Serikali za Kenya na Somalia zimekubaliana kushirikiana ili kuwaangamiza wanamgambo wa Kisomali wa Al-shabab.
Mkutano ulifanyika jana jumanne mjini Mogadishu na kuwakutanisha Waziri wa mambo ya nje Moses Wetang’ula na wa ulinzi Yusufu Haji wa Kenya na Raisi wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed pamoja na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed na kwa pamoja walikubaliana kufanya mashambulizi makali dhidi ya al-Shabab.
Wakati mkutano huo ukiendelea , bomu limeripuka nje ya makao makuu ya zamani ya wizara ya mambo ya nje ya Somalia kujilipua .
Majeshi ya Kenya yameingia ndani ya Somalia eneo la Afmadow lililopo kilometa 120 ndani ya Somalia.
Hali ndio hiyo!...
Wakati huo huo.. Maafisa wa Ufaransa wametangaza kuwa mama raia wa kifaransa aliyetekwa nyara kutoka Kenya na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kisomali wa al Shabab mapema mwezi huu amefariki.Maafisa wa kibalozi wanasema walifahamishwa kifo cha Marie Dedieu na watu ambao wamekuwa wakijaribu kuzungumza na watekaji nyara ili wamuachie huru mama huyo. Haijulikani alikufa lini na nini kilichosababisha kifo chake, ingawa inakumbukwa kuwa afya yake ilikuwa dhaifu na kuwa hakuruhusiwa kutumia dawa,na kwamba tukio kama hili lilitarajiwa.
Bi. Dedieu mwenye umri wa miaka 66 ni mmoja wa wageni kutoka mataifa ya magharibi waliotekwa kutoka Kenya mwezi October.Mwezi September raia kutoka Uingereza David Tebbutt aliuawa na mke wake Judith kutekwa katika hoteli moja ya kifahari huko Kiwayu pwani ya Kenya.Na mwezi jana wanawake wawili raia wa Uhispania wafanyakazi wa misaada walitekwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.Wanawake wote watatu waliotekwa bado hawajulikani walipo.
Somalia imekabiliwa na mapigano ya mwenyewe kwa wenyewe kwa miongo miwili, hili limesababisha silaha kupatikana kwa urahisi na kuna makundi mengi ya watu wenyewe silaha ambao pia wanaweza kuwa walihusika na utekaji huo.
Al-Shabab wamekanusha kuhusika na utekaji nyara wowote na wameonya kuishambulia Kenya ikiwa wanajeshi wake hawataondoka. Tusubiri tuone hatima ya Kenya kuivamia Somalia!
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, October 19, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment