Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, November 01, 2009

Sichemi!
Nyavu za Yanga zilitikishwa katika dakika ya 25 na Mussa Hassan Mgosi, na kuufanya mwanzo kuwa mbaya kwa Kocha mpya wa Yanga Kostadin Papic baada ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa jana Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa wa Uhuru .
Mgosi alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa krosi safi ya Danny Mrwanda kutoka wingi ya kulia aliyopiga baada ya kumpiga chenga beki Amir Maftah wa Yanga.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, Yanga ilijitahidi kucheza kufa na kupona lakini jitihada za washambuliaji Boniface Ambani, Mrisho Ngassa na Kiggi Makassy hazikuweza kusaidia kupata bao la kusawazisha hadi timu zinakwenda mapumziko.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini haikuweza kubadili matokeo ya awali licha ya Yanga kuwatoa Ambani, Makassy na Abdi Kasima na kuwaingiza, Jerry Tegete, Moses Odhiambo na Mike Barasa.Simba sasa imefikisha pointi 30 na kuendelea kujichimbia kileleni huku Yanga ikiwa ya pili na pointi 18 ilizopata katika michezo 10 iliyocheza ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, haya fungua ukurasa mwingine.

0 comments: