Usikilizaji wa muziki huweza kuwasaidia wagonjwa walio na matatizo sugu ya mkandamizo wa mawazo (stress) na tiba ya kiwango fulani kwa maradhi ya moyo pale mishipa ya moyo inapoelekea kuziba. Utafiti wa kitiba uliofanyika nchini Marekani umebaini kuwa kusikiliza muziki uliotulia unaweza kupunguza ongezeko la msukumo mkubwa wa damu na kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wa moyo.
Wataalamu hao wanasema kuwa kuishi huku ukiwa na matatizo ya moyo ni jambo linalosumbua sana kwahiyo hali hiyo inahitaji tiba mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri wa matumzi ya vyakula, vinywaji , lakini pia kuufanya ubongo usipate mkandamizo bila sababu.
Lakini hata hivyo Dr. Joke Bradt wa kituo cha sanaa na ubora wa maisha katika kituo cha utafiti wa kitiba katika Chuo Kikuu huko Philadelphia nchini Marekani anasema ‘majaribio yaliyokwisha fanyika ni machache na hasa aina ya muziki unaofaa ni kwamba usikilizwe kwa muda gani na kwamba bado wanalifanyia kazi suala hilo. Tafiti zilizokwisha fanyika ni 23 kwa wagonjwa 1,461 kwa kuwapatia muziki maalum uliorekodiwa na kuungwa katika mishipa , na kazi hiyo hufanywa na wataalamu mabingwa wa masuala ya maradhi ya moyo na sanaa.
Tayari wanamuziki duniani kila mtu anakuna kichwa kufikiria kitu gani atunge na kukiweka katika muziki mororo ili uteuliwe kuwa ‘dawa’ na bila shaka atakuwa billionea ghafla. Penda kusikiliza muziki laini unapojikuta umetindikiwa na mawazo kibao…
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, June 17, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment