Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, October 30, 2011

Kijana mmoja raia wa Kenya Elgiva Bwire Oliacha amehukumiwa na mahakama moja ya jijini Nairobi kifungo cha maisha baada ya kumtia hatiani kufuatia kukiri kwake kuwa yeye ni mfuasi wa al shabaab na aliyetekeleza shambulizi la gureneti kwenye kituo cha mabasi mapema wiki hii.

Elgiva Bwire Oliacha kwa jina jingine Mohammed Seif(pichani juu) alikiri kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 20 baada ya kuwarushia guruneti.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu mkaazi Grace Macharia, alisema mahakama imeridhika kuwa alipanga kuwaua watu wengi na lazima apewe adabu kali.
"Ili iwefunzo kwa watu wengine wenye nia kama yako, mahakama imeona vyema itoe kifungo hicho cha maisha kuwazuia kupanga harakati kama zako" alisema Hakimu Macharia.

Bw Bwire pia atatumikia kifungo cha miaka 15 kwa kuwa mwanachama wa kundi la al -shabaab ambalo limepigwa marufuku nchini Kenya na miaka mengine 7 kwa kupatikana na silaha bila kibali.
Mama yake mzazi anasemaje lakini!!!!!?

0 comments: