Wezi wanne waliotuhumiwa kuwaibia watu simu na bunduki nchini Somalia wamekatwa mikono ya kulia na miguu ya kushoto mbele ya umati wa watu 200 mjini Mogadishu.Mahakama ya kiislamu inayoendeshwa na wanagambo wa kundi la Shebbab linalotawala sehemu ya Mogadishu liliwahukumu vijana wanne kukatwa miguu yao ya kushoto na mikono ya kulia baada kuwaona wana hatia ya kuwaibia simu na bunduki wakazi wa Mogadishu.Vijana hao walikuwa wakatwe mikono yao ya kulia na miguu ya kushoto siku ya jumatatu lakini kutokana na kwamba siku hiyo kulikuwa na joto sana ilihofiwa kwamba mejaraha ambayo wezi hao wangebakia nayo yangehatarisha maisha yao na hivyo kufanya hukumu hiyo iahirishwe."Hukumu imefanyika kama ilivyopangwa" alisema afisa mmoja wa Shebabb ambaye hakutaka jina lake. "Kwa mujibu wa sheria za kiislamu, mtu yoyote anayewaibia watu huadhibiwa adhabu kama hii" alisema afisa huyo alipokuwa akiongea na shirika la habari la AFP.Wakazi wa kitongoji cha Sukahola walikusanyika kwenye eneo la wazi kushuhudia vijana hao wakiadhibiwa lakini simu na kamera zilikuwa haziruhusiwi eneo hilo.
Wanamgambo wawili wa Shebbab waliokuwa wameficha sura zao waliwakata vijana hao miguu na mikono yao kwa kutumia mabisu makali ya kisomali yanyoitwa "torey"."Kabla hukumu haijatekelezwa, madaktari waliangalia afya zao, tulitaka kuepuka kitu chochote ambacho kingeyaweka maisha yao hatarini" alisema afisa mmoja wa Shebbab.
Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea jinsi wezi hao walivyokuwa wakilia kwa kelele huku wakivuja damu wakati wanamgambo walipokuwa wakiwakata viungo vyao.
"Haikuchukua muda mrefu, ndani ya dakika tatu niliwaona tayari hawana mikono ya kulia na miguu ya kushoto" alisema Ali Mohamed mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyeshuhudia tukio hilo."Baadhi ya watu walishindwa kuwaangalia na kuangalia pembeni wakati hukumu ilipokuwa ikitekelezwa. Ni kweli ni adhabu yenye maumivu makali sana lakini nataka adhabu hii iendelee ili kutokomeza wezi eneo hili" alisema mkazi mwingine wa eneo hilo Farah Mohamed.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, June 26, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment