Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, January 22, 2010

Barani Yuropa hivi sasa kuna kibaridi kikali ile mbaya. Eeeh kibaridi hiki lawama mkubwa au nadanganya! Kibaridi kimekolea..
Pale taa za barabarani zinapozongwa na kibarafu... Maji yanapozidi unga...inabidi uvae nyenzo
Hapa Tokyo kibaridi nacho kinavuta kasi leo kimefikia digrii 7 . Kumetulia lakini kinapuliza. Hapo ni bustanini karibu na jengo la Matangazo NHK . Wajapani wanatunza mazingira , ukiwa ndani ya bustani hiyo utadhani uko Ngorongoro. Wanyama tu wakali hawapo ni vijindege na vijisungura!

0 comments: