Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, January 13, 2010

Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 limeikumba haiti saa chache zilizopita na na maelfu ya watu inasemekana wamekwama kwenye vifusi wengi wakiwa hai bado. Operesheni kubwa inaendelea kuwaokoa maelfu ya watu waliozikwa hai na vifusi vya majumba kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti ambalo halijawahi kutokea katika visiwa vya Caribbean.
Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 lilibomoa hospitali na majumba katika mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince na kusababisha maafa makubwa huku kila mtu aliyesalimika akihaha kumuokoa ndugu yake au ndugu zake waliofunikwa na vifusi.
Mamia ya watu wapo chini ya vifusi wakipiga kelele za kuomba msaada.
Tafadhali baadhi ya picha humu ndani ni zaa kutisha kidogo ...jiandae kisaikolojia... Unaweza kukadiria mtikisiko ulivyokuwa!...
Miili ya watu ikiwa imezagaa katika mji huo ambao mawasiliano ya simu yamekatika.
Matrekta yalionekana mitaani yakisaidia kufukua vifusi vya majumba mbali mbali yakiwemo makazi ya wanadiplomasia na wafanyakazi wa umoja wa mataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema Marekani tayari imeanza kutuma misaada ya dharura na Raisi Obama ametoa hotuba ya Pole kwa wa-Haiti.Wanajiolojia nchini Marekani wanasema tetemeko hilo la ardhi ndilo mbaya zaidi kwahi kuikumba Haiti kwa miaka mia mbili. Wataalamu hao pia wametoa tahadhari ya Tsunami.
Hali inapofikia hapo!

0 comments: