Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 24, 2010

Hokkaido kaskazini kabisa mwa Japani ilivyo hivi sasa.
Mwanamke mmoja mtu mzima alikutwa amekufa katika eneo la wazi katika jiji la Sapporo nchini Japani akiwa amefunikwa na theluji na polisi wanasema kuwa alionekana akiwa na majeraha katika mwili wake.Watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo waliuona mwili wa mwanake huyo mwenye miaka 72 katika eneo la Kita saa nane mchana na kuita Polisi. Mwili huo ulikuwa umefunikwa kwa theluji kwa maki ya sentimenta 10 .
Mwanamke huyo anaaminika kuwa ni mwenyeji wa maeneo hayo na kwamba alipotea siku nne zilizopita na familia yake pamoja na polisi walikuwa wakifanya jitihada za kumtafuta.
Kamera za ulizi katika eneo hilo zinamuonyesha mama anayefanana na huyo akiingia katika duka la jirani alfajiti ya saa 11 na nusu siku hiyo aliyopotea na upelelezi unaendelea. Bila shaka kuwepo kwa kamera katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Japani inarahisisha sana masuala ya upelelezi. Agharab kila unapopita sura yako hubaki kwenye kamera na polisi huzitumia kuunganisha mwenendo wako wa siku.

0 comments: