Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, November 16, 2009

Raisi Barack Obama wa Marekani anaendelea na ziara yake barani Asia. sasa yuko Singapore kabla hajaelekea China. Ilikuwaje alipokuwa hapa Japani..!
Mkutano wa Bw. Obama na Bw. Hatoyama , Waziri Mkuu wa Japani. Kilichonifurahisha hapo ni kuwa waziri Mkuu wa JP muda wote alikuwa akizungumza kijapani kwa ajili ya watu wake Millioni 128. Afrika sijui inakuaje pale viongozi wa nje wanapokuja ..na hata wanapotembelea vijiji..!

Wakubwa wanapokutana. Marekani na Japani ni mataifa yanayoongoza duniani kwa kuwa na chumi kubwa. Katika meza kama hiyo ni kama wenye dunia yao ya kiuchumi wanapokutana.

Pale Raisi Obama alipokwenda kwenye kasri la kifalme kumuona Mfalme Akihito na Malkia Michiko wa Japani. Kwa wajapani hawa ni watu wenye hadhi kubwa kuliko maelezo. Historia inaonyesha kuwa zamaani walikuwa wakiabudiwa kama miungu ya wajapani. Sasa mambo yamebadilika kidogo.Na kwa kukudokeza tu Wajapani huwa hawataji jina lake hadharani na hata kuliandika katika maandishi rasmi huishia tu..mtukufu Mfalme! ni tamaduni na mila za Wajapani!

0 comments: