitaifa zitafanyika katika msikiti wa Al Farouq uliopo Makao Makuu ya Bakwata, Kinondoni, Dar es Salaam. Wakati huo huo , Zaidi ya mahujaji millioni mbili wamewasili katika nyanda za Arafat katika siku ya pili ya ibada ya Hijjah huku mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na dhoruba kali ikinyesha mwanzoni mwa ibada hii takatifu siku ya Jumanne na kusababisha uharibifu katika maeneo matakatifu na vifo kadhaa kuripotiwa. Hatahivyo hali ya hewa inaonekana kutulia na mamilioni ya mahujaji wamekusanyika katika nyanda za Arafat. Kwa mahujaji wengi huu ni wakati wa msisimko mkubwa unaozingatiwa kuwa ni kilele cha hijjah takatifu. Hapa ndipo mtume Muhammad(SAW) alisimama karne 14 zilizopita na kutoa hotuba yake ya mwisho.Tangu wakati huo kila mwaka waislamu wamekuwa wakikusanyika hapo kusali na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu.
Mirindimo inawatakia Sikukuu Njema , Eid Mubarak!

1 comments:

mumyhery said...

Shukran na wewe pia