Miaka 17 iliyopita , Toshikazu Sugaya akiwa na miaka 45 wakati huo alikamatwa na Polisi akituhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto mdogo wa miaka minne, mwaka 1990 wakati huo akiwa anafanya kazi wa kuendesha basi la shule. Amekaa jela kizuizini miaka 17 na mwanzoni mwa mwezi huu Polisi walikiri kuwa kwa kutumia utambuzi wa vinasaba yaani DNA mtu huyo hakuhusika na mauaji hayo na ikaamua kuwa aachiliwe na Mahakama kuu ya Tokyo inatarajiwa kuidhinisha uamuzi huo wiki ijayo.
Mtu huyo amekuwa akionana na waandishi wa habari kuelezea yaliyomkuta na Jana jumatano alikutana na RPC wa Tochigi hapa Japani , Shoichiro Ishikawa ambaye alimuomba radhi na wakati wote huo wakili wake alikuwa akihaha kuthibitisha kuwa hakuhusika kabisa.
“Naomba radhi kutoka ndani ya moyo wangu kwa kukuweka katika hali ngumu kiasi hicho kwa kipindi kirefu”, alisikika Ishikawa akimwambia Toshikazu Sugaya ambaye sasa ana umri wa miaka 62 aliyekuwa akilengwa lengwa na machozi katika makao makuu ya polisi mkoa. Mwendesha mashitaka mwandamizi naye alionyesha masikitiko yake , majuto na kuomba msamaha jambo si maneno ya moja kwa moja.
Kama zilivyo tamaduni za kijapani Sugaya aliinamisha kichwa mara mbili wakati akikubali kusamehe yaliyotokea na baadaye aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri kuwa “ nimewasamehe tangu pale nilipowaona kwa dhati kabisa wakiniomba radhi na kwamba msamaha wake pia unawahusu wapelelezi na waendesha mashitaka “.Wakati huo huo Meya wa jiji la Ashikaga Minoru Omamiuda anaangalia uwezekano wa kujitolea kumpa makazi kama atapenda kuishi hapo. Inaonyesha kiwango cha uadilifu katika upelelezi, uendeshaji mashitaka na utu...Tuige basi kama tunaweza.
Kwetu Bongo inawezekana?
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, June 17, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment