Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, October 17, 2011

Wanajeshi wa Kenya wamevuka mpaka na kuingia Somalia kuwasaka wapiganaji wa kiislamu wa Al-Shabaab, ambao wanawalaumu kwa utekaji nyara wa wageni kadha katika ardhi ya Kenya.

Hii inafuatia na tukio moja ambapow wafanyakazi wawili kutoka Uspania wa Shirika la msaada la kimataifa, walitekwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab siku ya Alkhamisi, na wanawake wengine wawili walitekwa karibu na Lamu, mwambao wa Kenya, na inaaminiwa wamepelekwa Somalia. BBC ilisema kuwa wanajeshi wa Kenya waliingia Somalia Jumapili asubuhi na kwamba wanajeshi hao wa Kenya wakiwa na vifaru wameingia hadi kilomita 90 ndani ya Somalia.

Taarifa kutoka Liboi, kaskazini mwa Kenya,zinabainisha kuwa wanajeshi walionekana wakielekea Somalia.Hatua hiyo inafuata baada ya Waziri wa Usalama wa Kenya, George Saitoti kusema kuwa Kenya itachukua hatua yoyote kudhibiti mipaka na usalama wake, baada ya wanawake wawili wa shirika la msaada la kimataifa, kutekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab-BBC

0 comments: