Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, October 23, 2011

Polisi katika jiji la Suita, Osaka hapa Japani wamesema kuwa wamemkamata mwanamme mmoja akituhumiwa kuvunja sheria ya unyanyasaji dhidi ya watoto baada ya kusemekana kuwa alimlazimisha mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 11 kuomba katika mitaa ya Suita , Osaka.

Habari iliyoandikwa na moja ya magazeti ya hapa inaeleza kuwa kuwa baba huyo anayefanya kazi ya ujenzi mwenye umri wa miaka 33alimwambia mwanawe akae kando ya barabara na awaambie wapita njia kuwa amepoteza pochi yake na bila shaka wangemuonea huruma na kumpatia fedha.Baada ya Polisi kumkamata kijana huyo ,aliwaambia kuwa alikuwa akifanya hivyo mara tano hadi sita kwa siku na alikuwa akipata takriban Yeni 2000 kwa siku (zaidi ya elfu 40 za Tz) ambazo alimpa baba yake.
Hatua iliyofuata ilikuwa ni kumkamata baba wa mtoto huyo ambaye alikutwa pembeni mwa bustani moja akisubiri mwanawe kukusanya pesa na ndio alipodakwa.
Alipohojiwa baba wa mtoto huyo alikana kumwambia mwanawe aombe, na kwamba anahisi ilikuwa ni mapenzi yake tu kufanya hivyo!...Bila shaka atafikishwa mahakamani akituhumiwa kukiuka haki za mtoto na kusababisha usumbufu kwa watu wengine...

0 comments: